N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Monday, December 15, 2014

FAINALI YA Airtel UNI255 UDSM INTER-COLLEGE CHAMPIONS LEAGUE YAHIMITISHWA

SONY DSCWachezaji wa timu ya Chuo cha Sayansi za Jamii, wakijifua kwa mazoezi kabla ya mchezo wao dhidi ya timu ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia katika fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosaa taa. unnamed1  SONY DSCWachezaji wa timu za Chuo cha Sayansi za Jamii (jezi nyeusi) na Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, wakigombea mpira wakati wa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa. unnamed4Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram Mapunda akikagua wachezaji wa Chuo cha Sayansi za Jamii, kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa. unnamed6Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram Mapunda akikagua wachezaji wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa.Kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga.
…………………………………………………………………………………………
Na: Mwandishi Wetu.
Fainali ya Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yanayojulikana kama Airtel UNI255 yaliyoshirikisha wanafunzi wote wa schools na Colleges zilizopo chuoni hapo yamemalizika siku ya jumamosi ya tarehe 13/12/2014 Katika Fainali iliyovikutanisha vyuo vya Sayansi ya Jamii(College of Social Science)na Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (College of Engineering and Technology) ambapo hadi dakika tisini(90) zinamalizika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Timu ya kitivo cha CoET iliyokua na upinzani mkali kwa jumla ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Justin Rupia kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa CoSS Chawaka Francis na kumfanya mwamuzi wa mpambano huo Wema Ngota pamoja na wasaidizi wake Benjamini Mbughi, Hellen Mduma, Iddi Mfaume, Ramadhan Pondamali,Jackison Msilombo, Ally Sarehe na Faraji Gaibu,walioichezesha michezo hiyo tangu tarehe 8 mwezi huu kuwa katika hali tete kutokana na shangwe, nderemo na vifijo kutoka kwa Mashabiki wa CoET kucharuka uwanja mzima.
Kipindi cha Pili kila timu ilifanya mabadiliko ambapo CoSS iliwatoa Emmanuel George na Morrison Ng’owo na nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji Rashidi Hussen na Ramadhan Hussen dakika ya 67 na 75 huku wenzao wa kitivo cha CoET aliingia mchezajji Tibe Mario kuchukua nafasi ya mchezaji George Michael katika dakika ya 62 mabadiliko yaliyowanufaisha zaidi CoSS waliposawazisha bao dakika za Majeruhi baada ya kutokea piga nikupige na hivyo kuleta mtafaruku kutokana na Muda(Kiza) kuingia ambapo timu hizo zilishindwa kupigiana Penalti ili kupata mshindi wa kwanza na mshindi wa pili.
Katika michezo ya awali timu hizo za College of Social Science waliokuwa kundi B lililokuwa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo Hostel ilifanikiwa kuongoza vizuri ambapo ilicheza mechi 3 ikashinda moja na kutoa sare ya bila kufungana mechi 2. matokeo yalioyowapa pointi 5 na goli 2 na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali.
Katika michezo ya awali timu ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia-College of Engineering and Technology(CoET) iliyokuwa kundi A lililokuwa katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) ilifanikiwa kuongoza pia vizuri na kupata pointi zilizoiweka kwenye nafasi ya kucheza Fainali baada ya kushinda hatua ya nusu fainali dhi ya timu ya UDBS.
Timu iliyochukua nafasi ya tatu ni kitivo cha UDBS waliofanikiwa kuwafunga Kitivo cha SoED kwa njia ya penalty baada ya kumaliza dakika 90 kwa kufungana 2-2 katika mchezo uliokuwa wa upinzani mkubwa kutokana na timu ya SoED kuwa na wachezaji wengi wakongwe waliokaa muda mrefu hapo chuoni na wameshiriki michuano mingi na wamefanya vizuri na ndiyo timu pekee iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kunyakua Uchampioni huo wa Chuo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti timu Capateni wa Timu zilizoshiriki hatua ya nusu fainali, Bodoo Oduon wa Timu ya CoET, Michezo hiyo imeleta changamoto kubwa kwa wanafunzi na kuwataka wadhamini kujitokeza kudhamini michezo ya vyuo vya mkoa wa Dar es Salaam.
“Tumefurahi pamoja, tumecheza na kuruka ruka hii ni shangwe, tena mimi nasema hawa Airtel hakika wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa, ni pesa ngapi wamewekeza hapa, na hii ni kwa Chuo Kimoja tu ch UDSM na bado kuna hiyo michuano ya vyuo vya Dar es Salaam, ni muunganiko mzuri unaoletwa na hawa Airtel kwa kutuunganisha kati ya vyuo na vyuo”alisema Bodoo Oduon
Kuhusu kutopata matokeo ya Mshindi wa kwanza timu kampteni wa CoSS  Elias Mshomba alisema kuwa ni kawaida kutokea jambo hilo, maana Fainali ilihusisha watoto wa baba mmoja, kwamba jambo kubwa ni juu ya hizo College zilizoingia fainali kuwa wawakilishi wa College Championship Dar es Salaam inayotazamiwa kuunguruma mapema kuanzia mwezi wa tatu mwakani.
“Wewe unadhani kuna jambo limeharibika hapa kwa kutopata mshindi wa kwanza ama wa pili, sisi tulikuwa katika mchujo wa kupata wawakilishi wa chuo, kama ni zawadi zote ni za UDSM, hivyo nawaomba wachezaji wote waliofanikiwa kuzifikisha timu zao hatua ya nusu fainali, kuendelea na maandalizi makali ya kuhakikisha tunatwaa hizo zawadi zinazokuja za ushindani wa vyuo vya Dar es Salaam, mwenyewe umeona kiza kimeingia hivyo wachezaji wasingekuwa na uwezo wa kumaliza penalty tano kabla ya usiku na hapa hakuna taa, tusubiri hiyo michuano ambayo sijui wadhamini ni nani kama watakuwa ni Airtel basi itakuwa Raha sana maana tumefurahishwa na Airtel” alisema Elias Mshomba.
Akiongea kuhusiana na mwenendo wa mashindano hayo kwa Waziri wa michezo wa jumuiya ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam STANLRY JULIUS alisema “Mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto wa kipekee hasa kutokana na wadhamini wetu Airtel kutupatia vifaa vya kutosha na kwa namna moja yameongeza hari sana kwa washiriki wote, na Pengine hii imekuwa ni changamoto kwetu kutokana na Uwepo wa Michuano ya Wanavyuo, College Championship Tanzania” alisema
 Na kuongeza kuwa “sisi kama UDSM tumepewa heshima kubwa ya kutoa wawakilishi wane watakaoungana na College zingine Kuunda jumla ya Timu 32 za College Kanda ya Mashariki,hivyo tumefaidika sana sisi kama chuo, kwa kuwa jambo lingine tumeweza kufanya Selection (Usahili) wa kupata timu ya chuo (UDSM ALLY STARS)ambayo inaweza kuwakilisha chuo kwenye michezo ya EAST AFRICAN UNIVERSITIES COMPETITION, inayoshirikisha nchi za Afrika mashariki kwa michezo ya Vyuo Vikuu,lakini pia nichukue Fulsa hii kuwaomba tena Airtel, kupitia hii hii Airtel UNI255 kuweza kudhamini hatua inayofuata ya Michezo ya Vyuo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, NACTE & Inter College Championship-Dar es Salaam,itakayoshirikisha jumla ya vyuo 32, Kama ulivyoona mwenyewe jinsi ushindani ulivyomkubwa na hata soka lenyewe lipo vyuoni,shamra shamra zote hizi hapa ni chuo kimoja je itakapokuwa imekutanisha vyuo vingine kama vile IFM,DIT,NIT,TRA,ISW,IAE,BANDARI COLLEGE,CBE, DACICO, HEDEN HILL, NJUWENI, MUHIMBILI MEDICAL SCHOOLS, KIBAHA COTC na St. JOSEPH UNIVERSITY ambazo tayari zimefuzu hatua ya Makundi yake ya Michuano ya Bonanza la NACTE INTER COLLEGE DAR ES SALAAM BONANZA unadhani shamra shamra zitakuwaje, na tunaomba hiyo Fainali ya College za Dar es Salaam ifanyike Uwanja wa Taifa ili TFF na Makocha wa Timu ya Taifa waje wachague wachezaji watakaoisaidia Tanzania katika michuano ya Taifa na kimataifa”alisema STANLRY    
Timu iliyoonyesha nidhamu  na Ushindani mkubwa wa kuwania hizo nafasi wakati wa mchujo huo wa College ya UDSM ili kuingia kwenye ushiriki wa michuano ya Vyuo vya Dar es Salaam ni SJMC iliyokuwa kinara wa kundi A katika viwanja vya ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaa ni (School of Journalism and Mass Communication) ilicheza mechi mbili na kushinda zote na kujitengenezea pointi 6 na huku akiongoza kwa kuwa na bao 5 za kufunga.
Akizungumzia michezo hiyo kwa upande wa College za UDSM mratibu  wa College za chuo hicho bwana. Albert Kimaro alisema kuwa “ Kundi B ambalo mechi zake zilichezewa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo Hostel, ndilo lililokuwa na timu zenye wachezaji wakongwe na liliongozwa na COSS (College of Social Science) timu iliyokuwa na mashabiki wengi na ambayo imeweza kucheza Fainali, lakini pia ndani ya UDSM zimeshiriki College kama CONAS, ambayo pia ilikuwa na wachezaji wazuri, UDSL,  COET, COICT,ISK,na COHU” alisema Albert.
Mgeni Rasmi katika Fainali hiyo (Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram Mapunda ) baada ya ukaguzi wa wachezaji aliwaasa kuwa na utulivu, Upendo, mshikamano,  wakati wote wa michezo na waepuke ugomvi wakati wote kwani michezo ujenga na kuimarisha mahusiano mwao.
“kikubwa hapa ni jinsi ya kujenga misingi imara ya michezo ndani ya vyuo vyetu, sina maana katika chuo hiki pekee, bali vyuo vyetu vyote, lakini pia niseme kwamba miaka ya nyumba hatukuwa na hamasa ya michezo vyuoni kutokana na miundo mbinu, lakini wakati huu nadhani kwamba michezo ama vipaji vipo vingi vyuoni, nimesikia kuna kampuni ya MIDETA entertainment imeanza harakati za kuanzisha hii michezo ya vyuo vyote vya Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla,inayojulikana kama College Championship Dar es Salaam, ambapo kwa sasa kuna mtowano mwingine unaendelea wa vyuo vingine kupitia mfumo uliowekwa wa Bonanza la Nacte inter College Dar Es Salaam ili kupata timu zitakazoshiriki ligi hiyo itakayokuwa na timu 32, nina hakika kwamba michuano itakuwa mizuri na itapendwa sana na pia itazalisha vijana wengi watakaokuwa wasomi kasha wawakilishi wetu kimichezo” alisema Profesa Mapunda.
 Naye Meneja Uhusiano wa Airtel Jackison Mbando alisema kuwa kuwa Mashindano yalikuwa mazuri na timu na kwamba imewapa changamoto ya kuongeza udhamini kwenye michezo ya vyuo, “ kama unavyoona mwenye jinsi Fainali ilivyosheheni watu utadhani mechi yay a Mtani Jembe, upinzani ni mkubwa sana na imeleta changamoto sana, lakini kubwa ni kuhakikisha kwamba Airtel inawafikia Watu wote kwa namna ya pekee,
Tupo katika harakati za kuboresha maisha ya wanavyuo kwani tunatambua kwamba wanahitaji kusoma kwa kutumia Mitandao katika ulimwengu huu wa sasa ambao Airtel kama unavyoona ni zaidi ya mitandao mingine, tunaanza sisi kisha wanafuata wengine nah ii tumeanza kwa kuwa karibu na wanavyuo ili tuwape nafuu katika usomaji na upataji wa mawasiliano, lakini si hivyo tu kama unavyoona hapa leo mambo yamenoga katika kuwapa pia afya wanafunzi wa vyuo kwani Michezo inaleta afya ndiyo maana tumeamua kuingia sasa kusaidia na kudhamini hii michezo ya Vyuo, na sasa tumeanza na College za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tunatarajia kufanya mazungumzo na waandaaji wa Michezo ya vyuo kwa Mkoa wa Dar es Salaam (MIDETA entertainment) tupate mahitaji yao tuangalie, uwezekano upo wao waje tuzungumze na ikibidi hata kupata timu bora ya College za Tanzania,(College Championship Tanzania”alisema Jackison Mbando.
Aidha katika kilele cha tamasha hilo Airtel ilizindua kwa wanafunzi wa chuo kikuu huduma ya UNI255 itakayowawezesha kuwasiliana , kuperuzi internet kwa gharama nafuu.

No comments:

Post a Comment