N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Friday, July 29, 2011

REDDS MISS ILALA 2011- HATUA YA PILI KABLA YA WASHINDI- KUELEKEA TANO BORA









 Picha Zote za juu ni Washiriki Miss Ilala 2011, katika kuwania kuingia hatua ya tano bora, chini ya Udhamini wa PARADISE CITY HOTEL -iliyopo jengo la Benjamini Mkapa Posta,
Kamati ya Miss Tanzania, ikiongozwa na Hashimu Lundenga wakifuatilia kwa Makini Mashindano hayo(hatua inayofuata utaona washindi na majina yao usikose muda mfupi ujao)(Picha Zote na Shaaban Mpalule).

MISS ILALA 2011- MATUKIO KATIKA PICHA-MNAZI MMOJA USIKU WA JANA












 Picha za juu zote ni Washiriki wakiwa katika Mapozi kutafuta njia ya kuingia hatua ya Tano bora
 Mkurugenzi wa Lino Agency-Hashimu Lundenga akiwa na JAJI Mkuu wa Miss Ilala wakiteta jambo
Baadhi ya Wageni Waalikwa wakifuatilia kwa makini Onyesho la Miss Ilala 2011, katika viwanja vya Mnazi mmoja usiku wa kuamkia leo, Mashindano hayo yalidhamini wa PARADISE CITY HOTEL-Jengo la Benjamini Mkapa Posta, inayomiliki pia Ukumbi wa Burudani wa SAVANNAH.(Picha zote na Shaaban Mpalule).

UHURU WA KUABUDU NA WAJIBU WA VIONGOZI WA DINI

Katika nchi yetu yapo madhehebu mbalimbali ya dini, lakiniu yote yanatawaliwa na kusimamiwa na maelekezo yaliyoainishwa katyika katiba ya nchi yetu
Mbele ya sharia za nchi yetu, hakuna dini iliyo bora kuliko nyingine, imani na uhuru wa kuabudu unaolindwa na kuhifadhiwa katika katiba na sharia za nchi yetu, unatoa wajhibu kwa kila dini na waumini wake kutambua , kulinda , kuhifadhi na kuheshimu utu, heshima na maslai yaw engine.
Kwa mujibu wa sharia , madhehebu yote yana wajibu ufuatao kwa maslai ya jamii:-
-Dini zipo kwa ajili ya usalama wa jamii
-Dini zipo kwa ajoli ya amani katika jamii
-Dini zipo kwa ajili ya kulinda maadili ya jamii na
-Dinbi zipo kwa ajioli ya kujenga umoja na ustawi wa taifa
Aidha dini ni sehemu ya utamaduni wa jamii na kwa tafsiri hiyo pana dini zinapaswa kuwa ni gundi au sementi inayoshikamanisha jamii na kuipa ufahamu wa kutambua na kuthamini maadili ya jamii, umoja na mshikamano wa taifa.

Miongozo ya dini utawala na kudhibiti dhamira za wafuasi, ambamo ndimo liliko chimbiko la mema au matendo ya kiharifu ,ndiyo sababu inayofanya madhehebu ya dini kuwa na dhamana kubwa ya kusimamia dhamira za watu,katika ujenzi wa jamii adilifu na kuepusha vurugu au matendo mengine yanayoweza kuathiri maendeleo ya ustawi wa taifa letu.
Kwa lugha nyingine, viongozi wa dini ni askari wanaofanya doria za roho ,ili kupima kufanikiwa au kushindwa kwa askari wa doria ya roho, ni kuongezeka au kupungua kwa waumini wanaotenda uhalifu.

Thursday, July 28, 2011

FAINAL MISS ILALA 2011 NI KESHO MNAZI MMOJA- kila mrembo amejigamba kushinda taji hilo

 Washiriki wa Miss Ilala 2011 wakiwa katika picha ya pozi
 Mratibu wa Miss Ilala Jackison Kalikumtima akitoa ufafanuzi kuhusu zawadi za Miss Ilala wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, hafla hiyo imefanyika katika jengo la Benjamin Mkapa, PARADISE CITY HOTEL- SAVANNAH.





 Katika picha juu ni Miongoni mwa washiriki watakaochuana kesho kuwania Taji hilo
 Jackison akisisitiza jambo
Baadhi ya washiriki wa Miss Ilala 2011, wakisikiliza jambo kutoka kwa Mwandishi wa habari wakati wa hafla iliyofanyika leo kwenye Hotel ya Paradise City, ikiwa ni hatua za mwisho za maandalizi ya shindano hilo

TIGO YAKABIDHI VIBAO SHULE DAR ES SALAAM LEO.

Msimamizi wa biashara na masoko wa kampuni ya Tigo Bw.Gaudens Mushi (kushoto) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Msisiri A, Bi.Prisca Myalla. Kibao cha kuandikia, Kulia ni makamu mwenyekiti wa shule hiyo Bw. Joseph Shango.  
 Msimamizi wa biashara na masoko toka kampuni ya Tigo Bw.Gaudens Mushi akimwelekeza mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi ya Msisiri A ya jijini Dar es Salaam, Hifta Jafari jinsi ya kutumia vibao maalum vya kujifunzia vilivyotolewa na Tigo shuleni hapo jana.
Msimamizi wa biashara na masoko toka kampuni ya Tigo Bw.Gaudens Mushi akimwelekeza mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi ya Msisiri A ya jijini Dar es Salaam, Hifta Jafari jinsi ya kutumia vibao maalum vya kujifunzia vilivyotolewa na Tigo shuleni hapo jana.

WIZARA YA AFYA YATILIANA MAKUBALIANO NA SERIKALI YA JAPANI KUHUSU MABORESHO KATIKA HUDUMA ZA AFYA NCHINI.

  Mwakilishi Mkuu wa JICA kutoka Serikali ya Japani, Yukihide Katsuta(kulia) akimkabidhi nyaraka  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Bi, Blandina Nyoni, katika iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Afya, Dar es Salaam leo, Nyaraka hizo ni za Makubaliano ya kuboresha huduma za Afya katika Hospitali za Mikoa yote ya Tanzania Bara, ambapo Japani italeta wataalamu wao nchini na Mradi huo utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia mwaka huu,
 Mwakilishi Mkuu wa JICA kutoka Serikali ya Japani, Yukihide Katsuta(kulia) akisaini nyaraka   na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Bi, Blandina Nyoni, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Afya, Dar es Salaam leo,

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Bi, Blandina Nyoni(wa pili mbele kulia) na Mwakilishi Mkuu wa JICA kutoka Serikali ya Japani, Yukihide Katsuta(wa pili kushoto mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliohudhulia katika hafla hiyo.