Mkurugenzi
wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya
Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo (mwenye shati la batiki),
akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Wafanyabiashara
wa Madini ya Vito wa Thailand, walipotembelea Banda la Tanzania katika
Maonesho ya 54 ya Vito na Usonara ya Bangkok, yaliyofanyika Septemba 9
hadi 13 mwaka huu.
Makamu
wa kwanza wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na
Usonara wa Thailand, Bw. Sutipong Dumrongsakul, akimkabidhi zawadi
maalumu Mkuu wa Ujumbe kutoka Tanzania ulioshiriki maonesho ya vito ya
Bangkok, Archard Kalugendo, mara baada ya kikao kati ya Ujumbe huo na
Viongozi wa Taasisi hiyo ya Wafanyabiashara wa Thailand.
Wateja
mbalimbali wakihudumiwa katika Banda la Tanzania kwenye maonesho ya
vito na usonara ya Bangkok yaliyofanyika hivi karibuni nchini
Thailand.
No comments:
Post a Comment