N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Friday, July 29, 2011

UHURU WA KUABUDU NA WAJIBU WA VIONGOZI WA DINI

Katika nchi yetu yapo madhehebu mbalimbali ya dini, lakiniu yote yanatawaliwa na kusimamiwa na maelekezo yaliyoainishwa katyika katiba ya nchi yetu
Mbele ya sharia za nchi yetu, hakuna dini iliyo bora kuliko nyingine, imani na uhuru wa kuabudu unaolindwa na kuhifadhiwa katika katiba na sharia za nchi yetu, unatoa wajhibu kwa kila dini na waumini wake kutambua , kulinda , kuhifadhi na kuheshimu utu, heshima na maslai yaw engine.
Kwa mujibu wa sharia , madhehebu yote yana wajibu ufuatao kwa maslai ya jamii:-
-Dini zipo kwa ajili ya usalama wa jamii
-Dini zipo kwa ajoli ya amani katika jamii
-Dini zipo kwa ajili ya kulinda maadili ya jamii na
-Dinbi zipo kwa ajioli ya kujenga umoja na ustawi wa taifa
Aidha dini ni sehemu ya utamaduni wa jamii na kwa tafsiri hiyo pana dini zinapaswa kuwa ni gundi au sementi inayoshikamanisha jamii na kuipa ufahamu wa kutambua na kuthamini maadili ya jamii, umoja na mshikamano wa taifa.

Miongozo ya dini utawala na kudhibiti dhamira za wafuasi, ambamo ndimo liliko chimbiko la mema au matendo ya kiharifu ,ndiyo sababu inayofanya madhehebu ya dini kuwa na dhamana kubwa ya kusimamia dhamira za watu,katika ujenzi wa jamii adilifu na kuepusha vurugu au matendo mengine yanayoweza kuathiri maendeleo ya ustawi wa taifa letu.
Kwa lugha nyingine, viongozi wa dini ni askari wanaofanya doria za roho ,ili kupima kufanikiwa au kushindwa kwa askari wa doria ya roho, ni kuongezeka au kupungua kwa waumini wanaotenda uhalifu.

No comments:

Post a Comment