N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Tuesday, January 12, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA KATIKA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO LA MKOA WA RUVUMA

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (Mb.)akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto, mbele ya Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto la Mkoa wa Ruvuma.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (Mb.) leo ametembelea Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto la  Mkoa wa Ruvuma, kwa lengo la kufuatilia hali ya Ulinzi na Ustawi wa Mtoto Mkoani humo.

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu aliwapongeza Wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto Mkoani Ruvuma kwa Ushirikiano waliouonyesha hadi kufanikisha Ujenzi wa Kituo hicho. 

Alieleza kuwa kwa Mkoa wa Ruvuma Wizara yake kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo ya Mtoto, itahakikisha inashughulikia kwa haraka tatizo la Usafirishwaji wa watoto kwenda nchi za jirani kutumikishwa katika kazi mbalimbali.

Pia aliagiza Uongozi wa Mkoa kuongeza jitihada zaidi katika kukabilina na Vitendo vya Ukatili wanavyofanyiwa Wanawake, kwakuwa Mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitatu yenye wastani mkubwa wa vitendo vya vipigo kwa wanawake.

WAZIRI KITWANGA AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE MISUNGWI, AWATAKA WANANCHI KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO FINANCIAL FITNESS CAMP ILIYOFANYIKA JANA JANUARY 9, 2016 FASTEST WAY TO FIND THE SERVICES YOU NEED MBUNGE WA JIMBO LA KIKWAJUNI MH. HAMAD MASAUDI ATEMBELEA MIRADI YA JIMBO LAKE G Classy__I Can (Laye Remake) {Official Music Video} LOOK OF THE DAY Msimamizi mkuu bomoa bomoa Dar alitekwa nyara, kuteswa jijini Haya ni majipu uchungu kwa Rais Magufuli MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA MUZDALIFAH WAFANYIKA. MISA YA KUMBUKUMBU YA MAMA BETISHEBA POLE KETANG'ENYI BALTIMORE, MARYLAND NDONDOO ZA MAGAZETI LEO Wala viwavi jeshi kuikabili njaa BAND YA SKYLIGHT SASA IMEKUJA KIVINGINE NJOOLEO UONE MAMBO MAPYA NDANI YA ESCAPE ONE Umeya wa Ilala, Kinondoni moto Samatta awafuata Dilunga, Mahadhi Bomoabomoa wakati wowote Morogoro KIJIJI CHA NANJILINJI A CHATOA RUZUKU KWA WA MAMA WAJAWAZITO

  • Posted: 10 Jan 2016 12:57 PM PST
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Kanyelele jimboni humo kabla ya kuanza mkutano wake na wananchi hao uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwakalima. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele ambapo kimeharibika. Hata hivyo, aliwataka wananchi hao waweke utamaduni wa kuchangia maendeleo ya vijiji vyao. Picha zote na Felix Mwagara.
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akimuuliza swali Diwani wa Kata ya Kanyelele, Paschal Kilangi (kulia) wakati Mbunge huyo alipokuwa akikiangalia choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele jimboni humo kilichobomoka. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho na kuwaomba wananchi wa kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.