N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Wednesday, March 11, 2015

Mkutano wa 19 baraza la wawakilishi kuanza jumatano


za3Katibu Mkuu Baraza la Wawakilishi Zanzibar Nd. Yahya Khamis Hamad akijibu maswali yaliyoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo. (Picha na Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar).
Na Rahma Khamis na Mwanaisha Moh’d Maelezo-Zanzibar. Mkutano wa Kumi na Tisa (19) wa Baraza la Nane (8) la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano Tarehe 11 March, 2015 saa 3:00 kamili za asubuhi ambapo miswada minne ya sheria itawasilishwa na kujadiliwa barazani hapo. Hayo yameelezwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Nd. Yahya Khamis Hamad alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Baraza hilo huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Amesema miswada itakayojadiliwa ni pamoja na Mswada wa Sheria ya kufuata Sheria ya Miradi ya Maridhiano Namba 1 ya mwaka 1999, Kutunga Sheria kwa ajili ya kuazishwa na kuendesha mashirikiano baina ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi zilizopo nchini ikiwemo na Kuwasilishwa mbele ya Baraza, Sheria ya Kura ya Maoni No. 11 ya Mwaka 2013 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa kifungu 132(2) cha Katiba ya Zanzibar. Vile vile Katibu huyo ametanahabahisha kuwa mswada mwengine utakaojadiliwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Baraza la Sensa ya Filamu na Utamduni Zanzibar ambalo litasaidia kukuza na kulinda utamaduni wa Wazanzibari. Sambamba na hayo amesema katika shughuli zitakazoendelea katika Baraza hilo ni pamoja na maswali na majibu ambayo yataulizwa na kujibiwa na wajumbe wa baraza hilo ambapo maswali 77 yanatarajiwa kujibiwa katika baraza hilo. Katibu Yahya amewaomba Wajumbe wa Baraza hilo kufika kwa wakati barazani hapo ili kwenda sambamba na muda kwa lengo la kutimiza majukumu yaliokusudiwa katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment