Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (Mb.)akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto, mbele ya Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto la Mkoa wa Ruvuma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (Mb.) leo ametembelea Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto la Mkoa wa Ruvuma, kwa lengo la kufuatilia hali ya Ulinzi na Ustawi wa Mtoto Mkoani humo.
Wakati wa ziara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu aliwapongeza Wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto Mkoani Ruvuma kwa Ushirikiano waliouonyesha hadi kufanikisha Ujenzi wa Kituo hicho.
Alieleza kuwa kwa Mkoa wa Ruvuma Wizara yake kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo ya Mtoto, itahakikisha inashughulikia kwa haraka tatizo la Usafirishwaji wa watoto kwenda nchi za jirani kutumikishwa katika kazi mbalimbali.
Pia aliagiza Uongozi wa Mkoa kuongeza jitihada zaidi katika kukabilina na Vitendo vya Ukatili wanavyofanyiwa Wanawake, kwakuwa Mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitatu yenye wastani mkubwa wa vitendo vya vipigo kwa wanawake.
No comments:
Post a Comment