(NA
VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO)
DAR
ES SALAAM
Haraiki ya wanafunzi wapatao 1,727 kutoka shule za msingi mbalimbali Tanzania bara na visiwani wameipamba vizuri sherehe ya maadhimisho ya
miaka 48 ya Muungano wa Tanzania
yaliyofanyika leo katika viwanja vya Uhuru
jijini Dar es Salaam.
Kati ya wanafunzi hao, ni
wanafunzi 727 ambapo 500 wanatoka Tanzania bara, 200 Tanzania visiwani na 27 ni
mahodari wa kucheza sarakasi ambao waliingia uwanjani na kutengeneza maumbo
mbalimbali pamoja na kuimba wimbo maalumu uitwao Uamuzi wa Busara.
Maumbo yaliyotengenezwa na
haraiki hiyo ni pomoja na bendera ya taifa, herufi zenye umbo la miaka 48 ya Muungano, na maumbo
ambayo ndani yake walicheza salakasi na ngoma za asili za ndalandala kutoka Tanzania bara na chaso kutoka Zanzibar.
Maumbo mengine ni pamoja na
madini ya Tanzanaiti ambayo hayapatikani sehemu yoyote duniani zaidi ya Tanzania na maumbo ya mazao ya uchumi ya katani
na pamba yanayolimwa Tanzania
bara na karafuu Tanzania
visiwani.
Haraiki hiyo imeandaliwa na
ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na
wakufunzi wake ni Kilema Athuman Kambangwa akisaidiwa na Mwalimu Grace Ernest
Kabohora kutoka shule ya msingi Wailesi katika manispaa ya Temeke.
Katika maadhimisho hayo Mgeni
rasmi alikuwa ni Rasi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
na kauli mbiu ni “Shiriki kikamilifu katika Sensa na mchakato wa Mabadiriko ya
Katiba”.(Mwandishi Shaaban Mpalule)
RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WANANCHI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MUUNGANO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipunga
mkono kusalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam leo Aprili 26, 2012 katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya
Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akiingia katika
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuongoza maadhimisho ya mika 48 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo asubuhi (Picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipowasili katika uwanja wa
Uhuru kuongoza sherehe za Muungano zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya miaka
48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam leo (Picha na Freddy Maro)
Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa
waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa
kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa
waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa
kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili
26, 2012 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa
Tanganyika na Zanzibar.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa
kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo
leo.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa
kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo
leo.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa
kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo
leo.
Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha alaiki,
wakionyesha manjonjo ya michezo na maumbo mbalimbali wakati wa sherehe
hizo leo.
Kikundi cha Sanaa cha JKT Oljoro, kikionyesha umahiri wake wa kuimba na kucheza 'Kiduku' wakati wa sherehe hizo.