N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Wednesday, February 26, 2014

HALI YA USALAMA YAZIDI KUZOROTA JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

GIGI_3b22b.jpg

Waasi wa kundi la kikristo la Anti Balaka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wametishia kuwaua mamia ya waislamu wanaojificha katika kanisa moja kama hawataondoka nchini humo katika kipindi cha wiki moja ijayo.
Wanajeshi wa kulinda amani wapatao 30 kutoka Cameroon walilazimika hapo jana kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya wapiganaji wa Anti Balaka waliokuwa wamekusanyika nje ya kanisa hilo la Kikatoliki wakipania kuwaua waislamu hao ambao wamekimbilia katika kanisa hilo kuokoa roho zao.
Milio hiyo ya risasi iliwaogofya watoto waliokimbia kujinusuru na vilio vya watu hao waliojawa na uoga vilisikika vikirindima katika kanisa hilo.Wanajeshi hao wa kulinda amani kwa sasa ndiyo tegemeo la pekee kwa waislamu hao wapatao 800 dhidi ya kushambuliwa na magenge yanayotaka kuwaua.
Wapiganaji wa Anti Balaka tayari walionekana wakiwa na mitungi ya lita 40 ya petroli ambayo wametishia kutumia kulichoma kanisa hilo.Kasisi wa kanisa hilo Justin Nary ambaye anatoa hifadhi kwa waislamu hao anajua analengwa na waasi hao.
Waasi walizingira kanisa kuwasaka waislamu
Kasisi Nary amesema wapiganaji hao wa Anti Balaka wamemtishia maisha mara nne kwa kumulekezea mtutu wa bunduki na wamempigia simu kumuonya kuwa punde tu wanajeshi wa kulinda amani wataondoka,watamuua.
Baadhi ya wanaotafuta hifadhi katika kijiji hicho cha Guen wametoroka baada ya kiasi ya waislamu 70 kuuawa katika siku za hivi karibuni.Waislamu na wakristo walikuwa wakiishi kwa amani tangu jadi hadi kundi la waasi la kiislamu kutoka Kaskazini mwa nchi hiyo lilipoipindua serikali na kulitumbukiza taifa hilo katika ghasia.
Kundi hilo la kiislamu la Seleka linashutumiwa kwa mauaji katika vijiji vya wakristo katika taifa hilo.Viongozi waliosaidiwa na Seleka kuingia madarakani walipoondolewa madarakani mwezi Januari,ilichochea mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa kundi lililoibuka la Anti Balaka.
Mauaji yaripotiwa katika miji mingine
Mji mkuuu Bangui ambao ulikuwa ni kitovu cha maasi na ghasia tangu mwezi Desemba kwa sasa hali inaonekana kudhibitiwa kwa kiasi fulani lakini mauaji yanayofanywa kwa misingi ya kidini yanaendelea kuripotiwa katika miji mingine nchini humo.
Majeshi ya Ufaransa na ya umoja wa Afrika yaliyoko nchini humo kudhibiti hali hayatoshi kukidhia mahitaji ya kiusalama na kiulinzi yanayohitajika kwa dharura.
Umoja wa Mataifa umeiomba Jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kabambe na za dharura kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati kujikwamua kutoka kwa mzozo mbaya unaotishia kulisambaratisha taifa hilo.
Bunge la Ufaransa hii leo linatarajiwa kupiga kura kuidhinisha kuendelea kusalia kwa jeshi lake nchini humo hadi mwezi Februari mwaka ujao wakati ambapo Jamhuri ya Afrika ya Kati itafanya chaguzi.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian amekiri kuwa itachukua muda mrefu kuliko walivyotarajia kurejesha udhabiti nchini humo kutokana na kiwango cha juu cha uhasama na ghasia.Maelfu ya watu wameuawa tangu Desemba na zaidi ya watu milioni moja wameachwa bila makaazi.
Chanzo, dw.de.com/swahili.

MAREKANI YACHUKIZWA NA RAISI MUSEVENI KUSAINI MUSWADA WA SHERIA KALI JUU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA

John Kerry asema Uganda inakiuka haki za binaadamu
Marekani haikufurahishwa na hatua ya Uganda kuidhinisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry amesema tangu Uganda iidhinishe mswada huo miaka minne iliyopita, Marekani ilieleza wazi kwamba sheria hiyo inakiuka jukumu la kuhakikisha kuwepo haki za binaadamu ambalo tume ya haki za binaadamu Uganda inatambua linaambatana na sheria ya Uganda.
Kerry amesema,' Baada ya kuidhinishwa sheria hii, tunaanza ukaguzi wa ndani wa uhusiano wetu na serikali ya Uganda, kuhakikisha kwamba pande zote za uhusiano wetu, ukiwemo miradi ya msaada, zinapinga sera na sheria zinazowaonea watu na tuwe na uhusiano unaodhihirisha maadili yetu'.
Tamko hilo limetolewa siku moja baada ya rais Yoweri Museveni kukaidi shinikizo la kimataifa na kutia saini sheria hiyo iliyo zusha mzozo, inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja Uganda, hatua iliyozusha hisia kali.
Baadhi ya mataifa ya magharibi tayari yanatishia kukatiza msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Uganda.
Marekani inasema kuidhinishwa kwa sheria hiyo kunatishia hatari ya kurudi nyuma katika uwajibikaji wa Uganda kulinda haki za raia wake na kutishia jamii ya wapenzi wa jinsia moja Uganda.Chanzo BBC Swahili

Wednesday, February 19, 2014

CCM KARATU YAWAFARIJI WAGONJWA

index
Na: Gladness Mushi, Arusha
CHAMA  Cha Mapinduzi Wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha kimefanikiwa kutoa msaada kwa wagonjwa zaidi ya 100  wa hospitali teule ya wilaya ya Karatu(DDH KARATU)huku lengo likiwa ni kuwafariji na kuanza kutangaza mkakati mpya ambao utawasaidia wagonjwa kila mara.
Akiongea na waandishi wa habari wilayani humo mara baada ya kukabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa Wilaya hiyo Bw.Mustapha Mbwambo alisema kuwa misaada hiyo imetolewa kama njia mojawapo ya kutimiza upendo
Mustapha alisema kuwa kwa sasa wameweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa inawasadia wagonjwa na hata wale ambao hawajiwezi kwa misaada mbalimbali ambayo itaweza kuwasaida na kuona kuwa bado serikali na uongozi wa wilaya unawakumbuka.
‘ilani ya chama chetu inasema kuwa tuwapenda na tuwajengee mazingira ya kupona wagonjwa sasa sisi hapa Karatu tumeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa kila mara tunatoa msaada lakini pia kuwafariji wagonjwa ambao hawana uwezo na zoezi hili halitakuwa kwenye maazimisho haya ya miaka 37 pekee”aliongeza Mustapha.
 Katika hatua nyingine Katibu wa chama hicho ambaye ni Bi Elly Minja alisema kuwa kwa sasa Chama hicho kimeanza kutekeleza ilani ya Chama hicho lakini pia kuanzisha utaratibu maalumu wa kuweza kuwasaidia wananchi kwenye masuala ya msingi ambayo wakati mwingine yanachangia sana umaskini .
 Alifafanua kuwa kwa mikakati ambayo inalenga kwenye masuala ya msingi yatachangia kwa kiwango kikubwa sana historia ya mji huo wa Karatu ambao kwa sasa bado unahitaji nguvu kubwa sana ya chama hicho.
“leo tumeweza kufanya mambo mbalimbali ya kichama lakini pia tumeweka malengo ya kuhamkikisha kuwa hata ilani ya chama inatekelezwa kwani kama ikifanikiwa basi itaweza kuwasaidia sana wananchi wa hapa kwetu na hivyo hata kwa mkoa wa arusha nako historia ikiwemo ya umaskini itabadilika sana”aliongeza Bi Minja.
 Wakati huo huo akiongea na wananchi wa wilaya hiyo  kwenye viwanja vya Mazingira Bora Mgeni Rasmi kwenye maazimisho hayo, Daniel Awaki ambaye ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama hicho kwenye Wilaya hiyo ya Karatu alisema kuwa toka kuanzishwa kwa chama hicho miaka 37 iliyopitwa kuna mabadiliko makubwa sana na mabadiliko hayo hayapaswi kupuuzwa wala kuzomewa na mtu yeyoete.

“tujiulieze kwa sasa ukitoka Arusha mpaka hapa unatumia muda gani na hapo awali ilikuwaje, na wala sio kwenye sekta hiyo pekee bali hata kwenye sekta nyingine za msingi sasa mafanikio kama haya hatupaswi kuyapuuza hata kidogo”aliongeza Awaki.

MAONYESHO YA KAZI ZA VIJANA WAJASIRIAMALI DODODMA WADAU WAOMBWA KUDHAMINI

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Aj It Development  Bw Jackson Audiface akizungumzia  kuhusu Maonyesho ya Tatu ya Kazi za Vijana wajasiriamali Yatakayofanyika Mkoani Dododma Mwezi Aprili mwaka huu.Maonyesho hayo ya kazi za Vijana wajasiriamali Hususani Vijana wanaosoma Vyuo Vikuu vya Dodoma. Lengo la Manonyesho hayo ni Kuzitangaza Kazi za Vijana wajasiriamali Wa Tanzania.Pili kuwapa Muda wadau Mbalimbali Kukutana na Vijana Wajasiriamali Ili kutatua Kero zote zinazowakabili vijana Katika Shuguli zao za Ujasiriamalia .
 Baadhi ya Bidhaa Ambazo zinazozalishwa na Vijana wajasiriamali Waliohitimu Vyuo vikuu Mbalimbali hapa Nchini Na Ambao Bado wako Vyuoni kuendelea na Masomo yaoamabzo zitaonyeshwa katika Maonyesho hayo Yatakayofanyika Mkoani Dodoma Yakiwa Ni ya Tatu kuafanyika hapa Nchini kwa Lengo la Kukuza soko la Kazi za Vijana wajasirimali pia Kuzitangaza na Kuatatua Ngangamoto Mbalimbali Zinazowakabili Vijana wa Kitanzania Kama Vile Vibali vya Kufanya Biashara Kutoka Mamlaka Mbalimbali hapa Nchi.Wadau Mbalimbali wa Vijana Mnaombwa Kujitokeza Kudhamini Maonyesho hayo.
Bidhaa Mbalimbali za Kilimo Zinazozalishwa na Vijana wa Mkoani Dodoma Ambao watazionyesha kwa Wakazi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya Jirani.
Bw Jackson Audiface Akielezea Zaidi Kuhusu Maonyesho hayo Yatakayofanyika Mkoani Dodoma.Hapa Akiwa Ameshika Mafuta yanayozalishwa na Vijana wajasirimali wa Mkoani Dodoma jana Wakati wajasiriamali hao walipotembelea Ofisi za Kampuni ya Aj It Development Kwajili ya Kujisajili ili kushiriki Katika Maonyesho ya Kazi za Vijana wajasiriamali Yatakayofanyika Mkoani Dodoma
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Akikagua Moja ya Shuguli za Kikundi cha Vijana kijulikanacho Kama Mae Ambao watashiriki Katika Maonyesho hayo.
Kampuni ya AJ IT DEVELOPMENT  inatarajia kufanya Maonyesho ya Tatu ya Kazi za  vijana Wajasiriamali Yanayofahamika kama Tanzania Youth Enterprenuership Program (TAYEP) Yanayotarajiwa Kufanyika April 3 – 5 April, 2014 Mkoani Dodoma.
Kwa mujibu  Mkurugenzi wa Kampuni ya AAj It Development  Bw Jackson Audiface, Maonyesho hayo ya  aina yake kufanyika nchini Tanzania yenye lengo la Kuzitangaza Kazi za Vijana Wajasiriamali 
“Maonyesho haya Yalianzishwa Kwa Lengo la Kutatua changamoto zote zinazowakabili Vijana wajasiriamali Pindi wanapojishugulisha Katika Shuguli zao za Ujasiriamalia.
Aliongeza kuwa washiriki watapata Ya Kuzitangaza Kazi zao,Kujua Taratibu Mbalimbali na Namna Ya Kuingiza bidhaa zao Kwenye Masoko Mbalimbali kwa Wingi zaidi.Namna ya Kupata vibali Mbalimbali vya Kufanyia Biashara Kutoka Mamlaka Mbalimbali za serikali.Kupata elimu namna ya Kuziboresha Bidhaa zao ziendane na soko pia Kukidhi viwango na Matakwa ya Wateja.Kuwakutanisha na wadau Mbalimabali wa Vijana na Kujua taratibu  namna ya Kushirikiana na Wadau hao katika Kuboresha Bidhaa zao.
Akizungumza mfumo utakaotumika kuendesha Maonyesho hayo Bw Jackson Audiface Alisema Kila Mshiriki Atapata Fursa ya Kuonyesha Kazi yake na Kuilezea Kwa Kina pia na Changamoto Anazokabiliana nazo kazi kazi zao za Ujasiriamali.
Walengwa wakuu wa Maonyesho hayo ni Vijana Kutoka Mkoani Dododma Hususani Vijana Kutoka Vyuo Vilivyoko Mkoani Dodoma.        
Washiriki wa Maonyesho hayo wanatarajiwa kuwa 3,000 Ambapo Vijana 250 Wataonyesha Kazi zao Zikiwemo Bidhaa za Kilimo ,Teknolojia ya Habari,Sayansi ya Kompyuta,Utalii wa Ndani na Ufugaji.
“Tunaomba makampuni na mashirika  Ambao ni Wadau wakubwa wa Maendeleo ya vijana kutumia fursa hii Kufadhili Maonyesho Hayo ili waweze Kujione Fursa Mbalimbali Wanazofanya Vijana. Pili  kujitangaza, na kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao 
Mgeni rasmi wa Maonyesho Hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Mizengo Pinda.

ENDABASHI WAFURAHIA UANZISHWAJI WA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO

GEDSC DIGITAL CAMERA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akitoa elimu ya Ulinzi Shirikishi kwa viongozi na wananchi wa Tarafa ya Endabashi iliyopo wilayani Karatu. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)GEDSC DIGITAL CAMERADiwani wa kata ya Buger Bw. Emmanuel Tlaqho akitoa shukrani zake kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (SACP) Liberatus Sabas mara baada ya kueleza uanzishaji wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto katika eneo hilo. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)GEDSC DIGITAL CAMERAKamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya wananchi wa Tarafa ya Endabashi mara baada ya kumaliza kutoa elimu ya ulinzi shirikishi kwa wakazi hao. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
…………………………………………………………………………………………………………..
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wananchi wa Tarafa ya Endabashi iliyopo wilayani Karatu wamefurahishwa na utaratibu mpya wa jeshi la Polisi wa kupeleka askari 15 kila Tarafa kwa lengo la kuimarisha ulinzi katika maeneo yao. Akimshukuru Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, kwa niaba ya wananchi hao Diwani wa kata ya Buger Bw. Emmanuel Tlaqho, alisema kwamba mbali na mpango huo pia wamepokea kwa mikono miwili uanzishaji wa Dawati la Jinsia na Watoto.
Bw. Tlaqho alisema kwamba Dawati hilo litasadia katika mambo mengi ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro ya ndoa na utelekezwaji wa familia. Alisema pamoja na kuwepo kwa Dawati hilo pia viongozi wa mtaa wa maeneo hayo wanatakiwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuwaasa  wanandoa ili waishi kwa amani ndani ya familia zao pia kutotumikisha watoto pamoja na kutowanyanyasa.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akizungumza na viongozi na wananchi wa maeneo ya Tarafa hiyo ambayo ina jumla ya vijiji 16 na wakazi wapatao 68,339, alisema kwamba mpango huo wa kupeleka askari 15 kila Tarafa una nia ya kuliweka Jeshi la Polisi karibu na wananchi ili waweze kushirikiana katika utatuzi wa matatizo ya kiulinzi na kiusalama kabla hayajafika kwa Mkuu wa Polisi wa wilaya.
Kamanda Sabas aliongeza kwa kusema kwamba, mbali na askari hao kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo pia watakuwa wanatoa elimu ya Polisi Jamii kwa askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi ili wajue namna ya utendaji wa kazi za ulinzi ikiwa ni pamoja na ukamataji salama na pia kutoa elimu kwa wananchi kupitia mikutano mbalimbali ili waweze kujua haki zao na wajibu wao katika suala zima la ulinzi.
Kamanda Sabas aliwasisitizia wakazi wa Tarafa hiyo wawe wanatumia mbinu za Ulinzi Jirani katika nyumba zao. Alisema suala la ulinzi ni la kila mmoja na haliihitaji kusubiri kudra ya M/mungu kwani uwezo wa kuzuia uhalifu upo ndani yao.
Akimalizia kutoa elimu hiyo kwa wakazi hao, Kamanda Sabas aliwaambia katika suala la ulinzi itikadi za kisiasa na udini hazina nafasi kwani mhalifu anapovamia eneo lolote hamuulizi mtu kwamba ni wa Chama gani au Dini gani bali yeye anatekeleza kile alichokikusudia.
Kwa upande wake mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la John Bula alisema kwamba, inaonyesha dhahiri kwa sasa jeshi la Polisi limeamua kushirikiana na wananchi kwani katika maisha yake hayawahi kuongea na Kamanda wa Polisi wa Mkoa ana kwa ana mbali ya kumuona kwenye runinga au akiwa katika msafara wa Viongozi wa kitaifa lakini kupitia kikao hicho ameweza kuongea naye.
Bw. Bula alisema kutokana na hamasa iliyotolewa na Kamanda Sabas yeye kwa kushirikiana na wananchi wenzake watakuwa bega kwa bega na askari hao waliopo tarafani hapo ambao wanaongozwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Robert Majenga.
Mpaka hivi sasa katika Mkoa wa Arusha tayari Kamanda Sabas amekwisha toa elimu juu ya ulinzi shirikishi kwa wananchi  wa Tarafa mbalimbali za wilaya nne huku bado akisubiri kumalizia wilaya mbili ambazo ni Ngorongoro na Longido.

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AKABIDHIWA DVD YA VIDEO YA MATEMBEZI YA HIYARI DAR MPAKA MORO

SEMINA YA WASANII WA BONGO MOVIE KUFANYIKA IJUMAA 21 FEBUARI 2014 KATIKA UKUMBI WA VIJANA KINONDONI

KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI APOKEA MITAMBO YA KUZALISHA UMEME

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw.   Eliachim Maswi akishuka kutoka juu ya meli wakati wa Hafla ya kupokea mitambo miwili ya kuzalishia umeme thamani ya Dola za Kimarekani  milioni 183 kutoka kwenye Kampuni ya General Electronics ya Marekani  inayokwenda kufungwa Kinyerezi,hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.

IMG_3141Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw.   Eliachim Maswi (Kushoto) akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Felchesmi Mramba wakati wa Halfa ya kupokea mitambo miwili ya kuzalisha umeme yenye thamani ya Dola za Kimarekani  milioni 183 itakayokwenda kufungwa Kinyerezi ambapo mitambo hiyo itaanza kufanya kazi mwezi wa kumi mwaka huu.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo .IMG_3188Moja ya mitambo ya kuzalishia umeme ikipakiwa katika gari tayari kwa safari ya kwenda Kinyerezi kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi wa Tatu na kukamilika mwezi wa kumi mwaka huu, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana) ambapo mitambo hiyo imepokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi. (Picha zote na Benjamin Sawe wa Maelezo

TAARIFA YA CCM KUHUSU MAAMUZI YA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA

IMG_2949

Nape Moses Nnauye Katibuwa Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari leo mchana katika makao makuu ya CCM Lumumba  ofisi ndogo ya chama jijini Dar es salaam kuhusu maamuzi ya vikao vya chama vilivyomalizika mjinDaodoma hivi karibuni.
…………………………………………………………………………………..
Kati ya tarehe 13/02/2014  na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama.
Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2013.
Waliohojiwa katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:-
1.    Ndg. Frederick Sumaye
2.    Ndugu Edward Lowasa
3.    Ndugu Bernard Membe
4.    Ndugu Stephen Wassira
5.    Ndugu January Makamba
6.    Ndugu William Ngeleja
Baada ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo kupendekeza adhabu.  Mapendekezo hayo yalipelekwa kwenye Tume ya Udhibiti na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa adhabu kwa wahusika.
Kwa ujumla waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-
1.    Walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).
2.    Wamethibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii.  Kosa hili nalo ni kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo.
Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu ya ONYO KALI na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo Chama kitawachukulia hatua kali zaidi.
Tafsiri ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b) ni:-
“Mwanachama aliyepewa adhabu ya ONYO KALI atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha.”
Kamati Kuu imeitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine (mawakala na wapambe) kufanyika kwa vitendo hivyo vilivyovunja Kanuni za Chama.
Aidha, Kamati Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na kuwataka kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania Urais yanayovunja na kukiuka maadili ya Chama, wametakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu za Chama.
Imetolewa na:-
 
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI,
18/02/2014

UWT YAMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA

MHE. SOFIA SIMBA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO

Sophimba Mwenyekiti wa UWT Taifa
………………………………………………………………………………………………….
Na Anna Nkinda – Maelezo
Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT)  umempongeza Mhe. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba linalotarajia kuanza leo Mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Eva Mwingizi ilisema uteuzi wa Rais umezingatia umri, weledi, uzoefu na uwakilishi wa makundi mbalimbali yakijamii.
Mwingizi alisema uteuzi huo umeangalia asilimia 50 ya uwakilishi wa wajumbe 201 hii ikiwa ni wanawake 100 na wanaume 101 pia Bunge hilo linajumuisha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wajumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar.
Aidha katibu Mkuu huyo alilitakia heri Bunge hilo na kuwaomba wajumbe waliochaguliwa kutambua kuwa wamepewa dhamana kubwa ya kuzingatia maoni ya wananchi ya kutengeneza katiba ya Tanzania yenye kulinda, kutetea  na kusimamia maslahi ya Taifa kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

IGP MANGU KWENYE MKUTANO MKUU WA MAAFISA WAKUU WA JESHI LA POLISI

1(10)

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Jumbe Mangu akisisitiza jambo kwenye mkutano Mkuu wa Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika Chuo cha Taluma ya Polisi Moshi, mkoani Kilimanjaro. Mkutano huo umebebwa na kauli mbiu isemayo “Zingatia Weledi katika Kutoa Huduma Bora Kwa Jamii”. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA KAIMU KAMISHNA WA TRA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Kaimu Kamishna Jenerali wa TRA, Risherd Badei, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 18, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Kaimu Kamishna Jenerali wa TRA, Risherd Badei, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 18, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR

KAMPENI YA VIRUTUBISHI CHAKULA

Mwelimishaji  wa masuala ya lishe kutoka mradi wa USAID Tuboreshe Sara Luzangi, akiongea na wanafunzi wa shule za msingi wilayani Babati mkoani Manyara, juu ya umuhimu wa matumizi ya vyakula vilivyowekwa virutubishi katika kampeni za kutoa elimu hiyo zinazoendelea katika wilaya mbalimbali za hapa nchini

Blog Archive