Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa Bi. Khadija Hassan Aboud akimkaribisha Mbunge
ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha FRELIMO cha Msumbiji Bi. Nyeleti
Mondlane Ofisi kuu ya CCM Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha FRELIMO cha Msumbiji Bi. Nyeleti Mondlane
akisaini kitabu cha wageni alipofika Ofisi kuu ya CCM Zanzibar (kulia) Katibu
wa FRELIMO Zanzibar Bw. Agostino Andrea.
Kiongozi wa Ujumbe wa Chama cha FRELIMO Bi. Nyeleti Mondlane (watatu kushoto) akibadilishana
mawazo na wenyeji wake wajumbe wa Chama cha Mapinduzi katika Ofisi Kuu Kisiwandui
Zanzibar ikiwa ni mkakati wa kuimarisha Uhusiano wa Vyama vyao na kuzindua Kampeni
ya Uchaguzi Mkuu Nchini Msumbiji.
Picha ya pamoja ya Ujumbe wa Chama cha FRELIMO na baadhi ya wajumbe wa Chama
cha Mapinduzi CCM wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa Bi. Khadija
Hassan Aboud wakatikati.
========= ======== ========
Picha na
Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
CHAMA
cha FRELIMO kimesema Wananchi wa Msumbiji wataendelea kukumbuka na kuthamini
juhudi mbali mbali zilizochukuliwa na Watanzania wakati wa harakati za ukombozi
na kuwafanya kuwa watu huru.
Kauli
hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha FRELIMO Bibi Nyeleti Mondlane, alipokuwa na
mazungumzo maalum na Uongozi wa CCM Zanzibar, hapo Afisi Kuu ya CCM,
Kisiwandui.
Amesema
Wananchi wa Msumbiji wana kila sababu ya kuwapongeza Watanzania kutokana na
misaada yao ya hali na mali, jambo lililosaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa
Msumbiji kujikomboa na kuishi wakiwa watu huru ndani ya nchi yao huru.
Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu ya FRELIMO na pia ni Mbunge, amesema nchi hiyo imo katika
amani na utulivu mkubwa, hali inayotoa fursa kwa Serikali ya FRELIMO kuweza kufanikisha shughuli za kimaendeleo kwa
maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Ametumia
kikao hicho kutoa wito kwa Wana FRELIMO wanaoishi Zanzibar kuendeleza
mashirikiano ya karibu na wananchi wa Tanzania, CCM na Serikali zake, ili umoja
na maendeleo kwa wananchi wa pande zote mbili.
Naye
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM Mhe. Khadija Hassan Aboud, amemuhakikishia
Bibi Mondlane kuwa Chama Cha
Mapinduzi kitafanya kila linalowezekana kuhakikisha uhusiano wa kihistoria
baina ya CCM na FRELIKO unaendelezwa kwa nguvu zote.
Amesema
Vyama vya CCM mrithi wa ASP na FRELIMO, vina undugu wa kihistoria uliodumu kwa
miaka mingi na kumesisitiza haja kwa Viongozi wa Vyama hivyo wanapaswa kuuendeleza
na kuudumisha kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo.
Bibi
Mondlane yupo Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya kichama, ambapo katika
mazungumzo hayo aliongoza Ujumbe wa watu watano, akiwemo Balozi Mdogo wa
Msumbiji nchini Zanzibar Bwana Jorge Augusto Menezes.
No comments:
Post a Comment