Rais wa Zambia Rupiah Banda amekubali kushindwa kwake na kiongozi wa upinzani Michael Sata.
Bw Sata, aliyegombea urais mara nne, alitangazwa kuwa mshindi usiku baada ya kupata asilimia 43 ya kura zote.
"Watu wa Zambia wamezungumza na lazima sote tusikilize," Bw Banda aliwaambia waandishi wa habari, huku akifuta machozi baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.
Chama chake cha Movement for Multiparty Democracy kimeongoza Zambia kwa miaka 20.
"Nikizungumza kwa nafsi yangu na chama changu, tunakubali matokeo. Sisi ni chama cha kidemokrasia na hakuna namna nyingine yeyote ile," Bw Banda alisema.
Siku ya Alhamis, kulikuwa na ghasia eneo la kaskazini lenye migodi zilizofanywa na wanaounga mkono upinzani wakiwa hawana subra na matokeo ya Jumanne.
Matokeo hayo yalitangazwa huku majimbo saba yakiwa bado kura zao kuhesabiwa, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema Bw Banda hatoweza kumfikia Bw Sata.
Mwandishi wa BBC Louise Redvers kwenye mji mkuu, Lusaka, alisema kuhusu tangazo hilo, wasiwasi uliogubika matokeo hayo ulisababisha makelele huku wafuasi wa Patriotic Front wakishangilia ushindi wao.
Maelfu ya watu walifurika nje ya geti lenye ulinzi mkali wakipiga ngoma, wakipiga honi na kupeperusha bendera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Rais Mstaafu wa Zambia,Mh. Ruphia Banda kwenye ofisi za Mahakama Kuu ya Zambia wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Michael Sata zilizofanyika jana mjini Lusaka Zambia.
(Picha na Amour Nassor VPO).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini,John Tendwa kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata mjini Lusaka jana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia), Mama Asha Bilal (kulia) na Rais mstaafu wa Zambia Ruphia Banda, wakimsikiliza Rais mpya wa Zambia Michael Sata alipokuwa akijitambulisha kwa viongozi wakuu wa Nchi mbalimbali waliohudhuria kwenye sherehe ya kuapishwa kwake iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia
katikati ni Mama Asha Bilal.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) na mkewe Mama Asha Bilal (wa pili kushoto), Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa (kushoto) na Rais wa kwanza wa Zambia,Dkt. Keneth Kaunda wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia
Tukio la Madereva wa Mabasi ya masafa marefu kutoka Mbeya kugoma kuendesha mabasi yao kwa kulalamikia 'TOCHI' nyingi barabarani limenishangaza sana, kwa faida ya wasioelewa, TOCHI ni Kamera za usalama barabarani zinazotumiwa na Matrafiki kuangalia magari yanayokwenda mwendo wa kasi katika eneo ambalo hawastahili kwenda mwendo huo.
KAPINGAZ Blog inapata shaka kidogo, ni kweli hao Madereva wanagomea TOCHI! au kuna kitu kingine Chini ya kapeti? nadhani wao madereva wanalijua hili. Wosia wangu, kama Madereva wanagomea TOCHI kama TOCHI isitende kazi yake, nitapingana nao kwa asilimia 100; ila kama kuna lingine nje ya hapo nawasapoti vile vile kwa asilimia hizo hizo.
"TAFADHALINI, TAIFA BADO LINAZIHITAJI NGUVU HIZI ZA WATANZANIA WANAOPOTEA KILA SIKU KWENYE AJALI AMBAZO NYINGI ZINASABABISHWA NA UZEMBE"
Tumepokea ombi la kusogeza mbele kwa siku moja mechi iliyotajwa hapo kutokana na Uwanja wa CCM Kirumba kuwa awali ulikuwa umeombwa kwa ajili ya shughuli nyingine ya kijamii inayofanyika kesho (Septemba 25 mwaka huu).
Ombi hilo limekubaliwa, hivyo mechi kati ya Toto Africans na Oljoro JKT sasa itachezwa Jumatatu ya Septemba 26 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Nawatakiwa mchezo mzuri ambao bila shaka utakuwa burudani tosha kwa mashabiki wa mpira wa miguu wa Mwanza na mikoa ya jirani.
Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoongozwa na Kamishna wa Polisi mstaafu Alfred Tibaigana imempiga faini ya sh. 500,000 na kuwekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu baada ya kumuona ana hatia kwa mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake na TFF.
Uamuzi wa kamati hiyo iliyokutana leo (Septemba 24 mwaka huu) umetokana na ushahidi uliowasilishwa na TFF, na pia Sendeu mwenyewe kukiri kuwa alifanya makosa.
Sekretarieti ya TFF ilimshtaki Sendeu kwenye kamati hiyo kutokana na matamshi yake dhidi ya mwamuzi Alex Mahagi mara baada ya mechi kati ya Yanga na Ruvu Shooting iliyochezwa Septemba 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Sendeu aliita mkutano na waandishi wa habari na kumshutumu Mahagi kuwa alisababisha timu yake ikose ushindi kwa kuwabeba wapinzani wao na kudai anamfahamu Mahagi kuwa ni mwanachama wa Simba, kadi nyekundu aliyompa kiungo wao Haruna Niyonzima si halali na alifanya hivyo kwa lengo la kuisadia Simba ili iendelee kukaa kileleni mwa ligi.
Kauli hiyo ililenga kumjengea chuki Mahagi mbele ya mashabiki wa Yanga kama ilivyo kwa viongozi na watendaji wa TFF wakati Sendeu akiwa ofisa wa Yanga alikuwa anajua taratibu za kufanya pale klabu yake isiporidhishwa na uamuzi wa mwamuzi au suala lingine lolote.
Kamati hiyo haikusikiliza mashtaka dhidi ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage kwa vile hakufika kwenye kikao kutokana na kuwa katika kampeni za uchaguzi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora.
Pia kamati hiyo haikusikiliza mashtaka ya kwanza ya Sendeu kwa vile yanakwenda pamoja na yale ya Rage. Kamati itapanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusikiliza mashtaka dhidi ya viongozi hao ambapo watapewa taarifa.
Wakati michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara inayoshirikisha timu 18 imepangwa kuanza Oktoba 15 mwaka huu timu ambazo hazijakamilisha usajili wa wachezaji zimeongezewa muda hadi Oktoba Mosi mwaka huu.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Septemba 24 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais, Ramadhan Nassib pia imepanga makundi ya ligi hiyo itakayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Oktoba 3-9 mwaka huu majina ya wachezaji walioombewa usajili na timu zote 18 yatabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa TFF kwa ajili ya pingamizi, na Kamati ya Mashindano itakutana Oktoba 10 mwaka huu kwa ajili ya kupitia majina hayo.
Kundi A litakuwa na timu za Mgambo Shooting Stars ya Tanga, Morani ya Manyara, Polisi Dar es Salaam, Temeke United ya Dar es Salaam, Transit Camp ya Dar es Salaam na Burkina Faso ya Morogoro.
Timu zinazounda kundi B ni Majimaji ya Songea, Mbeya City Council, Mlale JKT ya Ruvuma, Polisi Iringa, Small Kids ya Rukwa na Tanzania Prisons ya Mbeya. Kundi C ni 94 KJ ya Dar es Salaam, AFC ya Arusha, Polisi ya Morogoro, Polisi ya Tabora, Rhino Rangers ya Tabora na Samaria ya Singida.
Leo, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) inayomiliki kinywaji cha Tusker, inazindua kampeni mpya kusheherekea ubora na urithi wa kinywaji hicho uliodumu tangu ilipoingia nchini mwaka 1922.
Tusker inayozalishwa Tanzania kwa vimelea asilia kwa 100% inaonyesha uasilia wa kinywaji cha Afrika kwa 100%. Kampeni hiyo itakayokuwa na hamasa za kipekee itahusisha Matangazo ya mvuto wa kipekee,Ubalozi maalumu kuwakilisha kinywaji cha Tusker na Matukio ya kipekee katika maeneo mbalimbali nchi nzima katika Promosheni maalumu itakayojulikana kama Tusker ‘Life and Soul’.
“Ikiwa ni bia ya pekee iliyokuwepo wakati Tanzania ikipata uhuru wake mwaka 1961, Kinywaji cha Tusker kimeendelea kuwa na ladha yake ya kipekee na ubora wa kipekee tangu wakati huo”, alisema Ephraim Mafuru,Mkurugenzi wa Masoko wa SBL.
Aliongeza kusema kuwa “Tusker imekuwa kinywaji bora kwa wakati wote na kimekuwa kinywaji kinachoweza kutumika katika sherehe na hafla mbalimbali huku kikitumika kuwakusanyana kuwaweka pamoja watu wenye rika na hulka tofauti katika maisha ya kila siku”,
Alisema promosheni ya kitaifa kwa wateja wote iliyomalizika hivi karibuni iliyojulikana kama ‘Tusker Milioni 500 kwa Mashabiki’ ilikuwa ya mafanikio makubwa ambapo zaidi ya watanzania 121 walijazwa mamilioni ya shilingi.
“Tunajivunia kinywaji cha Tusker ambacho kupitia promosheni hiyo kimeweza kutengeneza mamilionea ambao kwa hakika fedha hizo zimeingia katika uchumi wa Tanzania”, alisema Mafuru
Alisema kinywaji hicho pia kinajivunia udhamini wake katika shindano la Tusker All Stars ambapo Peter Msechu mwakilishi wa Tanzania alishiriki katika mashindano ya kimataifa yaliyofanyika Nairobi, Kenya wiki chache zilizopita.
Kwa upande wake, Meneja wa kinywaji hicho Rita Mchaki alisema “Kujihusisha kwetu katika matukio tofauti ya kihuduma katika taifa hili kunatupa ujasiri wa kujivuna na kutembea kifua mbele”.
Mchaki alisema kinywaji cha Tusker kitaendelea kusaidia mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika maeneo tofauti katika kuhakikisha jamii ya kitanzania inakuwa na maisha bora.
“Tuna furaha kushiriki na jamii ya kitanzania katika kampeni yetu mpya ambayo itaanza hivi karibuni.Tunaomba watanzania waangalie mara kwa mara matangazo yetu yatakayoanza kurushwa hivi karibuni”, alisema.
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRMF) limehamisha mechi ya kundi D ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco kutoka Casablanca na sasa itachezwa Marrakech.
Mechi hiyo itachezwa saa 1.30 jioni Oktoba 9 mwaka huu. Pia Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo ziko kundi hilo zitacheza Oktoba 9 mwaka huu na muda huo huo ili kuepuka kupanga matokeo. Mechi hiyo itachezwa jijini Algiers.
Kwa vile hakuna mashirika ya ndege ya kimataifa yanayokwenda Marrakech, FRMF ndiyo itakayogharamia usafiri wa Taifa Stars kutoka Casablanca hadi Marrakech. Kwa mashabiki wa Tanzania wanaotaka kwenda kuishangilia Taifa Stars nauli kwa ndege za Morocco kutoka Casablanca- Marrakech- Casablanca ni dola 120.
Waamuzi wa mechi kati ya Stars na Morocco watakuwa Gassama Bakary, Jawo Dickory, Touray Sulayman na Camara Bakary, wote kutoka Gambia. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Zoumaro Gnofame kutoka Togo.
Kocha Jan Poulsen anatarajia kutangaza kikosi Septemba 26 mwaka huu kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco na kitaingia kambini Septemba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
JAMII imeshauriwa kujiunga na mfumo wa kisasa wa usimamizi wa vyombo vya habari wa kampuni ya Push Observer
Na Mwandishi wetu
JAMII imeshauriwa kujiunga na mfumo wa kisasa wa usimamizi wa vyombo vya habari wa kampuni ya Push Observer ili kuweza kupata taarifa mbalimbali sahihi za kisiasa, kiuchumi, kibiashara na kiafya.
Wito huo ulitolewa na gwiji la masuala ya usimamizi wa vyombo vya habari, Joe Taylor kutoka Marekani katika hafla fupi iliyowakutanisha wafau mbali mbali wa sekta ya habari, uchumi na biashara.
Bw. Taylor alisema kuwa kila mtu anawajibu wa kujua mambo mbali mbali kuhusiana na jamii na njia halisi ni kuputia mfumo wa kisasa (Digital Media Monitoring) ambao urekodi na kuhifadha taarifa hizo.
Alisema kuwa mfumo huo umeenea sana nchi za Amerika na Ulaya na kuishukuru kampuni ya Push Observer kuanzisha utaratibu huo ambao pia usaidia waandishi wa habari na wanafunzi.
Alifafanua kuwa kwa wafanya biashara, mfumo huo ndiyo utawapa mwanga zaidi wa biashara zao kwani utawawezesha kujua mwenendo wa biashara yake, kujua mpinzani au mshindani anafanya nini katika soko husika.
“Ni muhimu kwa wafanyabiashara kupata taarifa sahihi za mwenendo wa biashara husika, makampuni mengi nchi za Marekani na Ulaya yamefanikiwa kutokana na kutumia mfumo huo kwani biashara bila taarifa sahihi ni hasara,” alisema Taylor.
Afisa Mwendeeshaji Mkuu wa Push Observer, Omari Salisbury akimshukuru Bw. Taylor kwa ujio wake na kutoa mwanga wa mfumo huo ambao Tanzania haujaenea sana.
Salisbury alisema kuwa tokea kuanzishwa kwa kampuni yake, mpaka sasa makampuni sita yamejiunga na yanafanya vizuri katika soko.
“Kwa kweli tumefarijika sana na ujio wa Bw. Taylor na tunaamini wadau mbali mbali mbali pamoja na waandishi wa habari watafika katika ofisi zetu ili kupata kumbukumbu taarifa mbali mbali.
Alisema kuwa wameamua kuanzisha kampuni hiyo ili kuiweka Tanzania katika ramani ya kisasa ya mambo ya usimamizi wa vyombo vya habari na kuwapa taarifa wadau masuala ya kijamii kuweza kupata maendeleo ya kisasa.
Participants of a Good Governance workshop, in a group picture with the Minister of State in President’s Office Responsible for Good Governance Hon. Mathias Chikawe shortly after he opened a workshop on good governance organized by Oikocredit Tanzania. Oikocredit which is one the world’s largest sources of private funding to the microfinance sector, has so far loaned out Tshs44 billion to 44 Saccos in Tanzania. The workshop was held at Kuduchi Beach Hotel in Dar es Salaam this week.
Participants of a four-day good governance workshop,follow a lecture on good governance related topic in Dar es Salaam on Wednesday. The workshop has been organized by Oikocredit which is one the world’s largest sources of private funding to the microfinance sector. Oikocredit has so far loaned out Tshs44 billion to 44 Saccos in Tanzania. The workshop was held at Kuduchi Beach Hotel in Dar es Salaam this week.
Upi ? Msimamo wa viongozi wa nchi Afrika kuhusu Libya?
Je ? wanamtambua kiongozi halali wa Libya?
Vipi ? kiongozi wa waasi Mustafa Abdel-Jalil anatambulika na Viongozi wetu?
Wakati viongozi wa nchi mbali mbali wamekutanika mjini New York,kwa ajiliya mkutano wa umoja wa mataifa UN,katika mkusanyiko huo wamo pia viongozi
wetu kutoka nchi za kiafrika ambao pia ni wanachama wa umoja wa Afrika AU,
ambayo Libya pia ni mwanachama wa AU,lakini utata unakuja nani kiongozi halali
wa nchi hiyo Libya? Kanal Gaddaf au Mstafa Abdel-Jalil ambaye nae yupo huko
New York.
Swali lingine kubwa ambalo wengi wetu tunajiuliza je ?viongozi wa nchi za
Afrika wanautambua uhalali wa Mstafa Abdel- Jalil ?kama hawautambui
je? watakubali kuwepo ukumbini na kumsikiliza otuba ya kiongozi huyo aleyeingia
madarakani kwa njia ya bunduki tena kwa kusaidiwa na NATO? au watakuwepo
ukumbini kwa mithali za kiswahili kila moja na lwake? yaani ya Ngoswe muachie
Ngoswe! je? fadhila za Kanal Gaddaf na mchango wake katika bara la Afrika
ndio zitakua zimesauliwa.
Mengi tunajiuliza lakini siye wafrika tunategea sikio uko UN kusikiliza msimamo
wa viongozi wetu juu ya kauli ya pamoja kuhusu maslahi ya bara la Afrika.
Rais Kikwete ang'ara katika ufunguzi wa mkutano wa DICOTA 2011 jijini Washington DC leo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Watanzani nchini Marekani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Diaspora Council of Tanzania in America (DICOTA) 2011 huko Dulles, Virginia, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika (Picha na Mawasiliano Ikulu).
Wafadhili toka taasisi mbalimbali za umma na binafsi waliofanikisha DICOTA 2011 wakipozi na Rais Kikwete na Meza kuu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe akiongea kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete kuhutubi hadhira na kufungua rasmi mkutano wa DICOTA 2011
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa washiriki baada ya kutembelea banda la Nyumba Poa katikati ni Peter Mariki Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyumba Poa Ujumbe mzito toka NSSF ukiwa mkutanoni
MWENYEKITI WA TAASISI YA WAMA MAMA SALMA KIKWETE AKAGUA SHULE YA WAMA NAKAYAMA TARAYI KWA UZUNDUZI
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati akiongoza na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA iliopo Nyamisati Rufiji mkoa wa Pwani (kushoto) Twaha Twaha (mwenye tai) pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo Suma Mensah (kulia) Sept.3.2011 kwaajili ya ukaguzi wa maandalizi kabla ya ufunguzi rasmi wa shule hiyo Sept.29.2011 utakaofanywa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Mohammed Shein . (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (mwenye miwani) pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA Mwalimu Msaidizi Suma Mensah iliopo Nyamisati Rufiji mkoa wa Pwani wakikagua mazingira ya shule Sept.23.2011 kabla ya ufunguzi rasmi wa shule hiyo Sept.24.2011 itakayofunguliwa rasmi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt, Mohammed Shein. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Msanii mashuhuri na Mbunge wa Viti maalumu Vicky Kamata akiwa katika mazoezi ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya wasichana ya WAMA NAKAYAMA huko Nyamisati Mkoa wa Pwani kwaajili ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo Sept.24.2011 utakaofanywa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt, Mohammed Shein. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA huko Nyamisati Mkoa wa Pwani wakifanya mazoezi ya kimba wimbo maalumu Sept,23.2011 kwaajili ya uzinduzi rasmi wa Shule yao Sept.24.2011 utakaofanywa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar DDkt. Mohammed Shein. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).