Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Kombaini ya Makipa( Chama cha Makipa) wakati wa Mapumziko
Na: Mwandishi Wetu.
Kampuni
ya Twiga Cement ya jijini Dar es Salaam, jana imefanikiwa kuzindua
rasmi Chama cha Wachezaji wa Nafasi ya Golikipa wanaoshiriki ligi kuu ya
Vodacom Tanzania, ambapo katika uzinduzi huo timu hiyo ya Makipa
ilicheza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Timu ya Kombaini ya Waandishi wa
Habari TASWA F.C.uliofanyika kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini
Dar es Salaam jana.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa na Ushindani wa Kipekee kutokana na Timu zote
kuwa na Wachezaji Nyota na Tegemeo katika Vipaji vyao, Mashabiki
waliofika kushuhudia mchezo huo walifurahishwa na jinsi kila mchezaji
alivyoonyesha Ujuzi binafsi na kiwango cha hali ya juu.
timu
ya makipa ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufanya shambulizi kwenye lango la
timu ya TASWA ambapo dakika ya 26 mchezaji Shaaban Kado alikosa Penalt
kutokana na beki wa Taswa Martin Peter kunawa akiwa eneo la kumi na nane
na penalt hiyo ilidakwa na kipa nyota wa TASWA Ahmed Famau.
hadi
kipindi cha kwanza kinamalizika kikosi cha timu ya Makipa kilikuwa
mbele kwa bao 1-0,lililofungwa na Juma Kaseja baada ya kutokea piga
nikupige langoni mwa TASWA, ambapo kipindi cha pili kila timu ilifanya
mabadiliko ambapo Taswa iliwatoa, Majuto Omary, Ibrahim Masoud, Ally
Mkongwe, Zahoro Mlanzi, Shafii Dauda, na nafasi zao kuchukuliwa na Salum
Jaba, Juma Ramadhani, Hatibu Naheka,na Paul Limoy,mabadiliko ambayo
hata hivyo yalishindwa kupunguza kasi ya wachezaji hao Makipa wa Ligi
kuu waliokuwa muda wote wakilisakama lango la TASWA FC.
pamoja
na kuwa na wachezaji wa akiba timu ya Makipa lakini walishindwa kufanya
mabadiliko, kutokana na wachezaji wengi kuwa na pumzi ya kuwamudu TASWA
ambapo Makipa hao walisaidiwa na mlinda mlango kutoka timu ya Taifa ya
Wanawake Twiga Stars, Fatuma Omary ambaye hata hivyo alionyesha kiwango
kikubwa baada ya kudaka michomo ya wazi kutoka kwa washambuliaji wa
Taswa,Ibrahim Masoud, Shafii Dauda,Majuto Omary pamoja na Ally Mkongwe
waliokuwa wakilisakama Lango la timu ya makipa kila wakati.
goli la pili lilipatikana kunako dakika ya 67 kupitia kwa Ivo Mapunda aliyefunga kwa shuti kali lililomshinda mlinda wa TASWA Ahmed Famau,kabla ya shaaban Kado kuhitimisha Kapu la Magoli kwa timu hiyo ya Makipa.
Pamoja
na Kufungwa kwa Taabu 3-0 timu ya TASWA FC, iliweza kuwachezesha mputa
mputa wachezaji hao nyota wa Ligi kuu pamoja na kwamba wachezaji hao
muda mwingi wanakuwa kwenye Mazoezi Makali na Timu zao za ligi kuu ya
Vodacom Tanzania Bara,kitendo ambacho kiliwafanya kuonekana wakiwa na
Uhai wa kukimbiza huku na kule katika kipindi cha dakika zote za mchezo.
Taswa
ambayo kwa asilimia kubwa iliwachezesha wachezaji wake wengi ambao ni
wafanyakazi wa vyombo mbali mbali vya habari, ilisifiwa na mashabiki
waliohudhulia mchezo huo kwa kuwa Muda mwingi wanakuwa katika shuguli za
kiofisi ambapo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Timu hiyo wachezaji ukutana
mara moja kwa wiki kwa ajili ya mazoezi ya Pamoja.
"timu
yetu ni nzuri sana hii TASWA, mwenyewe umeona wachezaji walivyowapeleka
mpuata hawa Makipa pamoja na kwamba hii timu ya Makipa ni Wachezaji wa
ligi kuu, nasema ligi kuu kwa kuwa wanashiriki hiyo ligi isipokuwa
tofauti wao ni makipa, na tunapozungumzia suala la Wachezaji, mwenyewe
unajua timu ili iwe bora ni lazima kwanza iwe na Makipa wazuri ndipo iwe
bora, na kipa bora ni yule anayeweza kuwapanga wachezaji wake, hivyo
kama hawa wachezaji ndiyo wapangaji wa timu zao wakati wa Mashindano,
mimi nasema tumecheza na Timu ya Taifa na si kama unavyofikili wewe, na
ndiyo maana nathubutu kusema kuwa kufungwa kwetu mabao 3-0 ni sawa na
kupata ushindi sisi, maana hata hivyo wametuleta kwenye Uwanja wao,
nadhani wakati wa mchezo wa Marudiano bila shaka itakuwa zamu yetu
kuibuka na ushindi maana leo wameshinda wao na mpira ni mchezo wa mmoja
kushinda, asiyekubali kushindwa siyo mshindani" alisema majuto
na
kuongeza kwamba mchezo huo kwa pande zote mbili umewapa changamoto ya
kuifanya sasa timu hiyo ya Kombaini ya Makipa kutambuliwa kote Nchini.
"mkakati
uliopo sasa ni kuhakikisha kwamba timu hii inazunguka kwenye Majiji
Makuu kwa ajili ya kufanya michezo yake ya kirafiki na timu za Mikoa,
lakini lengo kubwa ikiwa ni kuwapa Fursa wakazi wa Maeneo hayo
kuwatambua zaidi hawa Makipa wetu, lakini pia wakati wachezaji hawa
wakiwa kwenye hayo maeneo ya Majiji watakuwa na jukumu la kuwaandaa
wachezaji wengine zaidi vijana katika nafasi za kipa ili kuweza kuwa na
Makipa wengi zaidi kwa ajili ya Faida ya Taifa letu la Tanzania" alisema
Majuto
Naye
kocha wa Taswa FC Ally Mkongwe wakati akizungumza na wachezaji wa timu
zote alisema kuwa ni jambo la kufurahisha ambalo limeweza kufanikiwa kwa
asilimia 100 kwa kuwa lengo ilikuwa ni kufanya uzinduzi na timu zote
zimeweza kucheza kwa hali kubwa bila vurugu wala kuonyeshana mchezo
mbaya.
"tumefurahi
sana, niwapongeze wachezaji wote yaani Makipa na Taswa, jambo hili si
la mzaha kama tulivyofikili hapo mwanzo, lakini kumbe mwitikio wa
watazamaji ulikuwa ni mkubwa sana na wengi wamekuja kuwatazama wachezaji
na Waandishi wa habari, Watangazaji, na wakati umefika tukae tuangalie
namna ya kuboresha mahusiano haya yawe ya kudumu baina ya TASWA na timu
hii ya Kombaini ya Makipa wa Ligi kuu, isipokuwa tusameheane kwa yale
Mapungufu madogo yaliyotokea maana sisi ni binadamu lakini wakati
mwingine nadhani hayatatokea kwa pande zote mbili endapo yametokea kwa
mchezo wa leo" alisema Mkongwe.
Hata
hivyo wachezaji hao Makipa wametakiwa kufanya jitihada za kuhakikisha
wanakuwa chachu ya kuleta Makipa wengine nyuma yao kutokana na kwamba
nafasi ya Makipa kwa Tanzania inazidi kupungua kutokana na nafasi hiyo
kuwa ngumu ukilinganisha na nafasi za wachezaji wengine wa ndani ambao
wanakuwa ni wengi.
Naye
mmoja wa Makocha wasaidizi wa timu ya TASWA Ibrahim Masoud aliwaasa
wachezaji hao kuwa kioo kwa wenzao na kuwa kishawishi cha kuwapata
vijana wengine watakaokuwa makipa wa Tanzania miaka ijayo"Sina Mengi ya
Kusema kwa kuwa Kocha na Mwenyekiti wameeleza kwa kirefu lakini mimi
niko tofauti kidogo na wenzangu, kikubwa hapa mimi ni kuhusu nyie Makipa
wetu, kumbukeni kwamba nyinyi kina Kaseja, Ivo Mapunda, Shaaban Kado,
Dida, mstafa na nyinyi wote, nyie sasa mnaelekea Ukingoni, ni kama kina
Mwameja wakati wao, kina Manyika, Mfaume,nk, walikuwapo lakini
walipopotea hao makipa Tanzania iliyumba sana kuwapata nyinyi, na hiyo
inatokana na kwamba Wachezaji wengi Makipa hawapati Fursa ya kuandaliwa,
na niwatake sasa kutumia mwanya huu kwa kuwa tayari mmekuwa ni makipa
Hodari kuhakikisha kwamba wakati wa Mapumziko ya Ligi, muweze kuingia
Darasani kwa ajili ya kupata ujuzi wa kuwa Walimu wa Makipa, Kila mmoja
kwa wakati wake lengo mtakapomaliza muda wenu wa kuitumia Tanzania
katika Soka, muweze kuwa walimu wazuri na wazalishaji wazuri wa Makipa
wengine" alisema Ibrahim Masoud(Maestro)
Kwa
Upande wao Makipa hao wao hawakuwa na la kusema isipokuwa kwa niaba ya
wachezaji wote wa Makipa Ivo Mapunda alisema kuwa wanashukuru kwa Sapoti
kubwa kutoka Chama cha TASWA, ambao mara zote wamekuwa mstari wa mbele
kuwapa maelekezo, kitendo kilichowaweka karibu zaidi hata wakati wa
Uzinduzi wa Chama hicho cha Magolikipa," Sisi binafsi tumefurahi
kukutana na timu hii ya TASWA, maana kiujumla wachezaji wengi wa Taswa
wanafahamu mpira, ila tumewafunga kutokana na kukosa Pumzi tofauti na
sisi wengi tunafanya mazoezi kila siku na timu zetu tena timu kubwa za
ligi kuu, mimi Kesho( Leo) naelekea Zazibar Kambini, kujiunga na Timu
yangu, kwa hiyo unaona jinsi mchezo huu ulivyokuwa ni muhimu sana kwetu
hata nimeshindwa kuongozana na wachezaji wazangu pamoja na Mwalimu wangu
kutaka nisicheze hii leo lakini nimemkatalia kwamba ni lazima nijumuike
na Makipa wenzangu kwenye jambo hili la Umoja, maana sasa sisi Makipa
pia tumekuwa ndugu wa karibu na Marafiki wa Kweli, zama za kale kwamba
huyu na huyu aziivi eti kwa kuwa wote ni Makipa imepitwa na wakati,
utatukuta mimi, Kaseja, Kado, Dida, Mstafa, na wengine tukizungumza na
kufurahi pamoja, sisi siyo maaduni ni marafiki tena niwapongeze
Wadhamini wa Mpambano huu(Uzinduzi) Kampuni ya TWIGA CEMENT kwa kufanya
jambo hili, limezidi kutuweka karibu zaidi, na naamini kwamba watazidi
kutuunganisha na kuandaa michezo Mingi zaidi kwa ajili ya kuwapa Raha
wakazi na mashabiki wetu Mikoani" alisema Ivo Mapunda
Akizungumzia
mchezo huo Afisa Masoko wa TWIGA CEMENT,Alex Gideon,
alisema kuwa maandalizi yamekwenda kama walivyopanga isipokuwa
mkanganyiko umetokea kwenye eneo dogo la Uwanja, ambapo awali mchezo huo
ilikuwa ufanyike kwenye uwanja wa KARUME kwa mujibu wa Matangazo
yaliyofanywa na vyombo vya habari,
"
sitaki kulizungumzia sana suala la mkanganyiko wa Uwanja, lakini
nadhani TFF katika hatua za mwisho imeshindwa kuruhusu mchezo wetu
kufanyika kwenye viwanja vyao ambako vyombo mbali mbali vilitangaza,
hivyo mashabiki wengi walifika Karume, na nichukue fulsa hii kuwataka
radhi sana wote waliotufuata kwenye viwanja vya Karume, mchezo wetu
ulibadilishwa uwanja kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu na
kwa kuwa ni TFF wenyewe waliopanga hatua za Mwisho Mchezo wa Ligi daraja
la kwanza kufanyika humo hatukuwa na kipingamizi, ni jambo la kimchezo
na ukizingatia ni ligi yetu pia sisi watanzania hivyo hilo niombe radhi
kwa mashabiki wetu wote, lakini kuhusu wadhamini wetu kama ulivyoona
mwenyewe wamejitaidi na huu ni mwanzo na maandalizi yamefanyika kwa siku
chache zana, wakati ujao tutaboresha na kulifanya jambo hili kuwa la
kudumu na lenye kuleta tija ya Maendeleo kwa hawa Makipa wetu, kingine
niwapongeze TASWA kwa ushirikiano wao maana wametufariji na kutupa
sapoti kubwa"
alisema Alex Gideon
aidha
mchezo huo ulikuwa kwa ajili ya kujenga mahusiano mema baina ya timu
zote, wachezaji pamoja na kufanya Uzinduzi wa Chama cha Makipa Tanzania,
waandishi
na Makipa wanaocheza ligi kuu Ya Vodacom Tanzania.