RC MWANZA AKABIDHI VISIWA KWA MALIASILI.
RC MWANZA AKABIDHI VISIWA KWA MALIASILI. Na Atley Kuni- RS Mwanza. Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameiagiza taasisi ya taaluma ya wanyamapori Pasiansi kuanza kutumia visiwa na majabali makubwa yaliopo mkoani humo kwaajili ya mazoezi ili kuweza kusaidia kupambambana na uhalifu ulioanza kujitokeza katika siku za karibuni katika mkoa huo. Akizungumza katika uzinduzi wa maonesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho nchini Tanzania, Mongella amesema badala ya wakurufunzi hao kwenda kufanya mazoezi kwenye maeneo ya nje ya mkoa ni vema kuanzia sasa mkaanza kutumia visiwa vyetu, “Ndani ya ziwa viktoria, hasa huko visiwani kuna watu wanafanya uvuvi haramu sasa ni vema wakati wa mazoezi mkawa mnafanyia kwenye maeneo hao ambayo yamekithiri kwa uvuvi usio na tija”, alisema Mongella na kuongeza, “lakini sio kukomesha tuu, uvuvi haramu bali pia itachagiza kwenye suala zima la utunzaji wa mazingira na maliasili” Amesema kuwa, endapo taasisi hiyo ikitumia sehemu ya mafunzo kwa vitendo, kama mkoa utakuwa hauna haja yakufunga shughuli za uvuvi kwa msimu na badala yake itasaidia kwenye uzazi salama wa samaki na viumbe wengine wa majini. Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho bi Lowael Damalu, amemuelezea mkuu wa mkoa kuwa chuo hicho hivi sasa, kinauwezo wakudahili wakurufunzi 415 kwa msimu mmoja, ambalo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na wakurufunzi 50, waliokuwa wakidahiliwa na chuo hicho wakati kinaanza mwaka 1966, amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kupata ithibati ya kutoka baraza la Elimu ya ufundi, ongezeko la kozi za askari kuwa (basic technician, Law Enforcement, uboreshaji wa maslahi ya watumishi, mafanikio mengine ameyataja kuwa ni kuongezeka kwa miundombinu na vifaa vya kufundishia, lakini pia taasisi kuwa na tovuti yake ya www.pasiansiwildlife.ac.tz sambamba na taasisi kujipatia ardhi. Mkuu huyo wa chuo amesema mbali yakuwa na mafanikio chuo hicho bado kinakabiliwa na matatizo ya uchakavu wa baadhi ya mabweni, uchache wa nyumba za watumishi, vilevila kutokuwepo kwa sheria ya uanzishwaji wa taasisi sambamba na uhaba wa ajira kwa wakurufunzi wanao hitimu katika chuo hicho
No comments:
Post a Comment