N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Wednesday, February 19, 2014

UWT YAMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA

MHE. SOFIA SIMBA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO

Sophimba Mwenyekiti wa UWT Taifa
………………………………………………………………………………………………….
Na Anna Nkinda – Maelezo
Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT)  umempongeza Mhe. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba linalotarajia kuanza leo Mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Eva Mwingizi ilisema uteuzi wa Rais umezingatia umri, weledi, uzoefu na uwakilishi wa makundi mbalimbali yakijamii.
Mwingizi alisema uteuzi huo umeangalia asilimia 50 ya uwakilishi wa wajumbe 201 hii ikiwa ni wanawake 100 na wanaume 101 pia Bunge hilo linajumuisha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wajumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar.
Aidha katibu Mkuu huyo alilitakia heri Bunge hilo na kuwaomba wajumbe waliochaguliwa kutambua kuwa wamepewa dhamana kubwa ya kuzingatia maoni ya wananchi ya kutengeneza katiba ya Tanzania yenye kulinda, kutetea  na kusimamia maslahi ya Taifa kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

No comments:

Post a Comment

Blog Archive