Ndugu Masaju pia ameeleza kuwa
wahalifu wanatumia fursa iliyoletwa na maendeleo ya mifumo ya
Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA) katika biashara mbalimbali
kutakatisha fedha zinazopatikana kwa njia ya uhalifu na kuzisafirisha
haraka katika nchi nyingine ili kuficha uhalisia wa mali hizo kwa
dhamira ya kuepuka kukamatwa na vyombo vya uchunguzi hapa nchini ambapo
ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo kutumia vizuri fursa waliyoipata
kujifunza na kupata majibu ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo
katika utendaji kazi ili kuongeza kuongeza ufanisi na kuhakikisha
wahalifu hawafaidiki na uhalifu wanaoufanya.
Awali, akimkaribisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw.Ayub Mwenda ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshugulikia Usimamizi na uratibu wa uendeshaji wa Mashtaka ya Jinai kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali alieleza kuwa Serikali inatoa uzito mkubwa katika suala la kukabiliana na uhalifu na mashauri yanayohusu masuala ya utakatishaji fedha hivyo nguvu na uelewa wa pamoja vinahitajika kutoka kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na kuendelea kushirikiana ili kujiimarisha zaidi katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment