Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Maalim Abdalla
Mzee (mwenye miwani) akibadilishana mawazo na watendaji wakuu wa Mpango
wa kubadilishana masomo kwa Vijana wa skuli za sekondari (Youth
Exchanging Study) kabla ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka unaofanyika
Hoteli ya Karafuu Michamvi Kusini Unguja.Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Maalim Abdalla
Mzee akifungua Mkutano Mkuu wa siku tatu wa YES huko Michamvi. Rais
wa Jumuiya ya wanafunzi wa Skuli za Sekondari Zanzibar waliosoma
Marekani mwaka mmoja kupitia Mpango huo (Zanzibar YES Alumni
Association) Jamila Ahmed Rashid akitoa maelezo ya jumuiya inavyofanya
kazi zake huko Michamvi.
Afisa wa masuala ya Zanzibar katika Ubalozi wa Marekani Jamal Jafari
akizungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mpango wa YES unaofanyika
Hoteli ya Karafuu Michamvi.Mkurugenzi
Mtendaji wa YES Del Christensen akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu Mkutano huo unaofanyika Michamvi Kusini Unguja.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment