Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika Hospitali ya rufaa ya Amana iliyopo Ilala, Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza baada ya sherehe za kuapishwa.
Na : Shaaban Mpalule
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala ikiwa ni masaa machache tangu kutoka kuapishwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Wizara hiyo.
Mhe. Ummy aliwasili katika hospitali ya Mwananyamala, majira ya saa 8 mchana na kuanza kuzungumza na wananchi mbalimbali waliokuwa wamekaa eneo la hospitali hiyo kuhusu matatizo yanayowakabili pindi wanapofika hospitali hapo kupatiwa huduma ambao wengi wao walionekana kutoridhishwa na huduma wanazopatiwa wanazozihitaji.
Mmoja wa wananchi ambao alielezea kwa masikitiko yaliyomkuta pindi alipofika hospitalini hapo ni, Bi. Khadija Meso ambaye alisema kuwa walikuwa na siku tatu tangu wamefika hospitalini hapo ambapo walikuwa wamempeleka mtoto wao ambae alikuwa anaumwa lakini alikuwa hapatiwi huduma hali imeyopelekea kupoteza maisha kwa mtoto huyo.
Mwingine aliyezungumza aliyejitambulisha kwa jina la Mama Madohoro alisema kuwa anashangazwa na hospitali ya rufaa kuwatoza wazee pesa licha ya sera ya afya kusema wazee na watoto chini ya miaka 5 kupatiwa bure huduma za kiafya.
Alisema kuwa alimpeleka hospitalini hapo ndugu yake mwenye umri wa miaka 90 ambae alikuwa akihitajika kulipia vipimo vilivyo na gharama kubwa huku vya gharama ndogo akipatiwa bure na kutokana na uwezo mdogo wa kifedha alionao ukapelekea kupoteza maisha yake kwa mgonjwa huyo.
Nae Othaman Rwambo alimuomba Mhe. Waziri kuwa ajaribu kuzungumza na wauguzi wa hospitali hiyo kutokana na kutoa majibu machafu kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikagua vyumba vya madaktari baada ya kuona mlundikano wa wagonjwa wakisubiri huduma.
Alisema kuwa kasi ya rais wa awamu ya tano ni kufanya kazi na wao kama watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuwahudumia watanzania na kuwataka watumishi hao kuweka uzalendo mbele kuliko maslahi binafsi.
Akiwajibu wananchi hao pamoja na kuelezea sababu ya ziara yake, Mhe. Ummy Mwalimu alisema kuwa amefika hospitalini hapo ili kujua changamoto zinazowakabili wananchi lakini pia kujifunza ni kitu gani ambacho wananchi wanahitaji kuboreshewa katika sekta ya afya.
Alisema kuwa matatizo aliyoyakuta ni changamoto kwake na wizara yake na watakaa kama wizara kuona ni jinsi gani wanaweza kutatua matatizo yanayojitokeza katika hospitali hiyo na kuutaka uongozi wa hospitali hiyo kumaliza matatizo yaliyo ndani ya uwezo wao ndani ya siku 3.
“Mambo ambayo nimeyakuta hapa ni kujifunza na kuona ni hali gani wanakumbana nayo wananchi wanapokuja kupata huduma za kiafya lakini pia kwangu ni changamoto lakini kwa kasi aliyonayo rais wetu wa awamu ya tano hatuna budi na sisi kuwa na kasi hiyo na mimi napenda kuwaambia wananchi wanaopata huduma katika hospitali hii tutatatua matatizo yanayowakabili,
“Nimeupa uongozi wa hospitali kazi ya kumaliza matatizo yaliyopo wanayoweza kuyamaliza kama neti kwenye wodi kama ile ya wajawazito, na hata mambo ya feni kwenye wodi za wanaume na mengine tutakaa kama wizara kuyajadili tuone jinsi gani tutayamaliza,” alisema Mhe. Ummy.
Mh. Naibu Waziri, Dkt. Hamis Kigwangala akiingia katika chumba cha X-Ray kuangalia utendaji wa kazi unavyoendelea.
Aidha Mhe. Waziri alisema siku ya Jumatano wanatarajia kutambulisha namba ambayo wananchi watakuwa wanaitumia kutoa taarifa wizarani kuhusu kero wanazokutana nazo hospitalini wanapokwenda kupata huduma za matibabu.
Nae Naibu Waziri wa Wizara hiyo ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya Amana na kukuta baadhi ya huduma za afya katika hospitali hiyo zikiwa zimesimama kwa sababu mbalimbali.
Baadhi ya matatizo ambayo amekutana nayo hospitalini hapo ni pamoja na kutokuwepo kwa mtoa huduma katika chumba cha Utra Sound, Ubovu wa mashine ya kuchunguza matatizo yaliyopo mwilini (MS4S) na kubakia moja ikifanya kazi ambayo inachukua muda mrefu kutoa majibu.
Matatizo mengine ambayo amekutana nayo ni uchache wa vitanda, kutokupatikana kwa dawa katika duka la hospitali huku maduka ya nje ya hospitali zikipatikana na kutokuwepo kwa baadhi ya watumishi ofisini kukiwa ni muda wa kazi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na mtoa huduma katika chumba cha X-Ray ambapo aliridhishwa na utoaji huduma wa mtumishi huyo.
Akizungumzia matatizo hayo alisema kuwa kuna uzembe umekuwa ukifanyika kwa baadhi ya watumishi hali inayofanya hospitali hiyo kuwa na wagonjwa wengi bila kupatiwa huduma na badala yake wanawapa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Tunachotaka ni kuona wananchi wanapata huduma, nimefika hapa nakuta hata chumba cha Utra Sound anaehusika hayupo na hata wagonjwa wakija hawatapata huduma na kinachofata hapo wanampeleka Muhimbili ndiyo maana Muhimbili imejaa wagonjwa kumbe sababu ni uzembe uliopo huku kwenye hospitali za rufaa,” alisema Dkt. Kingwangala.
Aidha Mhe. Naibu Waziri ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kufika wizarani siku ya jumatatu saa 10 jioni ili kupewa maelekezo jinsi ya kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi na kwenda sawa na kasi ya rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye anahitaji kuona serikali yake ikifanya kazi kwa kuhudumia wananchi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na baadhi ya wananchi kuhusu upatikanaji wa huduma wanazopata hospitalini hapo ambao wengi wao hawajaridhishwa na utendaji wa wahudumu wa zamu wa siku hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na mmoja wa Daktari (ambaye hakutaka sura yake iyonekane) kuhusu utaratibu wa utoaji huduma kwa wagonjwa wanaosubiri huduma hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akimuulizia Kiongozi wa zamu katika ofisi za mapokezi ya hospitali hiyo.
Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya rufaa ya Amana, Bupe Mwakalenge akijibu maswali ya Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusu kutokuwepo kwa baadhi ya Madaktari katika baadhi ya vitengo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akitazama moja ya cheti cha mgonjwa aliyekuwa akilalamika kusubiri kwa muda mrefu bila kupatiwa huduma.
Mwanasayansi wa Maabara ya Hospitali ya rufaa ya Amana, Jabir Mukhsin (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu ubovu wa mashine inayotumika kufanya vipimo mbalimbali (MS4S) ikiwemo mzunguko wa damu mwilini ambayo kwa sasa imeharibika na kubakiwa na mashine moja ambayo ufanyaji wake wa kazi unachukua muda mrefu kutoa majibu sahihi.
MS4S Mashine ambayo imeharibika.
Mmoja wa wagonjwa waliokuwepo wakisubiri huduma ya kipimo cha MS4S akimwelezea Mh. Naibu Waziri kuhusu kutokufanyika kwa kipimo hicho licha ya kuwa hospitali wamepokea malipo yake ya kufanyiwa kipimo hicho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akionekana kushangwazwa na jambo fulani wakati akiendelea na ziara yake hospitalini hapo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Gideon Malabeja.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwa nje ya chumba cha Ultra-sound ambacho kimefungwa kufuli licha ya maelezo ya Muuguzi Kiongozi wa Hospitali hiyo Bi. Mwakalenge kuwa mashine hiyo ni nzima na haina tatizo lolote.
Muuguzi Kiongozi wa wagonjwa wa nje, Francis Itima akimwelezea Mheshimiwa kuhusu changamoto ya upungufu wa vitanda katika wodi ya wakina mama waliojifungua.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikagua wodi ya watoto ambayo aliridhishwa na hali iliyopo katika wodi hiyo.
Mfamasia wa zamu katika hospitali ya Amana, Anna Kajiru akimpa maelezo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu upungufu wa dawa uliopo katika duka hilo la dawa hospitalini hapo.
Baadhi ya wananchi wakipatiwa huduma ya dawa katika duka la dawa lililopo hospitalini hapo.
Pichani juu na chini ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu ziara yake ya kushtukiza, matatizo yanayoikabili hospitali hiyo na hatua ambayo wizara itachukua.
|
Monday, December 14, 2015
WAZIRI WA AFYA NA NAIBU WAKE WAFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA NA AMANA
Tuesday, November 10, 2015
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATANGAZA MFUMUKO WA BEI WA MWEZI OKTOBA, 2015
Na Veronica Kazimoto
09/11/2015
Dar es Salaam.
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 mwezi Septemba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo amesema kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei kumesababishwa na kupanda kwa bei za bidhaa na huduma zingine za kijamii ikiwemo chakula na nishati.
“Kupanda kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2015 kumechangiwa na ongezeko la bei za vyakula kama vile Mchele ambao umeongezeka bei kwa asilimia 0.8, unga wa muhogo umeongezeka hadi asilimia 0.7, nyama kwa asilimia 0.8, samaki kwa asilimia 5.5, ndizi za kupika asilimia 0.7 na choroko kwa asilimia 0.9”, amesema Kwesigabo.
Bidhaa zisizokuwa za vyakula kama vile vitambaa kwa ajili ya nguo za kike zimepanda kwa asilimia 1.6, viatu vya kiume asilimia 1.1, mkaa asilimia 1.4 na gharama za kupata ushauri kwa daktari pia zimepanda hadi kufikia asilimia 1.4.
Kwa upande Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.1 ambao ni ongezeko sawa na mwezi Septemba, 2015. Fahirisi za bei pia zimeongezeka kutoka 159.04 hadi kufikia 159.17 kwa mwezi Oktoba, 2015.
“Fahirisi za bei za vyakula vya nyumbani na migahawani iliongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 10.0 kutoka asilimia 9.4 kwa mwezi Septemba, 2015 ambapo bidhaa zisizokuwa za vyakula zimepungua kidogo kutoka asilimia 1.9 hadi asilimia 1.7 kwa mwezi Oktoba, 2015,” amefafanua Kwesigabo.
Kwesigabo amesema kuwa Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa mwezi Oktoba, 2015 umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 2.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwezi Septemba, 2015.
Mwisho.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 ambao umepanda hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwezi Septemba, 2015.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 ambao umepanda hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwezi Septemba, 2015. Kulia kwake ni Mtakwimu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Muhdin Mtindo. (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO)
Tuesday, May 19, 2015
Monday, May 11, 2015
RAIS KIKWETE AWEKA SHADA LA MAUA KABURI LA MASHUJAA, ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA ALGERIA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au Whatsapp namba +255767869133.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka
shada la maua kwenye kaburi la Mashujaa wa Algeria, leo Jumapili, Mei
10, 2015. Rais Kikwete yupo nchini Algeria kwa ziara ya siku tatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo wakati alipotembelea Makumbusho ya Taifa la Algeria, Mjini Algiers, leo Jumapili, Mei 10, 2015. Rais Kikwete yupo nchini Algeria kwa ziara ya siku tatu.
PICHA NA IKULU.
Monday, April 13, 2015
Thursday, March 19, 2015
ZINDUKA Vocational Training Center Students:
Also the program established the tree planting in Nyamuswa area.
|
Wednesday, March 18, 2015
Serikali yajidhatiti Kudhibiti Makosa ya Utakatishaji fedha haramu Nchini- AG Masaju
Ndugu Masaju pia ameeleza kuwa
wahalifu wanatumia fursa iliyoletwa na maendeleo ya mifumo ya
Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA) katika biashara mbalimbali
kutakatisha fedha zinazopatikana kwa njia ya uhalifu na kuzisafirisha
haraka katika nchi nyingine ili kuficha uhalisia wa mali hizo kwa
dhamira ya kuepuka kukamatwa na vyombo vya uchunguzi hapa nchini ambapo
ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo kutumia vizuri fursa waliyoipata
kujifunza na kupata majibu ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo
katika utendaji kazi ili kuongeza kuongeza ufanisi na kuhakikisha
wahalifu hawafaidiki na uhalifu wanaoufanya.
Awali, akimkaribisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw.Ayub Mwenda ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshugulikia Usimamizi na uratibu wa uendeshaji wa Mashtaka ya Jinai kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali alieleza kuwa Serikali inatoa uzito mkubwa katika suala la kukabiliana na uhalifu na mashauri yanayohusu masuala ya utakatishaji fedha hivyo nguvu na uelewa wa pamoja vinahitajika kutoka kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na kuendelea kushirikiana ili kujiimarisha zaidi katika eneo hilo.
Wednesday, March 11, 2015
Serikali kuendelea kuandaa mazingira bora ya wavuvi Zanzibar
bdilah
Jihad Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea kuandaa mazingira bora ya
wavuvi ikiwa ni pamoja na kujenga masoko ya kisasa ili kuimarisha
sekta ya uvuvi na kuzalisha ajira kwa wananchi .
Amesema kuwa wananchi wengi wa Visiwa vya Zanzibar
wanategemea sekta ya Uvuvi kuendesha shughuli zao za uchumi na kueleza
kwamba jumla ya watu 34,000 wamejiajiri kupitia sekta ya uvuvi ambapo
kupatikana kwa masoko ya kisasa kutaongeza ajira kwa wananchi .
Kauli hiyo ameitoa wakati akikabadhi soko la Tumbe Wilaya ya Micheweni kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazni Pemba , ambalo limejengwa na kampuni ya Ngogo ya Iringa na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 712.
Aidha waziri jihad amewataka wananchi wa Wilaya ya Micheweni kulitumia soko hilo kwa kufuata mila , silka na tamaduni wa watu wa Tumbe .
Kauli hiyo ameitoa wakati akikabadhi soko la Tumbe Wilaya ya Micheweni kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazni Pemba , ambalo limejengwa na kampuni ya Ngogo ya Iringa na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 712.
Aidha waziri jihad amewataka wananchi wa Wilaya ya Micheweni kulitumia soko hilo kwa kufuata mila , silka na tamaduni wa watu wa Tumbe .
“Tunatambua kwamba soko hili
liko sehemu za mkusanyika wa watu wengi kutoka sehemu tofauti za Pemba ,
hivyo basi mnatakiwa kusimamia na kufuata mila , silka na tamaduni za
wenyeji wa hapa ili kusiwepo na mporomoko wa maadili ya jamii ”
alisisitiza Jihad .
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman
amewashauri wavuvi wa Wilaya ya Micheweni kuhamasishana kulitumia soko
hilo ili liweze kutumika na kukuza uchumi wao na Taifa kwa Ujumla .
Mkutano wa 19 baraza la wawakilishi kuanza jumatano
Katibu
Mkuu Baraza la Wawakilishi Zanzibar Nd. Yahya Khamis Hamad akizungumza
na waandishi wa habari kwa kutoa ufafanuzi kuhusu kikao cha Mkutano wa
Kumi na Tisa (19) wa Baraza la Nane (8) la Wawakilishi unaotarajiwa
kuanza siku ya Jumatano ya Tarehe 11 March, 2015. (Picha na Rahma Khamis
Maelezo-Zanzibar). Baadhi
ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano huo wakimsikiliza
kwa makini Katibu Mkuu Baraza la Wawakilishi Zanzibar. (Picha na Rahma
Khamis Maelezo-Zanzibar).
Katibu
Mkuu Baraza la Wawakilishi Zanzibar Nd. Yahya Khamis Hamad akijibu
maswali yaliyoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari wakati wa mkutano
huo. (Picha na Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar).
Na Rahma Khamis na Mwanaisha Moh’d Maelezo-Zanzibar.
Mkutano wa Kumi na Tisa (19) wa
Baraza la Nane (8) la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya
Jumatano Tarehe 11 March, 2015 saa 3:00 kamili za asubuhi ambapo miswada
minne ya sheria itawasilishwa na kujadiliwa barazani hapo.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Baraza
la Wawakilishi Nd. Yahya Khamis Hamad alipokuwa akizungumza na
Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Baraza hilo huko Chukwani nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Amesema miswada itakayojadiliwa ni
pamoja na Mswada wa Sheria ya kufuata Sheria ya Miradi ya Maridhiano
Namba 1 ya mwaka 1999, Kutunga Sheria kwa ajili ya kuazishwa na
kuendesha mashirikiano baina ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi zilizopo
nchini ikiwemo na Kuwasilishwa mbele ya Baraza, Sheria ya Kura ya Maoni
No. 11 ya Mwaka 2013 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa
kifungu 132(2) cha Katiba ya Zanzibar.
Vile vile Katibu huyo
ametanahabahisha kuwa mswada mwengine utakaojadiliwa ni pamoja na
kuanzishwa kwa Baraza la Sensa ya Filamu na Utamduni Zanzibar ambalo
litasaidia kukuza na kulinda utamaduni wa Wazanzibari.
Sambamba na hayo amesema katika
shughuli zitakazoendelea katika Baraza hilo ni pamoja na maswali na
majibu ambayo yataulizwa na kujibiwa na wajumbe wa baraza hilo ambapo
maswali 77 yanatarajiwa kujibiwa katika baraza hilo.
Katibu Yahya amewaomba Wajumbe wa Baraza hilo kufika kwa wakati barazani hapo ili kwenda sambamba na muda kwa lengo la kutimiza majukumu yaliokusudiwa katika mkutano huo.
Balozi wa China akutana na Rais Dk.Shein
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing Uholanzi
nchini Tanzania alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo (kulia) Balozi Mdogo
wa China anayefanyia kazi Zanzibar Xie Yunliang,[Picha na Ikulu.] Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing Uholanzi
nchini Tanzania alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]
Subscribe to:
Posts (Atom)