Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(Kulia) na Eng -Msaidizi wa Temesa Ngome Rajabu, wakiwasili kwenye Eneo la Kivuko cha Mv-Kilombero juzi, ambako walikwenda kushughulikia Kivuko cha Mv-Kilombero II kilichokuwa kimeharibika injini moja, lakini hata hivyo walifanikiwa baada ya kuagiza injini mbadala kutoka Songea,
Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru, akiendelea na zoezi la Ukaguzi wa Kivuko ambacho kilidaiwa kuharibika na hivyo kusitisha huduma ya usafirishaji,
Kutokana na hali hiyo, Wakazi wa Mahenge walilazimika kutumia usafiri wa Mitumbwi, kwani kivuko cha Mv-Kilombero I akikuweza kukidhi haja za kuondoa msongamano uliokuwapo kabla ya kutengemaa kwa MV-Kilombero II.
Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(wa pili kulia) akitafakari na baadhi ya watendaji wa TEMESA ambao walifuatana naye kushughulikia Tatizo la Usafiri lililokuwa limejitokeza Kilombero.
Fundi wa mashine akisimamiwa na eng wa Temesa, kutafuta kifaa kilichodaiwa kusababisha kutofanya kazi kwa kivuko cha MV-Klombero II,
Wakazi wa Mahenge, wakitelemka kwenye Kivuko cha Mv-Kilombero
Baadhi ya Wasafiri wakielekea Mahenge, kuvuka mto Kilombero
Baadhi ya Madereva wakisubiri kuvuka, katika foleni ambayo ilifikia idadi ya magari 62
Kutokana na hali ya kivuko cha MV-Kilombero kuwa mbaya inasababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo wanaotumia usafiri huo, ususani wenye vyombo vya usafiri kama baiskeli, pikipiki, na magari
Wafanyakazi wa Kivuko cha Mv-Kilombero wakiendelea na usafi wakati wa matengenezo ya kivuko cha MV- KILOMBERO II
Hali ya kivuko cha MV-Kilombero I, si shwari
pamoja na hali hiyo wakazi wa Mahenge na Kilombero hawakuwa na jinsi iliwabidi kuendelea kukitumia, ni hatari lakini salama
Injini ambayo ilikuwa tatizo baada ya kuharibika, ikiwa tayari kwa ajili ya kuirejesha Dar es Salaam kwa matengenezo
WAUDUMU wa MV-Kilombero I, wakiendelea kunyonya maji ambayo yanazidi wakati ikiendelea na safari zake
Dereva wa vivuko vya MV-KILOMBERO I na II akiwa hoi bin taabani, hapa akijipumzisha baada ya uchovu wa kila dakika
hali ambayo ilisababisha msongamano wa Abiria kama hivi,
Dr. Naibu katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(kushoto) Eng- Amosi na Msaidizi wa Eng Temea Rajabu Ngome(kulia) wakiendelea kusimamia zoezi la kutengeneza kivuko cha Mv-Kilombero II.
Askari wa kivuko akiendelea na ukaguzi wa tiketi katika kivuko cha KILOMBERO
Mashine ambayo ilipelekwa kutoka Songea, ikitelemshwa kwa ajili ya kufunga kwenye kivuko cha Mv-Kilombero II
Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(kushoto) akiendelea kusimamia zoezi la utengenezwaji wa kivuko cha Mv- Kilombero.
Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(kushoto) akifurahi baada ya kukamilisha zoezi la matengenezo ya Kivuko cha MV-kilombero II, hapa kivuko kikitoka kufanya safari ya majaribio mbele ya Naibu katibu Mkuu John Ndunguru
Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru, akitoa ufafanuzi wa kina kwa waandishi wa habari kuhusiana na kuharibika kwa kivuko cha Mv- Kilombero II, kulia ni eng msaidizi Temesa-Ngome Rajabu
Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(wa pili kushoto) akiagana na wakuu wa Temesa, baada ya kukamilisha zoezi la kutengeneza kivuko hicho(Picha Zote na Shaaban Mpalule)
No comments:
Post a Comment