- Posted: 10 Jan 2016 12:57 PM PSTWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Kanyelele jimboni humo kabla ya kuanza mkutano wake na wananchi hao uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwakalima. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele ambapo kimeharibika. Hata hivyo, aliwataka wananchi hao waweke utamaduni wa kuchangia maendeleo ya vijiji vyao. Picha zote na Felix Mwagara.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akimuuliza swali Diwani wa Kata ya Kanyelele, Paschal Kilangi (kulia) wakati Mbunge huyo alipokuwa akikiangalia choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele jimboni humo kilichobomoka. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho na kuwaomba wananchi wa kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akiwa na Diwani wa Kata ya Kanyelele, Paschal Kilangi (kushoto) pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kanyelele, Kudehwa Gapi (wapili kulia) wakiwa wanaikagua shule hiyo ambayo choo chake kilikuwa kimebomoka kwa kudidimia chini ya ardhi. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho na kuwaomba wananchi wa kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akikiangalia kikundi cha burudani cha Kijiji cha Mwakalima kilichokuwa kinatumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Kata ya Kanyelele jimboni humo. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Shule mya Sekondari Kanyelele kilichoharibika na kuwaomba wananchi wa Kata hiyo waanze kuchangia kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na wananchi wa Kata ya Kanyelele katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwakalima jimboni humo. Waziri Kitwanga kabla ya mkutano huo alikikagua choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele kilichobomoka na alichangia shilingi laki tano pamoja na kuwataka wananchi wa kata hiyo kuchangia fedha zaidi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.Diwani wa Kata ya Kanyelele, wilayani Misungwi, Paschal Kilangi akiwaonyesha wananchi shilingi laki tano alizotoa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Sekondari ya Kanyelele kilichobomoka shuleni hapo. Waziri Kitwanga aliwaomba wananchi wa kata hiyo kuhakikisha wanatoa michango zaidi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.Posted: 10 Jan 2016 10:20 AM PST
Camp iliyofanyika jana January 9, 2016, iliyoandaliwa na Seruwage Consulting and CPAs na kushirikisha America Classic Agency, ilizungumzia mambo mbali mbali ikiwemo, Retirement plans na jinsi ya kujiandaa na kujipanga, pia ilizungumzia maswala ya Education funds kwa watoto, Life Insurance.Camp hiyo pia ilionyesha nyia mbali mbali kwa wanaotaka kujiunga ili kuweza kutoa huduma za Bima na pia kuwa Financials advisors. Kama una swali pia 301-613-5165.Mr. Iddi Sandaly, CPA, Akielezea jambo.
Mr. Vincent Mongare, akielezea jambo.
=============================================================Posted: 10 Jan 2016 07:35 AM PSTViwango is a Tanzania-based website containing crowd-sourced reviews and ratings of local service providers. Viwango was created to help people find the best local service providers like electricians, plumbers, mechanics, handymen, hotels, restaurants, bars, coffee shops, and more. We collect reviews and ratings from consumers who have received different services from different service providers. All of our members are just like you looking for honest companies and individuals who provide high quality services. Our members provide highly detailed information regarding their experience from service providers. FASTEST WAY TO FIND THE SERVICES YOU NEED!PLEASE VISIT US AT WWW.VIWANGOTZ.COM==============================================================Posted: 10 Jan 2016 06:58 AM PSTMbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Yussuf Masauni na Aliyekuwa Mwakilishi wa Rahaleo kwa sasa ni Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salim Jazira wakiteta jambo wakati wa ziara ya Mbunge Mhe Masauni kutembelea Mradi wa Maji kaburikikombe Zanzibar.Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akiwa katika ziara yake kutembelea mradi wa kisima cha maji kaburukikombe migombani Zanzibar.Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Tanzania Youth Icon Abdalla Ahmeid akizungumza kuhusiara na mradi mkubwa wa Kisima cha Maji kilichofadhiliwa na TAYI kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar wakati wa ziara ya Mhe Mbunge Hamad Masauni katika jimbo hilo.Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Wananchi wa Jimbo hilo wakati wa ziara yake katika mradi wa maji kaburi kikombe migombani Zanzibar Mradi huo unasimamiwa na Jumuiya ya TAYI Tanzania Youth Icon kulia aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo na kwa sasa anagombea Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salim Jazira.Mgombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Abdalla Diwani akimsikiliza Mhe Mbenge wakati wa ziara yake katika kisima cha maji kaburi kikombe migombani Zanzibar.Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni akiangalia mradi wa kisima kipya kinachosimamiwa na TAYI kinachochimbwa katika eneo la Kaburi Kikombe Zanzibarb hicho kitakuwa kisima cha Pili kuchimbwa na TAYI kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kikiwa na urefu wa mita 42 kinachotarajiwa kukamilika kwake kutumia shilingi milioni 20 hadi kukamilika kwake.Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni akiangalia mradi wa kisima kipya kinachosimamiwa na TAYI kinachochimbwa katika eneo la Kaburi Kikombe Zanzibarb hicho kitakuwa kisima cha Pili kuchimbwa na TAYI kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kikiwa na urefu wa mita 42 kinachotarajiwa kukamilika kwake kutumia shilingi milioni 20 hadi kukamilika kwake.Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya TAYI Abdalla Ahmeid akitowa maelezo ya mradi huo wa Pili wa Uchimbaji wa Kisima cha Maji kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni na jirani zake kikiwa katika hatu ya mwisho ya uchimbaji wake.Katibu Mtendaji wa TAYI Abdalla Ahmeid akitowa maelezo ya uchimbaji wa kisima hicho kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya Mhe Mbunge Hamad Masauni.Afisa Rasilimali Maji wa Mamlaka ta Maji Zanzibar ZAWA Hassan Zaharan Said, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo wa kisima cha maji, wakati wa ziara ya Mhe Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.Afisa Rasilimali Maji wa Mamlaka ta Maji Zanzibar ZAWA Hassan Zaharan Said, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo wa kisima cha maji, wakati wa ziara ya Mhe Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.Aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni na Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mhe Mbunge wa Kikwajuni Zanzibar uliofanyika katika Kituo cha Jumuiya ya TAYI muembemadema Zanzibar.Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamad Yussuf Masauni na Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Abdalla Diwani wakimsikiliza mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni ambaye alikuwa Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa mkutano huo wa maadhimisho ya ziara ya Mbunge wa Kikwajuni.Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Abdalla Diwani akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mhe Masauni katika ukumbi wa Jumuiya ya TAYI muembemadema Zanzibar wakati wa kakamilisha ziara ya Mbunge wa Kikwajuni Zanzibar.Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na Wananchi wa Jimbo lake katika ukumbi wa Chuo cha TAYI muembemadema baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja kutembelea miradi ya Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.Viongozi wa Jimbo la Kikwajuni wakimsikilia Mbunge wao wakati wa ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maji na Kituo cha Vijana cha Tanzania Youth Icon muembemadema kinachotowa elimu ya Ujasiriamali kwa Vijana mbalimbali wa Jimbo la Kikwajuni na jirani zao.Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati akizungumza nao baada ya ziara yake katika jimbo hilo.Vijana wa Jimbo la jangombe wa uhamasishaji wakiwa katika ukumbi wa TAYI Miembeni wakimsikiliza Mhe, Masauni.akizungumza na Wananchi wa Jimbo lake baada ya ziara yake kutembelea Miradi ilioko katika Jimbo hlake inayosimamiwa na TAYI.Mgombea Udiwani wa Wadi ya Miembeni Mbarouk Abdalla Hanga akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mhe Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Masauni baada ya kumaliza ziara yake kutembelea miradi ya Maji ya Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni wakisoma dua baada ya kumaliza ziara ya Mhe Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Eng.Hamad Yussuf Msauni wakiwa katika Kituo cha Vijana cha TAYI muembemadema.Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.Zanzinews.com.======================================================Posted: 10 Jan 2016 02:57 AM PSTMartha Loy from Kampala, Uganda=======================================================Posted: 10 Jan 2016 02:35 AM PSTHeche SugutiAcha kuanguka na kupoteza fahamu akiwa ofisini akitoka kwenye operesheni mwanzoni mwa wiki. Imebainika kuwa Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NECM) anayesimamia zoezi la bomoa bomoa, Heche Suguti, aliwahi kutekwa na kuteswa mwaka 2012.
Nipashe limebaini kuwa Julai, 2012, tukio la kutekwa kwa Suguti liliripotiwa na vyombo vya habari ikielezwa kuwa huenda alifanyiwa kitendo hicho na waliokuwa wamewekewa alama ya X kwenye nyumba zao wakati huo.
Ilielezwa kuwa, Suguti alitekwa wakati akisimamia mpango wa ubomoaji wa mahekalu ya baadhi ya vigogo waliojenga kandokando ya mto Mbezi Beach, Mndubwe na eneo la Hifadhi ya Taifa ya Mikoko ufukweni mwa Bahari ya Hindi, jijini Dar es Salaam.
Aidha, tukio hilo lilitokea wiki chache baada ya kutekwa, kuteswa na kupigwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari (MAT), Dk. Steven Ulimboka.
Habari kutoka kwa ndugu wa karibu wa mtumishi huyo wa serikali zilieleza kuwa Suguti alitekwa nyara katika eneo la Leaders Club majira ya saa 4:00 usiku, wakati alipokwenda kupata vinywaji na chakula akiwa na na kuteswawadogo zake wawili.
Ilielezwa kuwa akiwa katika eneo hilo, ghafla liliibuka kundi la watu zaidi ya 10 ambao walimkamata Mwanasheria huyo mithili ya kibaka na kumpeleka eneo la giza na kisha kuanza kumpiga.
Ilielezwa kuwa Suguti aliteswa kwa muda na watu hao hadi alipookolewa na watu waliokuwa karibu na eneo hilo, ambao walishtushwa na kelele za kuomba msaada.
Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo zimethibitishwa na Suguti mwenyewe baada ya kutafutwa na Nipashe, tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay.
Katika kituo hicho, mwanasheria huyo alipewa PF3 na kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na majeraha aliyoyapata.
Ilielezwa kuwa kabla ya tukio hilo, mwanasheria huyo alikuwa akipokea simu na ujumbe wa vitisho kupitia ujumbe mfupi wa mkononi tangu NEMC ilipoanza taratibu za kutaka kubomoa mahekalu ya vigogo wa eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Suguti alianguka ghafla ofisini kwake Jumanne ya wiki hii na kukibimbizwa katika Hospitali moja ya jijini kwa ajili ya matibabu hadi juzi mchana aliporuhusiwa.
Licha ya kufanyiwa matibabu, vipimo vilishindwa kubaini ugonjwa unaomsumbua Suguti mara moja licha ya kuwa katika hali mbaya.
Kwa mujibu wa watu wa karibu na Suguti, mtumishi huyo anaendelea vizuri ingawa afya yake haijahimarika kiasi cha kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
NEMC kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, walianza operesheni ya kuweka alama ya X na kubomoa nyumba zilizoko maeneo hatarishi kuanzia Desemba 17 mwaka jana.
Bomoa bomoa hiyo ilisitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, siku sita mbele ili kuruhusu wananchi waweze kuhama kwa hiari yao na pia kushiriki sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Ingawa serikali juzi ilisema sasa haitabomoa tena nyumba zilizo nje ya eneo la bonde la Mto Msimbazi na mahoteli ya kitalii kwenye fukwe ya bahari ya Hindi:
Hadi juzi zaidi ya nyumba 16,000 zilikuwa zimewekewa alama ya X huku zoezi la kuzibomoa likisitishwa kupisha tathmini ya nyumba 681 zilizowekewa pingamizi Mahakama Kuu ya Ardhi kabla ya kuendelea tena kwa nyumba 16,532.
Uwekaji wa alama ya X umezikumba nyumba kadhaa za watu maarufu akiwemo Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God, Dk. Getrude Rwakatare, wachezaji wa zamani wa timu za Simba na Yanga, hoteli pamoja na uwanja wa Yanga.CHANZO: NIPASHE JUMAPILI===========================================Posted: 10 Jan 2016 02:30 AM PST
Dar es Salaam. Wakati viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano wamefanikiwa kutumbua majipu katika ukwepaji kodi, ushuru wa bandarini na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, bado kazi hiyo ya kuibua ufisadi inaonekana kuwa kubwa zaidi kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za ukaguzi na hoja zilizokuwa zinaibuliwa bungeni, kuna majipu uchungu sita yamebaki.
Suala la kampuni ya kufua umeme ya IPTL, kumalizika au kuanza upya kwa mchakato wa Katiba, mtandao wa ujangili unaopukutisha wanyama wa mwituni, mtandao wa biashara ya dawa za kulevya na mikataba mibovu na usiri wake ni majipu uchungu ambayo yanasubiri mtumbuaji baada ya kulalamikiwa kwa muda mrefu na wanaharakati, wabunge pia kubainishwa kwenye ripoti za ukaguzi.
Tangu alipoapishwa Novemba 5, Rais John Magufuli amevunja bodi za taasisi na mashirika ya Serikali, kuwasimamisha kazi na kutengua uteuzi wa vigogo mbalimbali, akiwamo katibu mkuu wa wizara, vigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Wakati akifanya hayo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliibua ufisadi mkubwa Bandari ya Dar es Salaam ambako tayari makontena takriban 14,000 yamebainika kupitishwa kinyemela bila ya kulipiwa kodi au ushuru wa bandari. Lakini wanasiasa na wadau wengine wanaona bado kuna majipu mengi ya kutumbua kama kweli Serikali imepania kupambana na ufisadi.
“Suala la IPTL lazima limalizwe,” alisema Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo,Zitto Kabwe alipoulizwa kuhusu mambo ambayo anaona yanaikwamisha Serikali katika jitihada zake za kuwahudumia wananchi.
IPTL ni kampuni ya ufuaji umeme ambayo iliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mwaka 1995, lakini ikapingwa vikali na wabunge, Benki ya Dunia na wadau wengine kutokana na gharama na teknolojia yake ya kutumia mafuta mazito.
Tangu kampuni hiyo iingie mkataba huo, imekuwa ikikumbana na tuhuma zinazoibuka kila mara tatizo la umeme linapojitokeza, ikidaiwa kuwa Serikali inalipia fedha nyingi katika mkataba wake na Tanesco.
Hoja ya kila mara ya wabunge kwamba suala hilo lifikishwe mwisho kwa Serikali kutaifisha mitambo hiyo kama ilivyokubaliwa katika mkataba huo wa takriban miaka 20 iliyopita, haijatekelezwa.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye alisimama kidete kutetea kuwa fedha zilizochotwa kwenye sakata jingine la umeme la Akaunti ya Tegeta Escrow si za Serikali, atalazimika kuibua uozo uliozunguka sakata hilo la IPTL ili kumaliza tatizo hilo. Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David Kafulila alisema hadi sasa kuna wahusika hawajachukuliwa hatua stahiki.
Kafulila alisema Rais Magufuli anapaswa kumchukulia hatua katibu mkuu wa Wizara ya Fedha ambaye alimpa ushauri Mwanasheria Mkuu wa Serikali kusamehe kodi ya Sh21 bilioni wakati akijua wazi kuwa mamlaka ya kusamehe kodi ni ya Waziri wa Fedha.
“Hata Gavana wa Benki Kuu naye ni jipu maana alipohojiwa kuhusu suala la escrow alikiri kushauriwa vibaya. Eliakim (Maswi-sasa Kaimu Naibu Kamishna TRA) na Profesa Muhongo nao wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa sababu hawajatutajia waliobeba fedha kwenye viroba,” alisema Kafulila.
Mtandao wa majangili
Mbali na suala la IPTL, jipu jingine lililotajwa na wadau ni kuuvunja mtandao wa ujangili. Wakati idadi ya tembo ikiendelea kupungua, nyara za Serikali zimekuwa zikipitishwa mipakani na kukamatwa nje ya nchi, jambo ambalo hata Rais Magufuli alishasema linashangaza kutokana na mamlaka husika nchini kushindwa kubaini mtandao huo.
Februari 14 mwaka jana, Rais mstaafu Jakaya Kikwete wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC alisema Serikali imeubaini mtandao wa ujangili unaojumuisha watu 40, akiwamo tajiri maarufu mkoani Arusha lakini mpaka sasa haujawekwa wazi.
Vigogo dawa za kulevya wanajulikana
Jipu jingine ambalo limekuwa gumu kutumbuliwa ni kufichua mtandao wa biashara ya dawa za kulevya, licha ya viongozi kueleza mara kadhaa kuwa wanawafahamu wahusika.
Tanzania imekuwa njia ya kupitishia au kituo cha dawa za kulevya aina ya heroin, cocaine, mandrax na morphine na mara kadhaa mizigo imekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kiwango kikubwa kukamatwa nje ya nchi baada ya kupita katika uwanja huo.
Wabunge wamekuwa wakipiga kelele kila mara kutaka Serikali iwafichue wahusika ambao wanatajwa kuwa ni vigogo wa Serikali, wafanyabiashara wakubwa na maofisa wa polisi, lakini hadi sasa wanaokamatwa ni wale wanaobeba na si walio kwenye mtandao.
“Matukio yote haya yametokea katika kipindi cha utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne. Kuna viongozi wa juu serikalini ambao waliwahi kusema kuwa wanawajua wanaojishughulisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, lakini mpaka sasa hawajawataja na wala hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa,” alisema msemaji wa kambi ya upinzani, Mohamed Mbarouk wakati akitoa hotuba ya kambi hiyo kuhusu muswada wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya ya Mwaka 2014. Aliwataja viongozi waliotoa kauli hiyo kuwa ni Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Kikwete, Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
Hadi sasa, usafirishaji wa dawa hizo unaendelea huku polisi wakikamata watu wanaoonekana kuwa wanatumwa.
Kitendawili cha mchakato wa Katiba
Wakati Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akisema amepewa jukumu la kumalizia mchakato wa kuandika Katiba Mpya kwa kuanzia pale ulipoishia, suala hilo linaonekana kuwa jipu jingine kwa Serikali ya Magufuli.
Wanasiasa, wanaharakati na wadau hawakubaliani na jinsi mchakato huo ulivyoendeshwa na wengi wanaona kuwa unatakiwa uanzie kwenye Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na mwenyekiti wa ilivyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba na liundwe Bunge jipya la Katiba ambalo halitatawaliwa na itikadi za kisiasa.
Lakini CCM inataka Katiba Inayopendekezwa ndiyo ipigiwe kura kumalizia mchakato huo, jambo ambalo limeshaonyesha kuwa litasababisha kutofautiana tena na Jaji mstaafu Warioba ambaye wiki iliyopita alikutana na Rais Magufuli.
Akizungumzia suala la Katiba, mkurugenzi wa utetezi na maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alisema wizara hiyo inatakiwa itunge sheria mpya ili watakaoshiriki katika mchakato wa kupata Katiba Mpya, wasiruhusiwe kujihusisha na masuala ya kisiasa kwa muda wa miaka 10. Alisema kukosekana kwa sheria madhubuti kulisababisha mchakato wa Katiba kutekwa na wanasiasa ambao walikuwa wanachangia hoja, kutoa mawazo kwa matakwa yao ya kisiasa badala ya masilahi ya nchi.
Migogoro ya ardhi
Wakati mchakato wa Katiba ukisumbua, matatizo yanayosababisha mapigano baina ya wakulima na wafugaji na kupoteza uhai wa watu na mifugo, migogoro ya wananchi na wawekezaji na uvamizi wa maeneo yasiyoruhusiwa kwa ujenzi, yanaonekana kutopatiwa ufumbuzi.
Imekuwa ikielezwa kuwa matatizo hayo yamekuwa yakitokana na ardhi kutopimwa na kugawanywa vizuri, lakini jipu linalosababisha mizozo yote hiyo bado halijatumbuliwa.
Maeneo yaliyokithiri kwa migogoro hiyo ni mikoa ya Manyara, Arusha na Morogoro ambako mapigano hutokea mara kwa mara.
Profesa wa uchumi katika kilimo wa Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua), Damian Gabagambi alisema tatizo kubwa la migogoro ya wakulima na wafugaji ni nchi kutopima ardhi yake ili kubainishwa matumizi ya kila mahali.
Rais Magufuli alishasema wakati wa kampeni kuwa atahakikisha waziri anayehusika, mkuu wa mkoa na wilaya husika na kamanda wa polisi wa eneo litakalokumbwa na mapigano baina ya wakulima na wafugaji, hatabakia kwenye wadhifa wake.
Mikataba mibovu
Wakati wabunge wamekuwa wakipiga kelele mikataba mibovu na usiri wake, bado suala hilo limekuwa kama kutwanga maji kwenye kinu; hakuna anayefanyia kazi kilio hicho.
Hadi sasa, hakuna aliyeadhibiwa kwa kuiingiza nchi kwenye mikataba mibovu ambayo inapukutisha utajiri wa nchi.
Profesa Abdallah Safari alisema mikataba hiyo imesababisha nchi kupata fedha kidogo kutoka kwenye rasilimali zake.
“Huwezi kusema kila mtu alipe kodi huku mikataba ya madini ikiwaruhusu wawekezaji kuchimba madini na kulipa kodi baada ya miaka mitano, nadhani huko ndiko kuna fedha nyingi inayopotea,” alisema.============================================================Posted: 10 Jan 2016 02:00 AM PSTBaadhi ya washiriki katika Mkutano Mkuu wa mwaka2015 wa Jumuiya ya Muzdalifah Islamic Charitable wakimsikiliza kwa makini mwenyekiti hayupo pichani wakati akitoa maelezo kuhusiana na muzdalifah na kumkaribisha mgeni rasmi katika Ukumbi wa Kidongo Chekundu (MENTAL) Zanzibar.Katibu Mkuu wa Muzdalifah Farouk akitoa maelwzo kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu na Kufungua Mkutano huo katika Ukumbi wa Kidongo Chekundu (MENTAL) Zanzibar.Mkutano huo katika Ukumbi wa Kidongo Chekundu (MENTAL) Zanzibar.-Mwenyekiti wa Muzdalifah Sheikh Abdalla Hadhar akitoa kuhusiana na muzdalifah na kumkaribisha mgeni rasmi katika Ukumbi wa Kidongo Chekundu (MENTAL) Zanzibar.-Mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Jumuia ya Muzdalifah Mkurugenzi kutoka idara ya Mikopo Zanzibar Suleiman Haji akizungumza na wafanyakazi wa Muzdalifa katika Mkutano mkuu wa Muzdalifa katika Ukumbi wa Kidongo Chekundu (MENTAL) ZanzibarMjumbe wa Mkutano Mkuu Salim Rashid akitoa mchango wake kuhusiana na maendeleo ya Muzdalifah katika Ukumbi wa Kidongo Chekundu (MENTAL) Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.======================================================Posted: 10 Jan 2016 12:49 PM PSTPadri Honest Munishi wa kanisa Katoliki la Mt. Edward la Baltimore, Maryland akiongoza misa ya kumbukumbu ya mama Betisheba Pole Ketang'enyi iliyofanyika siku ya Jumamosi January 9, 2016 na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki.John Kyoma kutoka Dallas, Texas akisoma somo la kwanza.Mama Mukami akisoma somo la piliMr and Mrs Sims wakisoma wasifu wa Mama Betisheba Ketang'enyi.Frederick Ketang'enyi akitoa shukurani za familia.Padri Honest Munishi akifanya maombi kwa familia.Familia ikiwasha mshumaa kwenye picha ya mama yao.Familia ikiwa katika picha ya pamoja.
=========================================================Posted: 10 Jan 2016 12:57 AM PST
Chamwino.Wakazi wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wanakula wadudu jamii ya viwavi jeshi, wanaojulikana kwa jina la fumbili kutokana na njaa kali iliyoikumba wilaya hiyo.
Hata hivyo, chakula hicho huenda kikapotea wakati wowote kutokana na mvua kutonyesha hivyo wadudu hao, ambao huishi kwa kutegemea majani, nao kupotea kwa kukosa chakula.
Mbali na fumbili, chakula kingine ambacho kilikuwa mkombozi kwa wakazi wengi, hususan Tarafa ya Chilonwa, ni matunda ya zambarau ambayo nayo yatakwisha wakati wowote kwani msimu wake umekwisha.
Chamwino ni wilaya iliyoko takriban kilomita 30 kutoka mjini Dodoma, ikikadiriwa kuwa na watu 349,714 na mazao ya chakula yanayolimwa kwenye wilaya hiyo ni mtama, uwele, mpunga, mahindi, mihogo, viazi vitamu, kunde, nyonyo, mbogamboga na choroko.
Juzi, Mbunge wa Chilonwa, Joel Mwaka aliitisha kikao cha dharura cha madiwani wote wa jimbo hilo lenye kata 14 kujadili suala hilo na kila diwani aliyechangia mjadala huo, alionyesha kujuta kugombea kwa kuwa wananchi wanamlilia.
Madiwani hao waliweka azimio la kusafiri kwenda Ikulu, Dar es Salaam kuwasilisha kilio cha wananchi wao.
Akizunguma kwenye kikao hicho, Mwaka alisema hali ya wakazi wa Chilonwa ni mbaya kiasi hakuna matumaini hata ya kupata mlo mmoja na badala yake wengi wanaishi kwa uji na matunda pori na fumbili.
Mbunge huyo alilaani mpango wa Serikali wa kuwapa vibali wafanyabiashara kwenda kuchukua mahindi katika ghala la chakula la Songea kwani bei zinakuwa kubwa.
“Ndiyo maana wanyabiashara wengi walikataa kwa kuwa bei inakuwa ni kubwa ambayo haiwezi kurudisha hata gharama zao, kitendo hicho kimefanya wafanyabiashara wa kawaida kuendelea kuwaumiza wananchi, lakini hakuna mwenye uwezo kipindi hiki, nasema walete mahindi ya bure siyo ya kununua tena,” alisema Mwaka.
Mbunge huyo alihoji ni kwa nini Serikali isiruhusu ghala la mahindi la Kizota, Dodoma kutoa mahindi kwa wafanyabiashara ili bei isiwe kubwa kama ilivyo sasa. Alisema bei ya sasa ya Sh15,000 kwa debe la kilo 20 ni kubwa na wachache ndiyo wanaoweza kuimudu.
Diwani wa Majeleko, Mussa Omari alifika kwenye kikao hicho akiwa na fumbili wengi akisema aliwakamata wakati akishirikiana na wapigakura wake kupata kitoweo.
Hata hivyo, hakuna diwani aliyeonyesha mshangao kwani kila mmoja alisema hata kwake wanakula wadudu hao na ni jambo la kawaida.
Mussa alisema hali ni mbaya zaidi kwenye kata yake na tayari baadhi ya watu wameanza kuvimba miguu kwa kukosa chakula, huku kukiwa na taarifa za vifo vinavyosadikiwa kuwa vimetokana na watu kukosa lishe.
Diwani wa Zajilwa, Farida Maulidi alisema katika eneo lake, kuna kaya 10 ambazo zimeelemewa zaidi na tayari kuna taarifa za vifo viwili. “Kwangu hali ni mbaya sana yaani naomba tuandamane kwenda hata kwa mkuu wa mkoa au niungane na wenzangu twendeni Ikulu tukamuone Rais. Mbona, pamoja na kusema hakuna mtu atakayekufa kwa njaa, huku watu wanateketea na sisi tupo? Kila siku nafanya kazi ya kutafuta uji kunusuru maisha ya watu wangu,” alisema Maulid.
Ofisa kilimo wa wilaya hiyo, Godfrey Mnyamale alikiri kuwa hali ni mbaya wilayani Chamwino na kusema kama juhudi za makusudi hazitachukulia ndani ya wiki moja, kutakuwa na madhara makubwa.
Mnyamale alisema tatizo kubwa lililoikumba Chamwino ni mvua kidogo zilizonyesha msimu wa mwaka jana iliyosababisha watu wasivune chakula cha kutosha.
Alisema ili kukabiliana na njaa iliyoanza wilayani humo tangu Aprili mwaka jana, jumla ya tani 14,377 za mahindi zinatakiwa kwenye vijiji 107, lakini hadi sasa Serikali imepeleka tani 150 tu ambazo ziligawiwa katika vijiji 10 tena kwa idadi ndogo.
Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa alisema Serikali haijalala katika kuwaza namna ya kuwasaidia.
Galawa alisema katika kipindi kilichopita, Chamwino ilipewa msaada wa chakula lakini kilikuwa hakitoshi na ndiyo sababu hakikupelekwa maeneo yote.
“Hata hivyo, lazima watu wajue kuwa huwezi kuomba chakula leo na ukapewa leo. Leo kamati ya mkoa imeshapeleka maombi taifa na juzi niliongea na mhusika kwamba wanalifanyia kazi,” alisema Galawa.
Kuhusu wafanyabiashara kulazimishwa kununua mahindi Songea badala ya Dodoma, alisema jambo hilo liko nje ya uwezo wake kwa kuwa wenye kuwapangia ni mamlaka ya chakula.
Aliwataka wanasiasa kuacha kukuza mambo kuwa kuna watu wamekufa kwa njaa, badala yake watumie muda huo kuwahamasisha wafugaji kuuza mifugo na kununua chakula.================================================================Posted: 09 Jan 2016 11:09 PM PSTMwimbaji wa Bandi ya Skylight, Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) uku akisindikizwa na Natasha(kulia) pamoja na Leah ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita sasa leo sio siku ya kukosa njoo ujionee mambo mapya kutoka kwenye bandi ya Skylight.Sam Mapenzi akiongoza marapa wenzake wa Skylight Band, Suzy na Sony Masamba kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.Waimbaji wa bendi ya Skylight, Joniko Flower na Sony Masamba wakiendelea kutoa burudani mbele ya mashabiki wao ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar.Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwasebenesha sehemu ya mashabiki pamoja na waimbaji wa bendi hiyo ndani ya Jumapili iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.Mashabiki wakiendelea kuziludi ngoma za Skylight ndani ya kiota cha Escape one jumapili iliyopita.Mwananziki wa bendi ya Skylight Sony Samba akiimba moja ya sebene la bendi hiyo uku waimbaji wa Skylight wakendelea kuserebuka ndani ya Kiota cha Escape One MikocheniRapa Mkongwe wa
.
No comments:
Post a Comment