Kwa hisani ya
Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere leo amezungumza na waandishi wa habari,nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam juu ya uvumi ulioenea nchini kuwa amefariki Dunia.
Mama Maria amewathibitishia watanzania kuwa bado yu hai na mwenye nguvu hivyo wasiwe na hofu nae.
Alisema jana amepokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto zake, wake wa watoto zake wote, familia yake pamoja na watu mbalimbali ili kumjulia hali.
Alisema jana amepokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto zake, wake wa watoto zake wote, familia yake pamoja na watu mbalimbali ili kumjulia hali.
Amesema alipopokea taarifa hizo wala hakushtushwa badala
yake alifanya sara kwani uvumi huo wawezekana inatokana na vuguvugu la
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, pia utandawazi uliopo wa
sayansi na teknolojia wa karne ya 21.
“jana nilipokea simu nyingi sana kutoka kwa watu
mbalimbali wakiwemo watoto wangu, wake wa watoto zangu, pamoja na
familia,walikuwa wakinisalimia, wengine waliposikia sauti yangu walikata
simu” alisema Mama Maria.
Mama Maria alisema taarifa hizi za kuzushiwa kifo
si mara ya kwanza kwani hata miaka ya nyuma akiwa na hayati baba wa
Taifa, mwalimu Julius Nyerere walipokea taarifa nyingi za uvumi wa kifo.
Mjane wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumbani kwake
Msasani jijini dar es salaam leo,juu ya uvumi wa kufariki Dunia ulioenea
jana kupitia simu na mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment