N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Thursday, March 19, 2015

ZINDUKA Vocational Training Center Students:




3
To respond to this community need, in 2011 Project Zawadi’s local partner organization, Zinduka Development Forum, opened the fully modern Zinduka Vocational Training Center (VTC) with significant financial support from Project Zawadi. This facility, in the final stages of receiving certification from the Tanzanian Government’s Vocational and Educational, is the community’s first high-quality vocational training center for local students. Currently providing course options in the areas of carpentry and needlework, the VTC will add welding to this list in 2013. It also houses the first ever computer lab and provides introductory computer skills training to students and local residents. It is a fully modern facility with a theory classroom, carpentry workshop, sewing room, library space, computer lab, secure materials storage area, teacher office, and staff and student toilets. It is supplied with electricity and running water and has the advantage of allowing students to remain in their local community while furthering their education. Zinduka Vocational Training Center - dormitory will be built three blocks away providing easy access for the students.




 Also the program established the tree planting in Nyamuswa area.
This program needed to be expanded to more villages if funds will be presently available

Wednesday, March 18, 2015

Serikali yajidhatiti Kudhibiti Makosa ya Utakatishaji fedha haramu Nchini- AG Masaju

Ndugu Masaju pia ameeleza kuwa wahalifu wanatumia fursa iliyoletwa na maendeleo ya mifumo ya Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA) katika biashara mbalimbali kutakatisha fedha zinazopatikana kwa njia ya uhalifu na kuzisafirisha haraka katika nchi nyingine ili kuficha uhalisia wa mali hizo kwa dhamira ya kuepuka kukamatwa na vyombo vya uchunguzi hapa nchini ambapo ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo kutumia vizuri fursa waliyoipata kujifunza na kupata majibu ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utendaji kazi ili kuongeza kuongeza ufanisi na kuhakikisha wahalifu hawafaidiki na uhalifu wanaoufanya. Awali, akimkaribisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw.Ayub Mwenda ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshugulikia Usimamizi na uratibu wa uendeshaji wa Mashtaka ya Jinai kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali alieleza kuwa Serikali inatoa uzito mkubwa katika suala la kukabiliana na uhalifu na mashauri yanayohusu masuala ya utakatishaji fedha hivyo nguvu na uelewa wa pamoja vinahitajika kutoka kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na kuendelea kushirikiana ili kujiimarisha zaidi katika eneo hilo.

Wednesday, March 11, 2015

Serikali kuendelea kuandaa mazingira bora ya wavuvi Zanzibar



Mkutano wa 19 baraza la wawakilishi kuanza jumatano


za3Katibu Mkuu Baraza la Wawakilishi Zanzibar Nd. Yahya Khamis Hamad akijibu maswali yaliyoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo. (Picha na Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar).
Na Rahma Khamis na Mwanaisha Moh’d Maelezo-Zanzibar. Mkutano wa Kumi na Tisa (19) wa Baraza la Nane (8) la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano Tarehe 11 March, 2015 saa 3:00 kamili za asubuhi ambapo miswada minne ya sheria itawasilishwa na kujadiliwa barazani hapo. Hayo yameelezwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Nd. Yahya Khamis Hamad alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Baraza hilo huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Amesema miswada itakayojadiliwa ni pamoja na Mswada wa Sheria ya kufuata Sheria ya Miradi ya Maridhiano Namba 1 ya mwaka 1999, Kutunga Sheria kwa ajili ya kuazishwa na kuendesha mashirikiano baina ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi zilizopo nchini ikiwemo na Kuwasilishwa mbele ya Baraza, Sheria ya Kura ya Maoni No. 11 ya Mwaka 2013 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa kifungu 132(2) cha Katiba ya Zanzibar. Vile vile Katibu huyo ametanahabahisha kuwa mswada mwengine utakaojadiliwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Baraza la Sensa ya Filamu na Utamduni Zanzibar ambalo litasaidia kukuza na kulinda utamaduni wa Wazanzibari. Sambamba na hayo amesema katika shughuli zitakazoendelea katika Baraza hilo ni pamoja na maswali na majibu ambayo yataulizwa na kujibiwa na wajumbe wa baraza hilo ambapo maswali 77 yanatarajiwa kujibiwa katika baraza hilo. Katibu Yahya amewaomba Wajumbe wa Baraza hilo kufika kwa wakati barazani hapo ili kwenda sambamba na muda kwa lengo la kutimiza majukumu yaliokusudiwa katika mkutano huo.

Balozi wa China akutana na Rais Dk.Shein

MAHAKAMA KUU YAFUTILIA MBALI KESI ILIYOFUNGULIWA NA ZITTO KABWE

MAMA MARIA NYERERE AKANUSHA UVUMI ULIOENEA JANA KUWA AMEFARIKI DUNIA

unnamed (69)
Kwa hisani ya
Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere leo amezungumza na waandishi wa habari,nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam juu ya uvumi ulioenea nchini kuwa amefariki Dunia.
Mama Maria amewathibitishia watanzania kuwa bado yu hai na mwenye nguvu hivyo wasiwe na hofu nae.
Alisema jana amepokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto zake, wake wa watoto zake wote, familia yake pamoja na watu mbalimbali ili kumjulia hali.
Amesema alipopokea taarifa hizo wala hakushtushwa badala yake alifanya sara kwani uvumi huo wawezekana inatokana na vuguvugu la uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, pia utandawazi uliopo wa sayansi na teknolojia wa karne ya 21.
“jana nilipokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto wangu, wake wa watoto zangu, pamoja na familia,walikuwa wakinisalimia, wengine waliposikia sauti yangu walikata simu” alisema Mama Maria.
Mama Maria alisema taarifa hizi za kuzushiwa kifo si mara ya kwanza kwani hata miaka ya nyuma akiwa na hayati baba wa Taifa, mwalimu Julius Nyerere walipokea taarifa nyingi za uvumi wa kifo.
Mjane wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam leo,juu ya uvumi wa kufariki Dunia ulioenea jana kupitia simu na mitandao ya kijamii.