DKT. KASHILILAH AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA BUNGE LA ISRAEL
MANYARA YAPITISHA BAJETI YAKE
Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera Na Woinde Shizza,manyara
Mkoa wa Manyara unatarajia kutumia sh202.1 bilioni kwa ajili ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017, ambapo mishahara itakuwa ni sh5.5 bilioni, matumizi ya kawaida sh2.1 bilioni na sh2.7 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Katika mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 mkoa umekadiriwa kukusanya mapato ya ndani ya sh18 bilioni ambapo sh17.9 bilioni ni kwa ajili ya serikali za mitaa na sh192 milioni ni za sekretarieti ya mkoa.
Akisoma mpango wa bajeti ya mkoa huo juzi, Katibu Tawala wa mkoa huo Eliakim Maswi alisema kijiografia Manyara yenye kilomita za mraba 50,921 ni kubwa kuliko baadhi ya mikoa, hivyo inahitaji gharama kubwa za uendeshaji.
Maswi alisema katika mpango huo wa bajeti, Babati mjini wanatarajia kutumia sh25 bilioni, Babati vijijini sh37 bilioni, Hanang’ sh33 bilioni, Kiteto sh30 bilioni, Mbulu vijijini sh38 bilioni, Mbulu mjini sh6 bilioni na Simanjiro sh19 bilioni. “Pia tunakabiliwa na changamoto ya kuchelewa au kutopatikana kwa fedha za ruzuku za matumizi ya kawaida na ruzuku ya miradi ya maendeleo, ufinyu wa bajeti wa kuboresha na kujenga miundombinu ya zahanati na shule,” alisema.
Alisema umbali kutoka makao makuu ya halmashauri ya wilaya hadi makao makuu ya mkoa ambapo ni lazima upitie wilaya nyingine kama Kondoa, Monduli na Arusha ili ufike mkoani wakati wa kufuata huduma mkoani pia ni kikwazo.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa huo Dk Joel Bendera alizitaka halmashauri zote saba kuhakikisha zinachangia bajeti zao kwa asilimia 60 ya mapato ya vyanzo vya ndani kama serikali kuu ilivyoagiza ili kutekeleza miradi ya maendeleo yao.
NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JNIA
Mkuu
wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Abuu Mvano (kulia), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), alipotembelea
Idara za Wizara hiyo zilizopo katika Uwanja huo. (Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliopo katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waandishi wa Habari
wakati wa ziara yake aliyoifanya kutembelea Idara za Wizara hiyo
zilizomo katika Uwanja huo.
Wakimbizi Kigoma waadhimisha Siku ya Maji Duniani
Tangu
kufunguliwa tena kwa makambi hayo mwaka jana, mashirika mbalimbali
yamekuwa yakitoa misaada ya kibinadamu katika makambi likiwemo shirika
la Oxfam ambalo linatoa huduma za maji na ujenzi wa vyoo ikiwa ni pamoja
na kuwafundisha wakimbizi namna mbalimbali za kuishi kwa kuzingatia
kanuni bora za afya ili kujilinda dhidi ya magonjwa.



Meneja
wa bidhaa wa Samsung,Rayton Kwembe(kushoto) Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu, Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom
Tanzania,Samson Charles, Meneja masoko wa Samsung,Tulisindo
Mwachula,wakionesha simu aina ya Galax S7 na S7 Edge kwa waandishi wa
habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu hizo ambazo haziingizi
maji ulifanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar
es Salaam.
















Baadhi
ya washiriki wakiifuatilia uzinduzi huo wa ugawaji wa fedha za Mikopo
ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa
hiyo ya Kinondoni mapema leo
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya
hundi hiyo zilizozinduliwa rasmi wa ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko
wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya
Kinondoni mapema leo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo
No comments:
Post a Comment