Saturday, December 29, 2012
Tanzania haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia ya utandawazi duniani
Naibu
katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua Warsha
kwa maafisa wa mipakani kuhusu usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo
na Bioteknolojia ya kisasa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Julius Ningu na kushoto ni Afisa Mazingira
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Esta Makwaia. Warsha hii imefanyika leo
kwenye Hotel ya La kairo jijini Mwanza
Washiriki
wa Warsha ya Usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia
ya kisasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi (katikati) Mara
baada ya kufungua warsha hiyo kwenye Hoteli ya La kairo Jiji Mwanza
…………………………………………….
Lulu Mussa na Ali Meja
Mwanza
Imeelezwa kuwa Tanzania kama nchi
nyingine haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia kutokana na
utandawazi na maendeleo duniani kote, kwa kuwa bioteknolojia ya kisasa
ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini, kuboresha
kilimo, uzalishaji viwandani, afya na hifadhi ya mazingira.
Hayo yamesemwa leo na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava katika warsha ya
siku moja kwa maafisa wa mipakani kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, warsha
iliyolenga kukuza uelewa kwa watendaji wanaosimamia mazao na bidhaa
zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa.
Amesema, Serikali kwa kutambua
mchango mkubwa unaoweza kupatikana kutokana na matumizi ya bioteknolojia
ya kisasa katika sekta za afya, kilimo, viwanda na mazingira, imeridhia
Itifaki ya Cartagena ya Mkataba wa Bioanuai mwaka 2003 kwa lengo la
kuhifadhi mazingira kwa kuzingatia usalama katika usafirishaji, kuunda
na kupitisha mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa matumizi salama ya
Bioteknolojia mwaka 2007.
Eng. Mwihava amewaasa watendaji
katika maeneo ya mipakani kuwa na usimamizi madhubuti katika maeneo yao
ya kazi kwa kuwa mipaka kati ya Tanzania na nchi nyingine ndiyo njia kuu
za uingizaji wa mazao na bidhaa zitokazo nje.
Pamoja na faida za bioteknolojia
hiyo ya kisasa Eng. Mwihava amewataka watendaji hao kuwa makini na
athari zinazoweza kutokana na matumizi ya teknolojia hiyo pale
itakapotumiwa bila kufuata taratibu za usalama zilizowekwa.
Warsha hii ya siku moja kwa
imewashirikisha maafisa forodha, Maafisa Afya na watafiti wa Mazao
kutoka Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera, kutoka Idara , wakala za
Serikali na sekta binafsi.
Waziri mukangara akagua vikundi vilivyopata mkopo wa vijana Bukoba
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akiangalia kahawa katika shamba darasa inayolimwa na Ibrahim
Mulokozi (kulia) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ibwera wilayani Bukoba
aliyenufaika na mkopo wa shilingi laki nne kutoka mfuko wa maendeleo ya
vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea shamba hilo la kahawa na
migomba jana ili kuona fedha za mkopo walizozipata vijana kutoka SACCOS
ya Ibwera zimewanufaishaje kimaisha.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akimuangalia samaki mwenye umri wa miezi mitatu anayefugwa
katika bwawa la Kikundi cha Msifuni kilichopo kijiji cha Kemondo
wilayani Bukoba ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya
vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea bwawa hilo jana ili kuona
fedha za mkopo walizozipata vijana kupitia mfuko wa Halmashauri
nimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa tatu
kulia) akiangalia jana nyavu za kuvulia samaki za Kikundi cha Msifuni
kilichopo katika kijiji cha Kemondo wilayani Bukoba ambacho kilipata
mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na kuanzisha mradi wa bwawa la
samaki. Kushoto ni Katibu wa kikundi hicho Johanes Joel.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akipokea taarifa ya SACCOS ya Ibwera iliyopo wilayani Bukoba
kutoka kwa Benedicta Peter ambaye ni katibu msaidizi. SACCOS hiyo
ilipata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wa maendeleo ya
vijana na kuvikopesha vikundi mbalimbali vya maendeleo vya vijana.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa SACCOS ya Ibwera
na viongozi wa wilaya ya Bukoba wakati alipowatembelea jana ili kuona
fedha walizopata kutoka mfuko wa waendeleo ya vijana zilivyoweza
kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
akiangalia shamba darasa la kahawa na migomba la mkazi wa kijiji cha
Ibwera wilayani Bukoba Ibrahim Mulokozi (hayupo pichani) wakati
alipolitembelea jana ili kuona fedha za mkopo wa mfuko wa vijana
alizozipata kupitia SACCOS ya Ibwera zimemnufaishaje kimaisha. Kushoto
ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Serikali yaombwa kuongeza fedha za mkopo wa vijana
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akipokea taarifa ya SACCOS ya Ibwera iliyopo wilayani Bukoba
kutoka kwa Benedicta Peter ambaye ni katibu msaidizi. SACCOS hiyo
ilipata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wa maendeleo ya
vijana na kuvikopesha vikundi mbalimbali vya maendeleo vya vijana.
……………………………………………………….
Na Anna Nkinda – Maelezo, Kagera
Serikali imeombwa kuongeza kiasi
cha mkopo kinachotoa kwa vijana kupitia mfuko wa maendeleo wa vijana na
Halmashauri za wilaya kwani kiwango kinachotolewa kwa sasa cha shilingi
milioni tano kwa vyama vya Kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS) ni kidogo
ukilinganisha na mahitaji ya mkopo huo.
Ombi hilo limetolewa jana na
baadhi ya vijana waliopata mkopo huo kupitia SACCOS ya Ibwera na
halmashauri ya wilaya ya Bukoba wakati wakiongea kwa nyakati tofauti na
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
alipotembelea wilaya hiyo ili kuona jinsi fedha hizo zilivyoweza
kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
Vijana hao walisema kuwa fedha za
mkopo walizozipata zimewasaidia kujiinua kiuchumi ikiwa ni pamoja na
kuajiri vijana wenzao, kupanua mitaji ya biashara zao, kulipa karo za
shule za watoto wao na kujikwamua kimaisha tofauti na ilvyokuwa awali
kaba hawajapata mkopo na kufanya shughuli za ujasiriamali.
Kwa upande wake mkazi wa kijiji
cha Ibwera Ibrahim Mulokozi ambaye alipata mkopo wa shilingi laki nne
kupitia SACCOS ya kijiji hicho alisema kuwa ameweza kununua matandazo na
kulipa wasaidizi wanaohudumia shamba lake la migimba na kahawa
ambalo ni la mfano kwa vijana na wazee wanaotoka kata ya Ibwera, Mikoni
na Nyakibimbili na kwenda kujifunza na kuchukua miche ya migomba.
Alisema kuwa anakabiliwa na
changamoto za kutokuwa na fedha za kuendeleza shughuli za kilimo, kutoka
na mbolea ya kutosha ya kurutubisha shamba, bei ya miche ya kahawa
kupanda kutoka shilingi 50 hadi 500 kwa mche mmoja, kuendelea kutumia
jembe la mkono, kutokuwa na masoko ya uhakika hasa soko la ndizi na
magonjwa ya migomba.
Naye katibu wa kikundi cha
Msifuni Johanes Joel ambacho kilipata mkopo wa shilingi milioni moja na
laki tano kutoka Halmashauri ya wilaya ya Bukoba alisema kuwa kikundi
chao kinajishughulisha na kazi ya ukulima wa samaki na walianza na
bwawa moja na hivi sasa wana mabwawa matatu na wanampango wa kuhakikisha
kuwa kila mwanakikundi anakuwa na bwawa lake.
Flightlink yawaandalia chakula cha jioni wafanyakazi wake na familia zao katika kuuaga mwaka
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akizungumza
wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichokuwa kimeandaliwa maalum kwa
ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na
familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.Picha zote na Othman Michuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akiendelea kuzungumza.
Sehemu
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink pamoja na familia zao
wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Munawer
Dhiren (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla
ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana
kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni
sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam jana.
Mazungumzo ya hapa na pale kwa wadau wa Kampuni ya Flightlink yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
Wakati wa Chakula uliwadia na kila mmoja alipita kuchukua chakula akipendacho.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kampuni ya Flightlink wakipozi kwa picha wakati wa
hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya
kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao
ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam jana.
Picha ya pamoja kwa wafanyakazi wote wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink.
Wakurugenzi wa Kampuni ya Flightlink wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)