Ngorongoro. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametangaza neema kwa wakazi wa Tarafa ya Ngorongoro ya kutoa maguni kumi kwa kila kaya kwa mwaka ili kusaidia wakazi wa eneo hilo kukabiliana na njaa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Enduleni jana, Waziri Mkuu huyo alisema Serikali imefikia uamuzi huo wa maombi ya wananchi wa tarafa hiyo ya kuomba kuruhusiwa kulima kama njia ya kujikimu kimaisha yakifanyiwa kazi.
Waziri Mkuu alisema Serikali,itakuwa ikitoa gunia tano kwa kila kaya kila baada ya miezi sita na hivyo kaya 20,000 za tarafa hiyo zenye watu 87,000 zitakuwa zikipatiwa magunia 200,000. Eneo hili mnaloishi ni la kipekee dunia kwani limetangazwa ni urithi wa dunia na moja ya maajabu saba ya asili ya Afrika hivyo tunapaswa kulilinda na tukiruhusu kilimo bila kuwa na utaratibu tutaliharibu,”alisema Pinda.
Hata hivyo wakizungumza baada ya ahadi hiyo ya chakula cha bure, wananchi wa tarafa hiyo,walionyesha wasiwasi wao kama ahadi hiyo itatekelezwa kwa kuwa tayari Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamisi Kagasheki aliagiza wapewe chakula bure wakati wa njaa lakini baadaye walitakiwa kununua.
Eliamani Laltaika, William ole Sekei na Nasyera Nangai walisema hawana tatizo na ahadi ya chakula cha bure, lakini uzoefu unaonyesha ni vigumu kutekelezwa kwa kuwa haitawezekana kulishwa kwa maisha yao yote. Ole Sekei alisema kilimo kiliporuhusiwa mwaka 1992 ilitokana na hali ya njaa kama ilivyo sasa na Serikali ilitoa ahadi nyingi lakini hazikutekelezwa . Waziri mkuu,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema ahadi hiyo itatekelezwa mara moja sambamba na kuliongezea fedha Baraza la Wafugaji pia kuongezwa fedha za miradi ya maendeleo kutoka Sh5 bilioni hadi kufikia Sh8 bilioni kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment