MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA WANANCHI HUKU MWINGINE AKIJERUHIWA MKOANI MBEYA.
MNAMO TAREHE 17.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONI HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA MTU MMOJA ALIYEFAHAMI
KA KWA JINA LA SELEMAN KADUMU (25) MKAZI WA ILEMI ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU PAMOJA NA MWENZAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DEVID SAMSON (26) MKAZI WA ILEMI WALISHAMBULIWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI HUKU WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU NA MWENZAKE HUYO MNAMO TAREHE 15.02.2014 MAJIRA YA SAA 23:45HRS USIKU KUVUNJA DUKA MALI YA OMARY ABUU (20) MFANYABIASHARA NA MKAZI ILEMI NA KUIBA REDIO AINA YA SUB – WOOFER, SIMU YA MKONONI NA COMPUTER. MTUHUMIWA DEVID SAMSON ALIPATIWA MATIBABU NA KURUDISHWA MAHABUSU. WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
MTU MMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA
BHANGI.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA STEPHANO FESTO (25) MKAZI WA SOGEA ALIKAMATWA AKIWA NA BHANGI KETE TATU SAWA NA UZITO WA GRAM 15. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 17.02.2014 MAJIRA YA SAA 17:30HRS JIONI HUKO KATIKA MTAA WA SOGEA – TUNDUMA WILAYA YA MOMBA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment