N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Friday, March 11, 2016

REGISTER FOR DICOTA CONVENTION BY 03/10/16 TO WIN A FREE ROUND TRIP AIR TICKET TO DALLAS - LESS 24 HOURS REMAINING



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt. Natu Mwamba akiwasili makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza leo Machi 10, 2016 .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua CV za wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania alizoendazo wakati wa ziara yake ya kushtukiza jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Gavana wa Benki Kuu Beno Ndulu March 10, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na uongozi wa juu wa Benki Kuu ya Tanzania ambao ameupa maelekezo mbalimbali katika kuboresha utendaji wao wa kazi wakila siku
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana kutoka nje Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016.Picha na Ikulu






“Suala la kushusha sukari hadi kufikia Sh1,800 kwa bei elekezi halitawezekana kwa kuwa bei ya jumla ya kilo moja tunauziwa Sh2,000 hivyo tunalazimika kuuza Sh2,200 ili kilo moja tupate faida ya Sh200,” alisema Brayton. Mfanyabiashara mwingine wa duka la jumla Magomeni, Idrisa Abraham aliyekuwa akiuza mfuko wa sukari wa kilo 50 kwa Sh98,000 na wa kilo 25 kwa Sh48,000, alisema kabla ya kutoa bei elekezi, Serikali ilitakiwa kufanya utafiti ili kubaini sababu ya kutoonekana kwa bidhaa hiyo na kukutana na wafanyabiashara wanaosambaza na wa maduka ya jumla ili kujua kwa nini sukari ya Tanzania haionekani na kinachoifanya kupanda “...nina imani wangebaini kitu, kinachonishangaza sukari iliyokuwa inatoka Malawi na Brazil ilikuwa inauzwa kwa bei nafuu sana na ilikuwa inalipiwa kodi kwa nini ya Tanzania iwe bei juu?”





Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Maafa Zanzibar ndugu Ali Juma Hamad akifungua mafunzo ya waandishi wa habari juu ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu katika Ukumbi wa gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar, (kulia) daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt Fadhili Mohd na (kushoto) Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhili Mohd alipokuwa akielezea njia za kukabiliana na kipindupindu katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji Mkame akiwasilisha mada ya wajibu wa waandishi wa habari katika kukabiliana na maradhi ya miripuko katika mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar.
Katibu wa Jumuiya ya Maafisa wa Afya Zanzibar Ahmed Suleiman Said akitoa elimu ya kupambana na maradhi ya kipindupindu kwa wananchi wa shehia ya Shaurimoyo Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wa shehia ya Shaurimoyo Mjini Zanzibar wakifuatilia juu ya elimu ya ugonjwa wa Kipindupindu iliyotolewa na Jumuiya ya Maafisa wa Afya Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Wakati Rais John Magufuli akipambana na wakwepa kodi ili kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa, takwimu za zinaonyesha uwapo wa wafanyabiashara wanaopitisha bidhaa za magendo kwa njia ya panya kati ya mianya 509, Zanzibar inaongoza kwa kuwa na mianya 422, huku Tanzania Bara ikiwa na mianya 87.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mwenendo wa ukusanyaji wa mapato, matumizi ya mashine za kielektroniki katika ukusanyaji kodi (EFD), kusitishwa kwa bei elekezi na usajili wa vyombo vya moto, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, alisema bidhaa hizo hupitishwa Bandari ya Tanga na Mtwara zikitokea Zanzibar.

Alisema hali hiyo isipodhibitiwa haraka inaweza kusababisha madhara kwa sababu licha ya Bandari ya Dar es Salaam kuchangia mapato kwa kudhibiti wafanyabaishara wanaokwepa kodi katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Magufuli, bado kuna haja ya kuandaliwa mazingira rafiki yatakayowabana wakwepa kodi wanaotumia njia hizo za panya.

Alisema licha ya Bandari ya Dar es Salaam na mashine za EFDs, kuchangia kuongezeka kwa mapato, pia mamlaka hiyo imeboresha mfumo wa udhibiti wa ukwepaji kodi kwa wafanyabaishara hasa katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Magufuli.


“Mianya ya panya ni mingi na inabidi idhibitiwe haraka, tukiangalia mara moja, Zanzibar kuna mianya 422 inayopitisha bidhaa za magendo, wakati Tanzania Bara ni 87, tusiridhike na kiwango hicho kidogo ila iwekezwe nguvu kubwa kumaliza tatizo hilo,” alisema Kidata.

Akitoa mchanganuo wa makusanyo ya kodi ya ndani, alisema kwa Februari mamlaka hiyo imekusanya Sh. trilioni 1.040 kwa Tanzania Bara na Visiwani sawa na asilimia 101.18 ya lengo la serikali kufikisha Sh. trilioni 1.028.
Alisema kwa Januari, TRA ilikusanya kiasi cha Sh. trilioni 1.079 kwa Tanzania Bara na Visiwani sawa na asilimia 102 ya lengo la serikali kufikisha Sh.trillioni 1.059.

Alifafanua kuwa kwa kipindi cha Julai mwaka jana hadi Februari mwaka huu mapato yamefika Sh. trilioni 8.569 sawa na asilimia 99 ya makusanyo yote ya ndani.

Kwa mujibu wa Kidata, makusanyo hayo yametokana na ari na udhubutu ambao mamlaka hiyo imeweka katika kusimamia na kuhakikisha inaendelea kuziba mianya ya ukwepaji kodi ma kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara kwa kutumia mifumo mbalimbali.

Naye Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Yusuph Salum, alielezea mikakati ya mamlaka hiyo kwa Machi hadi Juni mwaka huu, kuwa wataendelea kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi, kufichua wakwepa kodi, kupambana na rushwa, pamoja na kupanua wigo wa kodi kwa kusajili wafanyabishara ambao hawajasajiliwa kama washereheshaji na wanataaluma.

Kadhalika, alisema TRA itasimamia kwa karibu matumizi ya mashine za EFDs na utoaji wa risiti na itafuatilia na kudai malimbikizo ya kodi kutoka kwa wadaiwa sugu pamoja na kuendeleza ukaguzi wa kodi kwa wafanyabaishara.

“TRA iko katika mchakato wa mwisho wa kubadilisha mfumo wa kusimamia mapato ya ndani, hivyo kupitia bajeti ya serikali ya 2017/17, kutakuwapo na utaratibu mpya utakaochangia ukuaji wa mapato,”alisema Salum.

Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya Forodha, Akonary Kaima, aliongeza kuwa matumizi ya bei elekezi katika mchakato wa uthaminishaji wa bidhaa bandarini ni kinyume cha sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo TRA itaendelea na shughuli za kiforodha kulingana na sheria bila kuathiri eneo jingine.

“Kwa sababu TRA, itadhibiti ukaguzi na uthaminishaji halisi, kila mfanyabaishara anatakiwa kulipa ushuru na kodi kulingana na thamani ya bidhaa husika,”alisema.

Alifafanua kuwa, kuna magari yaliyoingia nchini na kusajiliwa bila kufuata taratibu za forodha na kusababisha yamilikiwe kinyume cha taratibu, hivyo wamiliki wajisalimishe TRA, kufanyiwa uhakiki ikiwa ni pamoja na kuyalipia kodi.

NIPASHE
Katika kile kinachoonekana kuendelea kusumbuliwa na kivuli cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, vikao vya CCM vya kutahmini sababu zilizofanya wapoteze baadhi ya majimbo, vimeingia dosari mkoani Mara kwa makada wa chama hicho kunusurika kupigana wakituhumiana kuisaidia upinzani wakati wa uchaguzi mkuu.
Lowassa alijiondoa CCM Julai 28, mwaka jana, na kujiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Agosti 4, mwaka huo, mwanasiasa huyo mkongwe aliteuliwa kuwania urais akiungwa mkono na vyama vinne vilivyounda Umoja wa katiba ya Wananchi (Ukawa) na kuwa mshindi wa pili huku upinzani ukiwa na wabunge takribani 110 na zaidi ya halmashauri 25, idadi ambayo haijawi kufikiwa na vyama vyama vya upinzani tangu nchi ipate uhuru.

Taarifa ambazo gazeti hili ilizipata jana, zilisema makada wa chama hicho mkoani Mara, nusura wapigane wakiwa kwenye kikao kilichokuwa kinalenga kuangalia sababu ya kupoteza majimbo ya Bunda, Tarime Vijijini, Tarime Mjini na Serengeti.


Katika kikao hicho kilichofanyika Bunda, habari zinasema, vurugu zilianza baada ya baadhi ya viongozi kutaka kumtoa nje ya kikao Katibu Mwenezi wa CCM wa Wilaya, Ezekiel Sariro, kutokana na kurekodi kilichokuwa kinachoendelea kwenye kikao ili apeleke kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Stephen Wasira.

Sariro aliiambia Nipashe kuwa baada ya kutakiwa kuzima simu yake, awali aligoma kwa madai kuwa yeye hata kurekodi hawezi.

Alisema baada ya mvutano, viongozi wa mkoa waliokuwa wakiendesha kikao hicho, walimvuta na kutaka kumnyang’anya simu yake, ndipo alipokubali kuizima.

Sariro alisema Katibu wa Mkoa, Adam Ngalawa; Mwenyekiti wake, Christopher Sanya na Mwenyekiti wa Wilaya ya Bunda, Mwita Chacha, walifanya kitendo hicho kwa sababu walijua anataka kufichua walivyosaidia Ukawa kwenye uchaguzi mkuu.

Hata hivyo, walikana kumuunga mkono Lowassa na Ukawa kwa ujumla kwenye uchaguzi huo na badala yake wanaamini kinachoendelea sasa ni propaganda zenye mwelekeo wa kuwapaka tope.

Ngalawa kwa upande wake alisema ushiriki wake na Mwenyekiti Sanya, ulilenga kuzuia vurugu ambazo zingetokea kutokana na kutoelewana kwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Bunda na Katibu Mwenezi wake.

Naye Chacha anayetajwa kuwa mshirika wa viongozi hao wa mkoa, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu jana kuwa ‘washirika’ hao ndio walioitisha kikao hicho ili kuandaa taarifa itakayowasilishwa Makao Makuu ya CCM.

Chacha na Ngalawa kwa nyakati tofauti walisema kushindwa kwa CCM katika jimbo la Bunda kulitokana na kasoro za aliyekuwa mgombea ubunge wao, Stephen Wasira.

Wakati Chacha akisema Wasira alishindwa kutekelezwa ahadi kwa vipindi vya awali vya ubunge wake, Ngalawa alisema pamoja na mambo mengine, mwanasiasa huyo mkongwe hakuushirikisha uongozi wa wilaya, badala yake aliteua watu wachache hivyo kukosa fursa ya kupata mbinu za ushindi.

Viongozi hao walizielekeza shutuma zao kwa Sariro kwamba alikuwa mpambe wa karibu wa Wasira, hivyo kusababisha asikutane na viongozi na wanachama wengine.

Naye Sanya alisema kushindwa kwa CCM kwenye majimbo hayo, likiwamo Bunda, kulitokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kwa kamati za ushindi za wilaya ambazo hata hivyo hazikuwa na ushirikiano.

Pia alisema baadhi ya wagombea wa CCM waliunda kamati zao binafsi zilizokuwa nje ya mfumo wa chama, hivyo kusababisha kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo, Wasira alikanusha madai hayo na kusema kabla na wakati wa kampeni, alishirikiana na sekretarieti ya CCM wilayani Bunda isipokuwa Mwenyekiti wake, Chacha anayemtaja kuwa miongoni mwa waliokisaliti chama hicho.

Licha ya Chacha kukanusha madai hayo, Wasira alisema kwa kushirikiana na wajumbe wa sekretarieti hiyo (isipokuwa Mwenyekiti), waliwafikia viongozi katika ngazi za mashina, matawi, kata na jimbo.

“Huyo jamaa (Chacha) na viongozi wa mkoa ajenda yao ilikuwa moja tu, kuhakikisha kwamba wanasaidia CCM ishindwe, hakuna jambo jingine,” alisema Wasira wakati akijibu madai dhidi yake.

Akizungumzia kushindwa kwa CCM kwenye majimbo ya Tarime Mjini, Tarime Vijijini na Serengeti, Ngalawa alisema kulitokana na ukabila. Hata hivyo, uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa wagombea wote wa maeneo hayo walikuwa kutoka kabila la Wakurya.

Nape ageuka mbogu
Gazeti hili lilipomtafuta Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, ili kujua kwamba kufanya tathimini kujua sababu za kupoteza baadhi ya majimbo ni jambo linalofanyika nchi nzima na jinsi utaratibu wake ulivyo, alitaka mwandishi aandike maswali kwenye simu ili amjibu kwa maelezo kwamba yupo kwenye kikao.

Baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwenye simu yake ya kiganjwani, hakujibu na ndipo baada ya muda alipopigiwa tena alisema: “sijakiri wala sijakataa kama tumeagiza, nasema kaulizeni kwenye ngazi husika.

“Shida moja na hili lipo Nipashe na (gazeti lingine la kila siku analitaja jina) na mimi samahani kwa kukwambia hili, kama vile ni ajenda za kutokea wakati wa uchaguzi ambazo nyinyi mmezibeba sana, hili suala wewe mwenyewe umekiri limetokea katika wilaya na mkoa kwa nini msiwaulize wao wajibu.

“Mimi ni msemaji wa taifa, kama kuna shida ya utekelezaji ulizeni ngazi iliyofikia. Mimi sijaingia kwenye hivyo vikao, ninachojua si kila mahali vikao vimefanyika, ninyi mnataka kuwasaidia Ukawa kuwa na ajenda ya kuwasema CCM.

“Sasa hivi nipo Lindi, nikizungumza ni kama vile ni jambo limetokea nchi zima wakati si kweli na nimewajibu jana (anataja jina la gazeti jingine) wakaacha kuandika. Nilijua limetoka (anarudia kutaja jina la gazeti hilo) litakuja Nipashe na kwenda (anataja gazeti jingine la kila siku),” alisema Nape.

Baada ya maelezo hayo, Nape alisema: “Mwaambie wenzako kuwa uchaguzi umeshaisha na hata kama hamkubali CCM imeshinda na watatawala miaka mitano.

“Nyinyi mkiendelea kutumiwa kubeba ajenda ambazo hazina maana wala msingi na nimeshalisema sana hili. Kama kuna tatizo katika kikao chochote, mnatakiwa kutaja maeneo mahususi si kujumuisha maeneo yote,” alisema.

Alisema kila ngazi ya chama kuna msemaji wake na kama ni Mkoa wa Mara tukio lilipotokea, waulizwe wao.

“Mnachotaka kufanya ni kuifanya story (habari) iwe juu na ili iwe juu ni kumwuliza Nape, CCM ina Katibu Mwenezi Wilaya na Mkoa, ikishafikia ngazi ya taifa nitajibu, msilichokonoe, hili zoezi umenielewa?

‘’Nchi hii haiwezi kuendeshwa kila siku na siasa tu, mbona yapo mambo mengi ya kulifanya taifa hili lisonge mbele, kwa sababu wamekosa ajenda basi wanatafuta uchafu wa kufagia na smenti, natumaini story hamtaiandika vibaya, (anataja jina la gazeti lililofutwa) niliwaambia mkienda huku mimi nawafungia wakasema Nape anasema tu, sasa hivi mimi Waziri na Katibu Mwenezi wa chama be careful (kuwa mwangalifu),” alisema.

Aliongeza kuwa: “Mara yenyewe mimi ni mlezi wa Mara, kuna mahali wamekaa pale Rorya wakafukuzana, waulizeni ni hii ni stori ndogo sana ila mnataka kuikuza mnaniuliza mimi, mtu anayekwambia tumeagizwa si unamwambie awape ushahidi, kwa nini mnakimbilia kwangu, mchezo wa waandishi naujua, mnataka Nape azungumze ili story iwe kubwa,” alisema.

tiffah-pinkDIAMOND-PLATNUMZ
Musa Mateja, AMANI

DAR ES SALAAM! Hii ni EXCLUSIVE stori! Kufuatia kelele kibao kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, yaani Latifah ‘Tiffah’ aliyemzaa na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ si wa nyota huyo, hatimaye, jamaa ameamua kupima vinasaba ‘DNA’ (DeoxyriboNucleic Acid).

ISHU ILIKUWA AFRIKA KUSINI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Diamond aliamua kutekeleza mpango huo nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako aliamini hakuna ‘macho mengi’ ya watu, hususan mapaparazi.

SIKIA HII
“Jamani mimi nataka niwape stori ambayo ni ya uhakika. Hivi mnajua kwamba Diamond aliamua kwenda Sauzi kupima DNA yake na mtoto wake Tiffah?
“Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.”

MAJIBU HAYA HAPA
Chanzo hicho kikasema: “Majibu ya DNA yamesema, Nasibu Abdul ni biological father (baba wa damu) wa mtoto Tiffah. Ilibidi jamaa amwage chozi maana alifikiria mengi, watu wamesema sana kuhusu yeye na Tiffah, kwamba si mwanaye, mara ni mtoto wa Ivan (Ssemwanga, mtalaka wa Zari), mara ni mtoto wa pedeshee mmoja wa Bongo. Yaani mengimengi yalisemwa.”

MAMA DIAMOND ASHANGAZWA
Chanzo hicho kikazidi kuweka wazi kwamba majibu hayo ya DNA yalimshangaza mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ hasa kutokana na maneno yaliyosambaa katika jamii, kwamba kijana wake huyo alibambikwa mtoto.

DIAMOND NA AMANI
Baada ya madai hayo, gazeti hili lilijihangaisha kwa kuzingatia weledi ili kumpata Diamond mwenyewe kwa lengo la kumpa nafasi ya kujieleza kama taaluma inavyotaka kwamba anasemaje kuhusu kuwepo kwa habari hii mpya kabisa ya kupima DNA.

KUMSIKIA DIAMOND, BONYEZA SOMA ZAIDI

“Yeah! Unajua watu wamesema sana. Wametunga sana, mimi sikuwa na wasiwasi, niliamini mtoto ni wangu, ila ili kujiridhisha zaidi nikasema niende nikapime DNA yangu na ya mtoto.
“Tiffah ni mtoto wangu kabisa, nimefurahi kwa majibu. Ndiyo maana sasa nimejiachia, ukifika ofisini kwangu nimeweka picha zake kwenye fremu. Sina wasiwasi kabisa mimi si mtu wa mikono kichwani tena.”

MAHOJIANO
Amani: “Ni kweli ulitoa machozi?”
Diamond: “Siyo ishu, kama unaishi katika nchi yenye baadhi ya watu wanaozusha maneno kama yale halafu unagundua ni uzushi wao tu, kulia ni nini?”
Amani: “Unasema tangu awali ulijua Tiffah ni mtoto wako, kwa nini uliamua kwenda kupima DNA?”
Diamond: “Utamaduni wa kutopima ni sisi Wabongo tu, wenzetu mbele siyo ishu. Ni kujiridhisha kwa asilimia mia moja tu. Bongo ukimwambia mwenzio mkapime DNA ya mtoto, anaweza kukujia juu kwamba humwamini.”

KUHUSU PEDESHEE KUDAIWA NDIYE BABA WA MTOTO
Diamond: “Nimesikia wakisema hivyo, lakini mimi nataka kuwaambia kwamba, huyo pedeshee (jina lipo) hajawahi kuwa mtu wa Zari. Mimi ndiye ninayejua nini kilitokea! Hao wanaosema waache waseme tu.”
Amani: “Nini kilitokea? Gusia kidogo tafadhali.”
Diamond: (kwa tabu sana), “kifupi nilimzidi jamaa mahesabu, mimi nikaondoka na Zari. Ndiyo maana leo hii nampa heshima kwa sababu hakuwahi kufanya lolote hapa Bongo.”

KUHUSU IVAN
Amani: “Wanaposema Tiffah ni mtoto wa Ivan, wewe unachukuliaje?”
Diamond: “Ingewezekana vipi! Watu watofautiane, miaka ipite halafu waseme mtoto ni wake! Mimba inakaa tumboni kwa miaka mingapi?”

MAMA DIAMOND AMEANZA MAMBO YAKE
Juzi, Amani lilimpigia simu mama Diamond kwa lengo la kumuuliza kuhusu alivyojisikia baada ya majibu ya DNA kuonesha kuwa, Tiffah ni mjukwuu wake kabisa lakini simu yake iliita bila kupokelewa, licha ya kupigwa mara kadhaa. Tabia ya kutopokea simu alikuwa nayo zamani, hapo katikati akaiacha. Inaonekana ameirudia tena!



                                                  WANAMUZIKI

No comments:

Post a Comment