N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Friday, June 10, 2016

Halmashauri ya Mji wa Kibaha yakamilisha miradi mitano ya maji








DUKA LA VIFAA LA AZAM FC LAZINDULIWA LEO NDANI YA BOTI YA KILIMANJARO 6.

Wafanyakazi wa Duka la Azam wakionyesha baadhi ya Jezi za  Timu ya Azam zinazopatikana katika Duka Maalum lililofungulia ndani yaboti ya Kilimanjaro 6 leo.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba  akizungumza Michuz TV wakati wa uzinduzi wa duka la vifaa vya vya michezo pamoja na vitu mbalimbali vya Azam duka hilo limezinduliwa ndani ya boti ya Kilimanjaro 6 leo.
Wafanyakazi wa Duka la Azam wakionyesha baadhi ya skafu na vitamaa vya  Timu ya Azam zinazopatikana katika Duka Maalum lililozinduliwa ndani ya boti ya Kilimanjaro 6 leo

RC MWANZA AKABIDHI VISIWA KWA MALIASILI.

RC MWANZA AKABIDHI VISIWA KWA MALIASILI. Na Atley Kuni- RS Mwanza. Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameiagiza taasisi ya taaluma ya wanyamapori Pasiansi kuanza kutumia visiwa na majabali makubwa yaliopo mkoani humo kwaajili ya mazoezi ili kuweza kusaidia kupambambana na uhalifu ulioanza kujitokeza katika siku za karibuni katika mkoa huo. Akizungumza katika uzinduzi wa maonesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho nchini Tanzania, Mongella amesema badala ya wakurufunzi hao kwenda kufanya mazoezi kwenye maeneo ya nje ya mkoa ni vema kuanzia sasa mkaanza kutumia visiwa vyetu, “Ndani ya ziwa viktoria, hasa huko visiwani kuna watu wanafanya uvuvi haramu sasa ni vema wakati wa mazoezi mkawa mnafanyia kwenye maeneo hao ambayo yamekithiri kwa uvuvi usio na tija”, alisema Mongella na kuongeza, “lakini sio kukomesha tuu, uvuvi haramu bali pia itachagiza kwenye suala zima la utunzaji wa mazingira na maliasili” Amesema kuwa, endapo taasisi hiyo ikitumia sehemu ya mafunzo kwa vitendo, kama mkoa utakuwa hauna haja yakufunga shughuli za uvuvi kwa msimu na badala yake itasaidia kwenye uzazi salama wa samaki na viumbe wengine wa majini. Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho bi Lowael Damalu, amemuelezea mkuu wa mkoa kuwa chuo hicho hivi sasa, kinauwezo wakudahili wakurufunzi 415 kwa msimu mmoja, ambalo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na wakurufunzi 50, waliokuwa wakidahiliwa na chuo hicho wakati kinaanza mwaka 1966, amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kupata ithibati ya kutoka baraza la Elimu ya ufundi, ongezeko la kozi za askari kuwa (basic technician, Law Enforcement, uboreshaji wa maslahi ya watumishi, mafanikio mengine ameyataja kuwa ni kuongezeka kwa miundombinu na vifaa vya kufundishia, lakini pia taasisi kuwa na tovuti yake ya www.pasiansiwildlife.ac.tz sambamba na taasisi kujipatia ardhi. Mkuu huyo wa chuo amesema mbali yakuwa na mafanikio chuo hicho bado kinakabiliwa na matatizo ya uchakavu wa baadhi ya mabweni, uchache wa nyumba za watumishi, vilevila kutokuwepo kwa sheria ya uanzishwaji wa taasisi sambamba na uhaba wa ajira kwa wakurufunzi wanao hitimu katika chuo hicho

SERIKALI YAPATA GAWIO LA SH. BILIONI 23 KUTOKA KAMPUNI ZA PUMA ENERGY, TIPER (T) na NMB BANK PLC

hazitoi gawio zikisingizia kupata hasara kwenye biashara wakati hawafungi biashara hizo" Alisisitiza Dk. Mpango Dk. Mpango pia amevitaka vyombo vya dola kufanya uchunguzi, ili kubaini mianya ya upotevu wa mafuta bandarini na kuagiza wale wote walihusika na upotevu huo wachukuliwe hatua. " Haiwezekani wajanja wachache wanafaidika halafu wananchi wanyonge wanalala chini hospitalini, Nilisema jana na leo narudia yeyote anayetukwamisha kwenye maendeleo ni msaliti lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria bila huruma,” alisema. Awali Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani, amezipongeza kampuni hizo kwa kutoa gawio hilo na kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango, kuwa gawio litaongezeka kwa kasi kubwa katika miaka ijayo ili kuiwezesha serikali kuwa na uwezo zaidi wa kuwahudumia wananchi. “Mwaka 2014 tulipata gawio la Sh bilioni 3 kutoka Kampuni ya PUMA Energy, mwaka huu tumepata bilioni 4.5 ni matarajio ya Serikali kwa mwendo huu mwakani tunaweza kupata bilioni 6" alisema Dkt. Kalemani. Alitoa wito pia kwa kampuni nyingine zenye ubia na Serikali ambazo hazitoi gawio zianze sasa kutoa akieleza kuwa mantiki ya gawio ni kwamba kampuni inafanya kazi na inapata faida, inapokuwa haitoi gawio mantiki yake ni kwamba kampuni inafanya kazi haipati faida. “Lakini ni vigumu kuamini kama kampuni hazipati faida kwa mfululizo wa miaka 10 na inafanya kazi, sisi tunaamini wanapata faida, na zipo kampuni nyingi ambazo si busara kuzitaja hapa zinadai kupata hasara kila mwaka,” alisema. Kuhusu upotevu wa mafuta bandarini, Dk. Kalemani alisema tatizo hilo hivi sasa limedhibitiwa, baada ya Serikali kuanzisha chombo maalumu kinachoratibu na kudhibiti upotevu huo. Alikuwa akijibu changamoto iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Puma Energy, Dkt. Ben Moshi, aliyeelezea kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2015 kampuni hiyo imepata hasara ya Dola za Marekani milioni 1.4 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 2.5 kutokana na upotevu huo wa mafuta. Kwaupande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tiper (T), inayojihusisha na uhifadhi wa mafuta, ambapo amesema tangu mwaka 2010, kampuni hiyo imetoa gawio la shilingi Bil. 6.4 kwa serikali na kuahidi kuwa gawio hilo litaongezeka siku za usoni. Naye Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, amesema kuwa benki yake inajisikia fahari kubwa kugawa faida iliyopata katika biashara zake kwa mbia wake ambaye ni serikali. Amesema kuwa pamoja na serikali kuwa mbia kwa hisa ya asilimia 31.8, lakini pia ni mteja mkubwa wa benki hiyo ambayo hurudisha faida ya uwekezaji kwa wananchi kupitia gawio hilo na kutoa wito kwa watanzania kuitumia benki hiyo kuweka amana na kukopa Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ambaye ametoa wito kwa wawekezaji wakiwemo wale wanaofanya biashara zao kwa kushirikiana na serikali kufanyakazi zao kwa uaminifu kwa kutangaza faida wanazopata kihalali ili serikali iweze kupata mapato yake yatakayosaidia kuboresha maisha ya wananchi Naye Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru, ameahidi kuyafuatilia na kuyasimamia mashirika yote ya umma na yale ambayo serikali imewekeza, ili kuhakikisha kuwa hawakwepi kulipa gawio ili kuiwezesha serikali kupata mapato yake Imetolewa na Benny Mwaipaja Kaimu Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango 0787087878

Friday, June 3, 2016

LEO KATIKA BUNGE JUNI 3,2016.


=============================================================

JK AOMBELEZA MSIBA WA RAIS WA SAHARA MAGAHARIBI

 
 
===============================================

Banc ABC yaanzisha huduma ya kukuza biashara Afrika









=========================================
 

HEINEKEN HOSTS THE BIGGEST FOOTBALL PARTIES IN DAR TO #CHAMPIONTHEMATCH

===========================================

NAIBU WAZIRI WA HABARI MGENI RASMI AZANIA BANK KIDS RUN 2016 YATAKAYOFANYIKA KESHO KUTWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR E SALAAM













ACT WAZALENDO WATANGAZA SIKU RASMI YA MAPOKEZI YA KIONGOZI WAO ZITTO NA WALE WA UKAWA


Katibu wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO SHAIBU akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi ya kumpokea kiongozi yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE ambaye naye amekumbwa na timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo yatafanyika Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili

Na EXAUD MTEI 

Story ambayo bado ipo maskioni mwa watanzania walio wengi ni mwenendo wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na mizengwe yake ambayo imesababisha wabunge saba wa vyama vya upinzani kusimamiswa kushiriki shughuli za bunge kwa vipindi Tofauti tofauti akiwemo mbunge kutoka ndani ya chama cha Act wazalendo Mh ZITTO ZUBERI KABWE na wabunge wa vyama vya UKAWA.

Sakata hilo limeendelea kuchukua Headline katika maeneo mbalimbali ambapo asubuhi hii chama cha ACT wazalendo kupitia kwa kiongozi wao ADO SHAIBU wamejitokeza mbele ya wanahabari kueleza msimamo wa chama chao kuhusu sakata hilo.


Akizungumza na wanahabari leo Katibu huyo wa itikadi mawasiliano na uenezi wa ACT ADO SHAIBU ameeleza kuwa chama hicho kimeandaa mapokezi ya kiongozi wao ambaye amekumbwa na adhabu hiyo mapokezi ambayo yanataraji kufanyika Jijini Dar es salaam na baadae kufwatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara ambao umepangwa kufanyika katika viwanja vya ZAKIEM mbagala lengo likiwa ni kuwapa nafasi wabunge hao kueleza ukweli wa yale yanayoendelea bungeni Dodoma.

Pamoja na mandalizi hayo chama hicho kimewaandikia barua makatibu wa vyama vya upinzani ambao nao wanapinga adhabu hiyo kutoka CHADEMA,CUF,na NCCR-MAGEUZI kuwaomba kuungana nao katika mapokezi hayo ambayo yamepewa jina la OPERATION LINDA DEMOCRASIA na bado hawajapata majibu yao lakini wanaamini wataungana nao katika Operation iyo ambayo itafwatiwa na mikoa mingine takribani minne.

SHIWATA kumkabidhi Samatta eneo Jumapili

SHEREHE za kukabidhi kiwanja cha ekari tano kwa mchezaji bora barani Afrika, Mbwana Ali Samatta unafanyika Jumapili 5,2016 kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib alisema jana jijini Dar es SAlaam kuwa maandalizi yamekamilika na Mbwana amewasili nchini kwa mechi ya timu ya TAifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Misri utakaochezwa Jumamosi.
Alisema sherehe hizo zitaambatana na ugawaji wa nyumba na misingi ya nyumba kwa wasanii 35 ambao wanafikisha ya wanachama 180 waliokwisha kabidhiwa nyumba zao.
Alisema SHIWATA imemzawadia Mbwana ekari tano ili ajenge kituo cha michezo kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana wa Tanzania watakaolitangaza taifa hili kwenye medani ya michezo kimataifa.
Taalib alisema mtandao huo unaomiliki eneo la ekari 300 za kujenga makazi unawakaribisha wadau wa michezo kuwekeza kwa kujenga kumbi za burudani,shule za michezo, studio za kurekodia, viwanda vya kutengeneza vifaa vya michezo na hosteli za kufikia wachezaji.
Alisema sherehe za kugawa nyumba zinafanyika kwa mara ya tano kutoka ujenzi huo uanze katika kijiji hicho ambapo wanachama 185 wamekabidhiwa nyumba zao walizojengwewa kwa njia ya kuchangishana.
Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa HAbari, Utamaduni na Sanaa, NApe Mnauye ambaye atakuwa waziri wa pili kutembelea kijiji hicho baada ya NAibu WAziri wake, Anna Wambura kutembelea mapema mwaka huu.
Viongozi wengine waliowahi kutembelea kijiji hicho ni kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2014, Wakuu wa wilaya ya Mkuranga wastaafu, Mercy Silla, Clemency na Mkuu wa wilaya hiyo wa sasa, Abdallah Kihato.
Wageni wengine walioalikwa kwenye sherehe hizo ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ITFF), Jamal Malinzi viongozi wa Serikali wa Wilaya ya Mkuranga na wasanii maarufu nchini.
=========================================

SHIMUTA wataka wanamuziki wasio na maadili kupuuzwa








=======================================

Wazanzibari wahimizwa kupanda miti

Na Salum Vuai, MAELEZO
JAMII nchini imehimizwa kujenga utamaduni wa kupanda miti ili kuirejeshea Zanzibar uoto wa asili na kuiepusha na janga la kimazingira.Akizindua zoezi la upandaji miti lililofanyika pembezoni mwa uwanja wa soka wa klabu ya Malindi mjini Zanzibar, mjumbe mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Ali Mzee, amesema miti ni uhai kwa kila binadamu.
Mzee alisema ni jambo la kusikitisha kwamba mazingira ya Zanzibar yamegeuka kutoka rangi ya kijani iliyokuwepo zamani na kuwa yabisi, hali inayosababisha kuongezeka kwa joto.“Bila miti, viumbe hutaabika na nchi inakuwa kavu na maradhi hasa presha huongezeka kila uchao. Lazima tuzinduke kwani tusipopanda miti, tunakaribisha janga kwa taifa,” alisema Mzee. 
Aidha alivitaka vyombo vya habari kuandaa vipindi na makala mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupanda miti.
Mapema, Mwenyekiti wa jumuiya ya Green World Family Foundation iliyodhamini zoezi hilo Nazir Ahmad Bachoo, alisema jumuiya yake inathamini mazingira na imeamua kulifanya zoezi la upandaji miti kuwa endelevu.
Alisema ni jambo lililo wazi kwamba dunia nzima sasa inalia na hali ya joto litokanalo na ongezeko la hewa ukaa (carbon dioxide), inayosababishwa na upungufu wa miti na kuongezeka kwa vyombo vya usafiri barabarani vinavyozalisha moshi kwa wingi.“Umefika wakati sasa kila mmoja ahamasike kupanda na kuitunza miti katika eneo analoishi na yale yanayomzunguka, ili ilete manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho,” alisisitiza.
Kwa upande wake, mratibu wa zoezi hilo na mwanaharakati wa mazingira Mohammed Abdulrahman Bajbeir, alisema Zanzibar imejaaliwa kuwa na wataalamu wengi wa masuala ya mazingira, lakini bado hawajatumika kikamilifu kuisaidia nchi.
Kwa hivyo amezishauri mamlaka za juu kutanabahi na janga la kimazingira linaloinyemelea Zanzibar kutokana na utashi wa binadamu ambao wamekuwa wakikata miti ovyo bila kupanda mingine.
“Zanzibar ya sasa sio kama ile ya zamani ambayo ilijaa kila aina ya miti pembezoni mwa barabara na mitaani. Tunafyeka miti kujenga nyumba za makaazi na maduka tukisahau kwamba miti ni muhimu kwa uhai wetu. Tubadilike,” alieleza Bajbeir.
Wananchi mbalimbali wa mitaa ya Malindi, Mchangani na Mbuyuni wakiwemo wanasoka wa zamani wa klabu ya Malindi SC walioshiriki zoezi hilo, walieleza umuhimu wa kuilinda miti hiyo ili kuunusuru uwanja wa michezo, kwani umekuwa ukiharibiwa sana na watu wanaoweka magari pamoja na mifugo.
Jumla ya miti 41 ya aina mbalimbali ilipandwa kuzunguka uwanja huo, na itakuwa ikilindwa na wananchi kwa kushirikiana na vijana wa ulinzi shirikishi na polisi jamii wa shehia ya Malindi.
==========================================

SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA MWANDISHI WA " THE ECONOMIST" GAZETI LA KIINGEREZA.






MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI PAPOA NEW GUINEA