N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA
FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC
Wednesday, March 9, 2016
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMLAKI RAIS WA VIETNAM MHE. TRUONG TANG SANG IKULU
Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang wakati walipokuwa wanazungumza Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Mazungumzo Rasmi kati ya ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuzungumza na wanahabari hawapo pichani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari hawapo pichani kuhusu mazungumzo yao na Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
RAIS DKT. MAGUFULI AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI MAALIMU SEIF SHARIF HAMAD.
Wednesday, March 09, 2016
Maoni: 0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif aliruhusiwa kutoka hospitalini jana na hali yake inaendelea vizuri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumjulia hali na kusema kuwa hali yake ya kiafya inaimarika siku baada ya siku.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS TUONG WA VIETNAM LEO
Wednesday, March 09, 2016
Maoni: 0
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga.
Rais Truong wa Vietnam akimsifia jambo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akati akimuaga baada ya mazungumzo yake na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kulia)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga na kulia ni Dk. Asha-Rose Migiro.
Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo hayo.
Read more »
NMB MDHAMINI MKUU WA MKUTANO MKUU WA ALAT TAIFA.
Wednesday, March 09, 2016
Maoni: 0
NMB Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT taifa.
Benki ya NMB imekabidhi hundi ya mfano ya shilingi Milioni 100 kwa uongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kwaajili ya udhamini wa mkutano mkuu wa ALAT taifa unaotarajia kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa Aprili Mjini Dodoma.
Fedha hizo ni kwaajili ya kugharamia gharama za mkutano mkuu unaotarajia kukutanisha wajumbe zaidi ya 400 kati yao wakiwa mameya 180 kutoka halmashauri zote nchini, wakurugenzi wa halmashauri wapatao 180, wawakilishi wa mikoa na wizara mbalimbali ambao jumla yao wanafika zaidi ya 400.
NMB imekuwa ikidhamini mikutano ya ALAT kila mwaka na kwa mwaka huu, malengo makubwa ni kuhakikisha halmashauri zote zinaingia kwenye mfumo wa malipo ya kielektroniki ili kuzuia upotevu wa mapato. NMB kama mpokeaji mkuu wa malipo kwa njia za kielektroniki kwenye halmashauri, tayari imeshafanya majaribio ya kupokea malipo kwa njia hizo na hivi karibuni itaanza kutoa huduma hiyo kwenye halmashauri zote nchini.
Kupitia mtandao wake wa matawi 180 nchini, NMB imekuwa karibu na wananchi wa halmashauri mbalimbali kwa kutoa huduma za kifedha na pia kusaidia serikali katika uboreshaji wa njia za ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki.
Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi milioni 100 kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Habraham Shamumoyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mawasiliano-ALAT, Seif Hassan. NMB imedhamini mkutano mkuu wa ALAT unaotarajia kufanyika mapema mwezi April mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Habraham Shamumoyo akiongea na waandishi wa habari (hawako kwenye picha) kuhusu Mkutano Mkuu wa Tawala za Mitaa utakaofanyika jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB - Richard Makungwa.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment