Kikosi cha Timu ya Raha Leo
Kikosi cha Timu ya Mtanda
Mkuu
wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga (Kushoto) Akiwa na
Mgeni Rasmi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, R.P.C Renatha Mzinga,
wakati wa Uzinduzi wa Michuano ya Kombe la R.P.C CUP LINDI 2016, kwenye
Uwanja wa Ilulu Mkoa wa Lindi tarehe 28/7/2016. Fainali ya Michuano ni
25/8/2016 katika Uwanja huo.(Picha Zote na Fungwa Kilonzo)
Mkurugenzi
wa Mashujaa Fm Radio, na Mratibu wa Michezo ya R.P.C CUP LINDI 2016,
Shaaban Mpalule, akiwagawia Mashabiki Furana mbali mbali za G.S.M na
T-Mark Tanzania, wakati wa Uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Mashujaa Fm Radio, na Mratibu wa Michezo ya R.P.C CUP
LINDI 2016, Shaaban Mpalule, akiwagawia Mashabiki Furana mbali mbali
za G.S.M na T-Mark Tanzania, wakati wa Uzinduzi huo.
Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
===================================
-R.P.C RENATAHA MZINGA AZINDUA KWA MBWEMBWE.
-DC LINDI AIPONGEZA KAMPUNI YA GSM
-MASHABIKI WATAKA GSM IFANYE MICHEZO HIYO KILA MWAKA.
Na: Mwandishi wa Miss Demokrasia Tanzania.
Kampuni
ya GSM Tanzania, wauzaji wa Pikipiki za GSM na Magodoro ya kisasa ya GSM, leo jumatano
28/7/2016 imekamilisha uzinduzi wa Michuano ya Kombe la R.P C Cup LINDI 2016, ambayo
lengo lake ni kuwaweka Vijana karibu na Jeshi la Polisi pamoja na kuwapa Elimu
mbali mbali Madereva kuhusiana na Usalama barabarani ususani vijana waendesha
Bodaboda na ilianza 13/7/2016 kwenye Uwanja wa Ilulu.
katika
uzinduzi huo GSM ambao ni wadhamini wa Jumla katika michezo hiyo kwa Upande wa
Jeshi la Polisi katika mikoa ya Lindi, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na
Dodoma, ilipongezwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga
kwa kuweza kujitokeza kusaidia mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa
mkiwango kisichoridhisha ikiwa ni pamoja na kukosekana na vifaa vya michezo
pamoja na furana kwa Wageni mbali mbali.
Aidha wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo Kamanda wa polisi Mkoa wa
Lindi, Afande R.P.C Renatha Mzinga, alisema kuwa wanaishikuru Kampuni GSM kwa
mwaka huu kujitokeza kusaidia michezo hiyo ambayo hata hivyo bado kuna upungufu
wa vifaa mbali mbali vya michezo ikiwemo mipira ya kuchezea.
"Mashindano ya Mwaka huu ni Mazuri na yameonyesha kuwa tofauti na miaka ya
nyuma, pengine ni kwa kuwa yamejitokeza makampuni kama hawa GSM, Halotel na BIG
BON, kwa kweli kunachangamoto nyingi sana kwenye hii michezo, na hata timu za
mwaka huu zimeonekana kujiandaa vizuri kwa ajili ya kuwania zawadi siku ya
Fainali, Niwapongeze wadhamini wote waliojitokeza kusaidia kwa namna moja na
nyingine, kile kidogo walichotupatia kwetu ni kikubwa sana, kwa maana
kimeonekana kuleta utofauti na miaka ya nyuma, hivyo nichukue fulsa hii
kuwaomba hawa wadhamini kuweza kukumbuka kutusaidia kwenye hii hatua ya mwisho
ambapo inaonekana vifaa bado havijatimia kama hii Mipira, Sare za Waamuzi na
Zawadi zingine kwa ajili ya Timu, pamoja na kwamba tumepata vikombe lakini
tunatakiwa pia kuwapa zawadi zingine ili kuonyesha tofauti ya mwaka huu na
miaka ya nyuma, niwashukuru GSM kwani hawa wamejitokeza hatua za mwisho mwsiho
lakini wametuwezesha leo kupendeza uwanjani, mashabiki wamevalia na watu mbali
mbali furana zao, kwa kweli ninawapongeza sana, wasiishie mwaka huu tu bali
wayachukue na kuyafanya mashindano kuwa ni ya kwao kila mwaka" alisema
R.P.C Renatha Mzinga.
Aidha
michuano hiyo imezidi kushika kasi na kufikia jumla ya michezo 27 ambayo tayari
imechezwa katika kuwania kinyang’anyoro cha ubingwa mwaka huu.
Wachezaji wa timu mbali mbali
wamezidi kuonyesha uwezo mkubwa katika michuano hiyo ambayo inashirikisha
jumla ya timu 18 kutoka kata zote za Mkoa wa Lindi.
Katika hatua hii michezo ambayo
imechezwa na matokeo ni kama ifuatvyo, Mtanda A imefanikiwa kuifunga Mitandi
kwa 1-0, Matopeni 1-0 Wailes, Mnazi mmoja 2-0 Mbanja, Nachingwe 0-0 Msinjaili,
Rahaleo 2-1 Mtanda B, Rasibula 2-1 Tandangongoro, Mingoyo3-0 Chikonji, Mtandi
5-1 Kitumbikwela, Makonde 5-0 Mikumbi, Polisi 1-1 Matopeni, Mnazi Mmoja 4-1
Mtanda A, Msinjaili 8-0 Wailes, Mtanda(B) 2-1 Mbanja, Rahaleo 2-0 Chikonji,
Rasibula 2-0 Nachingwea, Mikumbi 2-0 Tandangongoro.
MIchezo mingine ni Mingoyo
0-Kitumbikwela. Makonde 1-0 Polisi, Mitandi 1-1 Mnazi Mmoja, MAtopeni 3-0
Msinjahili, Mtanda(A)1-1 Mbanja, Wailes 2-5 Nachingwea, Kitumbikwela 3-4
Chikonji, Polisi 0-1 Mikumbi, Mnazi MMoja 0-0 Mingoyo, Msinjahili 0-3 Makonde,
Mitandi 2-0 Mbaja, MAtopeni 2-2 Nachingwea, na Mtanda 2-3 Raha Leo.
Michezo hiyo inaendelea tena kesho(leo) ambapo Wailes wataikaribisha timu ya
Tandangomgoro katika mchezo wa kwanza na mchezo wa pili Mtanda (B)
wataikaribisha Kitumbikwela kwenye mchezo wa pili majira ya saa kumi jioni.
mashindano yameendelea kuwa kuvutio
kikubwa kwa wakazi wa mkoa wa lindi kutokana na wenyeji kujitokeza
kuzishangilia timu za kata zao ambazo zinawania uchampioni huo wa kombe la
R.P.C Renatha Mzinga.
Zawadi ambazo mpaka sasa zimetolewa na GSM ni pamoja na Filimbi, Stopwatch,
Soksi, Mabegi, Kofia, Sare na Viatu kwa ajili ya Waamzuzi, pamoja na
zawadi ya Soksi kwa Wachezaji ambao wanafanikiwa kufunga magoli matatu katika
mechi moja, ambapo badala ya kuondoka na mpira umewekwa utaratibu wa
kuwazawadia Soksi kila anapotokea mchezaji amefunga mabao matatu.
Kiasi cha Shilingi Milioni Mbili tayari Kimetumika Mpaka sasa kutoka Kampuni ya
GSM ambazo zimetumika kulipa Posho za Waandishi wa Habari wanaoendelea kuripoti
matukio hayo kila siku na zingine zimesaidia kununua vifaa hivyo kwa ajili ya
Waamuzi na zawadi za kila siku kwa wachezaji.
katika kiasi hicho kutoka GSM pia kimesaidia kununua Filimbi na Stop Watch kwa
ajili ya Makocha wa Timu zote zinazoshiriki ligi hiyo ya R.P.C CUP LINDI mwaka
huu.
katika hatua nyingine kampuni ya T-Mark Tanzania ambao pia ni miongoni mwa
wawezeshaji wadogo wameweza kusaidia Furana za kwa ajili ya Vikundi vya
Uhamasishaji.
Kilele cha Michuano hiyo ni tarehe 25 ya mwezi wa nane ambayo itakuwa siku ya
kilele cha siku ya Polisi Day.
Mashindano haya yanaandaliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Afande R.P.C
Renatha Mzinga kwa ushirikiano na Mashujaa Fm Radio chini ya Wadhamini Wakuu Big
Bon na GSM Wauzaji wa Pikipiki za GSM na Magodoro ya GSM,wadhamini wadogo ni
CxC Tours & Safaris, Halotel, T-Marc Tanzania, Mkuu wa Wilaya ya Lindi
Shaibu Issa Ndemanga, Miss Demokrasia Tanzania, MPALULEBLOGS: na Pimak Limited.
Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
Mkurugenzi wa Mashujaa Fm Radio, na Mratibu wa Michezo ya R.P.C CUP
LINDI 2016, Shaaban Mpalule, akiwagawia Mashabiki Furana mbali mbali
za G.S.M na T-Mark Tanzania, wakati wa Uzinduzi huo.
Kikosi cha Timu ya Kata ya Raha Leo, Kikishangilia Bao la kwanza
DJ'S Machachali, Dj Kizo, akifanya Vitu vyake wakati wa Uzinduzi huo
Wakati wa Mapumziko
Mashabiki wakiwa wamejificha kivuli kwenye Miamvuli ya GSM wakati mchezo ukiendelea
Watoto ambao ni wakeleketwa wa Soka na Wajanja wa G.S.M wakifurahia
Vipeperushi vyenye Nembo ya Bidhaa za G.S.M, kama Piki Piki na Bidhaa
Zingine, Vipeperushi vilivyogawiwa kwa Mashabiki Wote UWanjani humo.
Kikundi
cha Ushangiliaji (Vijana) ambao walionyesha Staili ya Pekee katika
Kushangilia kwa Kuvaa Nguo za Kike, maarufu kama Dela ambazo
ziliwaonyesha kana kwamba wao ni Watoto wa Kike, waliokuwa wakizunguka
Uwanja huku wakionyesha Mbwembwe ikiwemo kutikisa Nyonga, Viuno, na
Vidole Juu, na kuwaacha MAshabiki kwa Vifijo, nderemo na Kelele za Mara
kwa Mara kwa kile walichokuwa wakifanya Vijana hao wakati wote wa
Mchezo, aikujulikana walikuwa mashabiki wa Timu gani.
Majukwa yakionyesha utulivu wakati wote wa mpambano
Timu zikiendelea kuchuana kusaka pointi tatu Muhimu
Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu wakifuatilia kwa Makini Mpambano huo huku wakivalia Furana za GSM
Paparazi akiwa kazini
Watu wa Huduma ya Kwanza (First AID) wakiwa eneo la Uwanja huo
Rahaleo wakishangilia Bao la Pili
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa
Ndemanga,(kushoto) na KAmanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, R.P.C Renatha Mzinga, wakifuatilia kwa makini Mpambano huo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, R.P.C Renatha Mzinga, akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa
Ndemanga, Muda Mfupi kabla ya Uzinduzi huo