N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Friday, September 13, 2013

YALIYOJILI NDANI YA WIKI KATIKA MWEZI WA SEP 2013. NI PAMOJA NA DEMOKRASIA YA KWELI MSINGI WA AMANI, UTULIVU

DEMOKRASIA YA KWELI MSINGI WA AMANI, UTULIVU

 Na Suleiman Abeid
Posted: 02 Sep 2013. www.missdemokrasia.blogspot.com
================

 MWAKA 1992, ni mwaka muhimu kwa Watanzania kufuatia mabadiliko makubwa ya mfumo wa siasa yaliyofanyika ambapo taifa letu lilitoka katika mfumo wa utawala wa chama kimoja na kuanza kutumika kwa mfumo wa vyama vingi.Pamoja na kukubalika kwa mfumo huo nchini kulitokana na busara za uongozi uliokuwepo madarakani wakati huo kuchukua maamuzi mazito ambayo wananchi wengi hawakuyategemea.Maamuzi hayo ni kitendo cha Taifa kukubali kuingia katika mfumo wa vyama vingi wakati wananchi wake waliukataa mfumo huo kupitia Tume maalumu iliyokuwa imeundwa kukusanya maoni ili kuweza kubaini iwapo nchi iingie katika mfumo huo au ibaki katika mfumo wa chama kimoja.


Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na tume iliyokuwa ikikusanya maoni hayo, asilimia 80 ya Watanzania waligoma Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi, huku hoja ya msingi ya kuukataa mfumo huo ikiwa ni kuchelea kutokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.Busara za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere zilisaidia aliposhauri kwamba, pamoja na Watanzania wengi kuukataa mfumo huo ilikuwa vyema mawazo ya Watanzania asilimia 20 waliokuwa wamekubali kuanzishwa kwa mfumo huo yakaheshimiwa na kuchukuliwa.


Kutokana na ushauri huo, hatimaye mwaka 1992, ilikubali kubadili katiba yake na kikubwa katika mabadiliko hayo ilikuwa ni kubadilisha kifungu cha katiba kilichokuwa kikieleza kwamba, Tanzania itakuwa nchi ya chama kimoja na badala yake ikawa, "Tanzania itakuwa ni nchi ya mfumo wa vyama vingi".Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja, katika nchi moja kwa lengo la kuleta ushindani wa kisiasa,

 ili kuleta maendeleo ya nchi.Upinzani wa kisiasa si uadui kama asilimia 80 ya Watanzania waliokuwa wameukataa mfumo huo walivyokuwa wakiamini.Ukweli ni kwamba nchi yoyote ulimwenguni yenye Demokrasia ya kweli inatumia mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa lengo la kuongeza wigo wa Demokrasia kwa wananchi wake ambapo chini ya mfumo wa chama kimoja sehemu kubwa ya wasio wanachama wa chama tawala hawakuwa na eneo la kuchangia mawazo yao katika kuongoza nchi.


Kuanzishwa kwa mfumo huo, kulifungua milango ya kuanzishwa kwa vyama vipya vya siasa mbali ya kile kilichokuwepo Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo vyama vya awali vilivyoanzishwa ni pamoja na Chama cha Wananchi (CUF).Vingine vilikuwa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Demokrasia Makini, Democratic Party (DP), National Convention for Constitution and Reconstruction-Mageuzi (NCCR-Mageuzi), United Democratic Party (UDP), UMD na vingine.


Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2011, zaidi ya vyama vya siasa 18 vilikuwa vimeanzishwa nchini, vyote vikiwa na lengo kuu moja la kupanuaDemokrasia katika suala zima la utawala wa nchi na pia kuweza kupata ridhaa ya kuongoza nchi ambapo kwa kawaida ni chama kimoja tu ndicho hupata ridhaa hiyo.Chama ambacho hakikufanikiwa kupata ridhaa ya kukamata dola na kuunda serikali, lakini kikapata idadi kubwa ya wabunge wanaoingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinapokuwa ndani ya bunge hupewa heshima ya kuongoza kambi ya upinzani kwa maana nyingine hujulikana kama chama kikuu cha upinzani.Upinzani hapa maana yake si kuwa na chama kinachoongoza mapambano yanayolenga kuifanya nchi isitawalike la hasha, maana halisi ni kule kukosoa muswada ama sheria yoyote ile inayopelekwa bungeni ikiwa haina masilahi kwa wananchi.Kutokana na hali hiyo kambi ya upinzani hupinga mswada au sheria hiyo kwa maslahi ya watanzania ambapo pia hupaswa kutoa ushauri wa njia mbadala itumike kwa lengo la kuleta maslahi bora zaidi kwa wananchi.


Ipo mifano mingi juu ya hili mmojawapo ni wa mabadiliko ya sheria ya ukusanyaji maoni Katiba Mpya.Kwa wanaoamini kwamba, uwepo wa vyama vingi nchini ni kwa ajili ya kuleta machafuko, ni wazi wamefilisika kifikra, wanapaswa kufuta mawazo hayo na kurejea katika mistari kwa kuviona vyama vya upinzani vipo kwa ajili ya kukionesha njia ama kukikosoa chama tawala kilichoko madarakani pale kinapokwenda kinyume na malengo ya nchi.Iwa p o c h ama k i l i c h o p o madarakani kitakaa tu katika kiti chake cha enzi na kukosa mtu wa kukikosoa; ni wazi kwamba utawala wake utakuwa ni wa ki-imla na wananchi wanaoongozwa na chama hicho watakuwa wako kifungoni daima kutokana na chama kujisahau kwamba kilichaguliwa ili kiwatumikie wao.Kutokana na hali hiyo kila Mtanzania ana wajibu sasa wa kuviona vyama vyote vya siasa hapa nchini vina haki sawa na tofauti yao ni kwamba, kimoja kati yao ndicho kinachokuwa kimepewa ridhaa ya kuongoza nchi baada ya kunadi sera na ilani yake kwa wapigakura na pale waliporidhika wakakipatia ridhaa hiyo ya kukamata dola na kuunda serikali.


Daima tunapaswa kuelewa kuwa vyama vya siasa ambavyo havikupata ridhaa ya kukamata dola na kuunda serikali si adui au vina lengo la kutaka kuleta machafuko nchini la hasha bali ni kwamba ili Demokrasia ya vyama vingi vya siasa iweze kuwa na maana ni muhimu nchi ikawa katika hali ya amani na utulivu wakati wote.Ili hali ya amani na utulivu iweze kupatikana daima suala la kuvumiliana kati ya wafuasi wa vyama ni lazima lipewe kipaumbele, hasa kwa vyama vile vilivyofanikiwa kupata wabunge wanaoingia bungeni kwa kujenga utamaduni wa kukosoana bila ya kupigana au kuzomeana.Katika hili chama tawala ndicho kinachopaswa kuwa mfano kwa kuelewa ipo siku moja kitajikuta kimekaa katika viti vya upande wa upinzani na kilichokuwa chama cha upinzani ndicho kimekuwa chama tawala, hivyo kisipoonesha mfano mzuri; ipo hatari ya kulipizana visasi ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha kupotea kwa hali ya amani na utulivu nchini.


Ha t a h i v y o , p amo j a n a matatizo yaliyowahi kujitokeza nchini na kuhusisha vyama vya upinzania ikiwa sasa imetimia miaka 21 tangu kuanzishwa kwa mfumo huu, Watanzania wengi wameanza kuielewa vyema dhana ya Demokrasia ya vyama vingi ikilinganishwa na pale mwanzo.Uelewa wa Watanzania utasaidia sana kuifanya nchi kuendelea kuwa ya amani na utulivu na hata kasi ya kuongezeka kwa uchumi itakuwepo iwapo chama tawala kitasimamia katika kuongoza kwa haki na kuwatumikia wananchi waliokiweka madarakani badala ya kujali masilahi binafsi, maana haki ndiyo msingi mwingine wa amani.


Mara kwa mara CCM imekuwa ikikiri maneno ya hayati wa Baba wa Taifa, aliyowahi kusema enzi ya uhai wake kwamba, “pasipokuwa na haki hapawezi kuwa na amani,” Kauli hii ni sahihi maana Tanzania kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuwa nchi yenye amani na utulivu kutokana na sera zake zinazoweka mbele uhuru, haki, usawa na utu.Msingi huu uhakikishe hauvunjiki daima hata kama CCM itaondoka madarakani na kuwepo kwa chama kingine cha siasa, ili amani iweze kuendelea kudumu hapa nchini ni muhimu kuheshimiana na kuvumiliana.


Kuvumiliana katika suala la siasa ni kitu muhimu, Tanzania ni yetu sote, hivyo si vyema kwa wanachama wa CCM kujiona bora kuliko wale wa vyama vingine, au wale wa vyama vingine kujiona wao ndiyo wanaojua zaidi ya wale wa CCM na kila jambo kinachofanya ni baya.Utamaduni wa kudharauliana ukipewa nafasi ni wazi tutafika sehemu nchi haitatawalika kabisa na hivyo amani na utulivu uliopo hivi sasa vitatoweka kwa kasi ya ajabu baada ya kundi moja kushindwa kuvumilia manyanyaso na vitendo vya haki za wananchi kukandamizwa kwa makusudi.Hivyo kila Mtanzania anapaswa kurejea katika katiba iliyopo sasa ambayo inatamka wazi kwamba, Tanzania itakuwa ni nchi ya mfumo wa vyama vingi vya siasa hivyo ili kifungu hicho kitumike vyema ni vizuri Demokrasia ya kuvumiliana ikapewa uhuru ili kuendelea kuilinda amani iliyopo nchini.

Posted: 02 Sep 2013 ,.www.missdemokrasia.blogspot.com
  • ADAI KUIGOMEA KAMATI KUU,CCM YAMPONGEZA
 Na Charles Mwakipesile, Mbeya


MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, ame s ema b a a d a y a kuteuliwa kwenye nafasi ya ujumbe wa tume hiyo, alikula kiapo cha kutetea masilahi ya Watanzania si ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Prof. Baregu aliyasema hayo juzi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia jijini Mbeya wakati akifungua Baraza la Katiba jijini humo na kuongeza kuwa, huo ndio mwanzo wa mgogoro uliokuwepo kati yake na viongozi wa CHADEMA.


"Wote mliofika katika baraza hili, mmeheshimiwa sana na Watanzania wenzenu waliowatuma mbebe mawazo yao ili yawekwe kwenye Katiba Mpya ambayo itadumu zaidi yamiaka 100...nawaomba msitetee masilahi ya vyama vyenu bali ya Taifa," alisema Prof. Baregu.Aliongeza kuwa, mbali ya kuwa mjumbe katika tume hiyo pia ni Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA ambapo wakati fulani kulikuwa na sintofahamu kati yake na viongozi wake.


Alisema CHADEMA walimtaka afike kwenye Kamati Kuu lakini aliwagomea kwa sababu alitambua alichokuwa akikifanya, kilikuwa kwa manufaa ya Watanzania si chama chake."Mimi s i k u a p a k u i t e t e a CHADEMA hata kama ni kada wake bali niliapa kuitetea Tanzania na wananachi wake, vyama vya siasa vinaweza kufa lakini Tanzania haiwezi, itaendelea kuwepo milele hivyo lazima tuheshimu hilo," alisema.


Prof. Baregu alisema kwa kutambua umuhimu wa vyama vya siasa kupewa nafasi na tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba, ilitoa nafasi kwa vyama hivyo kuunda Mabaraza ya Katiba, kukusanya maoni yao na kuyapeleta kwenye tume.Alisema fursa hiyo ndiyo inayoweza kutumiwa na vyama hivyo kutetea masilahi ya vyama si kwenye mabaraza ya wananchi.


"Vyama vya siasa vina nafasi yao ya kuunda Mabaraza ya Katiba na kujadili kwa mfumo ambao wataona unafaa, haya mabaraza tuwaachie wawakilishi wa wananchi ambao ndio ninyi."Hata katika tume, kuna wakati tulikuwa tukitofautiana mawazo lakini tunafikia muafaka kwa mfano, mimi ni muumini wa Serikali moja lakini nimewaletea rasimu yenye Serikali tatu," alisema.


Maelezo hayo ya Prof. Baregu, yaliwafanya wajumbe waliotoka CCM katika mabaraza hayo, kumpongeza kwa busara zake za kutanguliza uzalendo na masilahi yaTaifa.C HADEMA kilitangaza kujitoa ka tikamcha katow a mabadi liko yakati ba nakuda imchakatohuoumetekw an aCC Mnakudai wajumbew atu mehiy o h awanaweledi wa kutosha kufanya kazi hiyo.


Kuto kana nahalihiyo, cha mahichokilidai h akir idhishwina mchak atom zima wakut ungaKatibaMp ahivyok ilim takaProf. Baregu ajitokekw enyetum eili chamakianzis hekamp eninc hinzima ya kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo.
Posted: 02 Sep 2013 08:59 PM PDT


 Na Darlin Said

ZAIDI ya sh. bilioni 881, zitatumika katika mradi wa kusambaza umeme vijijini na kuwanufaisha zaidi ya wateja 250,000.Mwenyekiti wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Balozi Ami Mpungwe, aliyasema hayo Dar es Salaam jana baada ya kusaini mikataba 15 ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini awamu ya pili. Alisema lengo la mradi huo ni kusambaza umeme katika mikoa 24 ya Tanzania Bara hususan vijijini na kwenye Makao Makuu ya Wilaya 13 zisizo na umeme."Utekelezaji wa miradi katika mikoa 14 iliyopata makandarasi, unaenda sambamba na ujenzi wa vituo sita vya usambazaji umeme ambavyo vitajengwa Tunduru, Mbinga, Ngara, Kigoma, Kasulu na Kibondo," alisema Balozi Mpungwe.


Alitaja mikoa iliyopata makandarasi kuwa ni Ruvuma, Arusha, Dodoma, Mara, Iringa, Kilimanjaro, Singida Mtwara, Mwanza, Tabora, Njombe, Katavi, Shinyanga na Simiyu ambapo mikoa 10 haijapata makandarasi."Katika kutekeleza miradi hii, huduma za kijamii kama shule, zahanati na visima vya maji vitapewa kipaumbele kwa kuunganishiwa umeme," aliongeza.Wakati huo huo, Balozi Mpungwe aliwataka wakandarasi wote kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza wajibu wao kulinganana mikataba na wale ambao watakwenda tofauti hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


Alisema asilimia 98 ya vijiji vilivyopo nchini, vina matatizo ya kupata umeme usio na uhakika hivyo kuanzishwa kwa REA, kumesaidia ongezeko la upatikanaji umeme katika maeneo hayo kwa asilimia saba ukilinganisha na awali ambapo asilimia 2.5 ya wananchi waishio vijijini ndio waliokuwa wanapata umeme.Naye Kaimu Mkurugenzi wa REA, Bw. George Nchwali, alisema Utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini ni sehemu ya juhudi za Serikali kufanikisha Mipango ya Maendeleo ya Taifa kama ilivyoainishwa katika Dira ya Maenedeleo ya Taifa kufikia asilimia 30 wa wananchi waishio vijijini, wanapata umeme ifikapo mwaka 2015
Posted: 02 Sep 2013 09:04 PM PDT
  • RPC ALIPONGEZA MAJIRA KUWAFICHUA MATAPELI
Na Waandishi Wetu

SIKU chache baada ya gazeti la Majira kuandika habari iliyofichua uhalifu mkubwa uliokuwa ukifanyika kwa abiria kwenye Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo, Dar es Salaam (UBT), baadhi ya askari polisi wa Kituo cha Polisi Ubungo, wamehamishwa vituo vyao vya kazi .Akizungumza Dar es Salaam , Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura, amekiri askari hao kuhamishwa vituo vya kazi na kudai huo ni utaratibu wa kawaida unaofanywa na jeshi hilo mara kwa mara. 

Wakati Kamanda Wambura akitoa ufafanuzi huo, baadhi ya askari polisi wa kituo hicho, walihusishwa na vitendo hivyo kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na gazeti hili.Katika matoleo yaliyopita, Majira lilizungumza na baadhi ya viongozi wanaosimamia kituo hicho na Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (TABOA), ambao walisema baadhi ya askari polisi wa kituo hicho, wapo karibu na mtandao wa matapeli hao.

Viongozi hao walishauri askari hao, wahamishwe vituo vya kazi na kufanya operesheni endelevu ili mtandao husi usipate nafasi ya kuendelea kuwatapeli abiria wanaotoka mikoa ya mbali kama Kigoma, Kagera na nchi jirani za Uganda, Kenya, Malawi na Bunjumbura. KamandaWambu raali sema, operesheni n dani yaki tuohichoita endelea na kulipongeza gazeti laMajirakw akaziku bwanan zuriwaliyofan yaku fichu amtan dao huo.

"Nawapo ngeza  kwa kazi nzuri, ilikuimarisha  ulinzi katikakituohik i,Jeshi l a Polisi litashir ikiana naTA BOA,u ongozi waUBTna wananchi ilikukomesha uhal ifuuliokuwaukifanyika kw aabiri a,"alisem a. Baadhiy aab iriakit uonihapo ambaowalizungumza naMajira, walisem a ulinzi katikakitu o hichoumeima rishwatofauti naawali ambapobasi l ilikuwalik iingiakulikuwana makundi ya w atuwaliokuw awakiyavamiana kuwaka mataabiri a.

Kwaupa ndewao, TABOA wa mesem awa potayari kush irikiana najeshihi loku komeshauhalifundan iyaki tuohichoili kuondoakerok ubw ailiy okuwa ikiwakabili abiria.Akizungumza na Majira, KatibuMkuu wa TABOA, EneaMrutu alise ma waohaw anat atizoj uuya hilonak wam bawapo tayar iku toaushirikianao na jeshi hilo mchana na usiku.

Posted: 02 Sep 2013 09:07 PM PDT

 Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa amri ya kukamatwa wadhamini wawili waliowadhamini raia wawili wa Pakistan waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kukutwa na dawa za kelevya kinyume cha sheria ili waitwe mahakamani na wajieleze baada ya washtakiwa waliomdhamini kukimbia.

Wadhamini hao ni Amiral Sharif, mkazi wa Kisutu na Elias Kumrudin, mjumbe wa nyumba 10 Mtaa wa Libya .Wengine ni Mohamed Bahishi, mkazi wa Chang'ombe, Dar es Salaam na Nazar Mohamed Nuru, mkazi wa Mtaa wa Libya, Kisutu, Dar es Salaam, ambao ni waajiriwa wa kampuni ya Songea Mining & Construction Ltd Holdings. Amri hiyo ilitolewa jana mahakamani hapo na Jaji Grace Mwakipesile, baada ya washtakiwa hao na wadhamini wao, kutokutokea mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.Mahakama hiyo pia imetoa hati ya kuwakamata washtakiwa hao, ili kufikishwa mahakamani kuendelea na kesi inayowakabili.

Washtakiwa waliokimbia ni Abdul Ghan Bux na Shahbaz Malik, pamoja na Watanzania wawili Fredy William Chande na Kambi Seif ambao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kuingiza dawa za kulevya nchini kinyume cha Sheria ya Kuzuia Usafirishaji na Biashara ya Dawa za Kulevya.Katika kesi hiyo namba moja ya mwaka 2012, washtakiwa hao wanadaiwa kuingiza nchini dawa hizo aina ya heroin ambazo zinadaiwa kuwa na thamani ya sh. bilioni 6.Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa jana hatua ya awali ambapo washtakiwa hao wangesomewa maelezo ya awali juu ya mashtaka yanayowakabili, lakini ilikwama kusikilizwa baada ya washtakiwa wawili (Wapakstani) kutokomea kusikojulikana.

Kutokana na hali hiyo, Wakili wa Serikali Theophil Mutakyawa, alidai kesi ilipangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali lakini aliiomba mahakama itoe amri ya kukamatwa washtakiwa na wadhamini wao kwa kutofika mahakamani.Alidai kumbukumbu zinaonesha Julai, 2011, washtakiwa wote walipewa dhamana na mahakama hiyo hivyo mshtakiwa wa tatu na nne, wamekiuka masharti ya dhamana kutokufika mahakamani."Katika mazingira haya ni rai ya Jamhuri kwamba itolewe hati ya kuwakamata washtakiwa namba tatu na nne ili waweze kufika kwa tarehe itakayopangwa, pia itolewe hati ya wito wa mahakama kwa wadhamini wao waje wajieleze," alidai Mutakyawa.

Jaji Mwakipesile, alipomuuliza Wakili wa washtakiwa hao, Yassin Membar, alijibu hana taarifa zozote za washtakiwa hao hivyo alikubaliana na maombi ya Jamhuri kuamuru washtakiwa hao wakamatwe na samansi kwa wadhamini wao kama upande wa mashtaka ulivyoomba.Kesi hiyo iliahirishwa hadi tarehe nyingine itakayopangwa na Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu.Washtakiwa hao wanadaiwa kwa nyakati tofauti kati ya Januari mosi na Februari 21, 2011 katika maeneo tofauti nchini na Pakistani, walikula njama na kutenda makosa ya kusafirisha, kuingiza nchini dawa za kulevya.Inadaiwa walikamatwa Februari 21, 2011, Mtaa wa Jongoo eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam, wakiwa na dawa hizo zenye uzito wa gramu 179,000 zenye thamani ya sh. bilioni 6.2.

Wakati kesi yao hiyo ikiendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, katika hatua za awali, washtakiwa hao waliwasilisha Mahakama Kuu, Dar es Salaam, maombi ya dhamana.Wakati maombi hayo yakisikilizwa, upande wa utetezi ulidai hakuna uthibitisho wa thamani ya pesa za dawa hizo kwani hakuna hati inayothibitsha thamani hiyo.Mawakili wa utetezi walidai hata hati ya mashtaka haielezi ni nani aliyetuma dawa hizo kutoka Pakistan na aliyezipokea nchini.Waliongeza kuwa, hati ya mashtaka haikueleza taarifa binafsi za washtakiwa kama umri na utaifa wao hivyo kutokana na dosari hizo washtakiwa wana haki ya kupewa dhamana.


Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Julai 6, 2011, Jaji Upendo Msuya aliwapa dhamana, akisema upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha sababu za kuwanyima dhamana baada ya ukikiri kutowasilisha nyaraka muhimu za kutetea hoja zao.

Posted: 02 Sep 2013 09:11 PM PDT

Na Rehema Mohamed

MAHA KAMAK uu KandayaDares Salaam imeshindw a kuanzakusik iliza Rufaaya Mkurug enziwaM ashta kanchini( DPP) dhidi yaal iyekuwaBaloz iwaTanzani anchini Italia,Pro fesaCost aM ahaluna mwenz akekuto kanan akutope wakumbuku mbuzakes i yauhujumuuchumiiliyo ku waiki wakabili katikaMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu .Katikakesihiyo Mahalualishtakiwa pamo ja naaliyekuwa MkuuwaFedhana Utawala katika ubaloz i hu o, Gra ceMartin.JanaRuf aah iyoil ile twamahaka maniha pombe leyaJaji JohnUtamwakwaaji li yakua nza kusik ilizwa a mba poupan dewaMashta kaulikuwau kiwak ilishwanawakiliwa serikali, TimonVitalis na walikuw ataya ri kwausiki lizwaji.

Hatahiv yo,Jaji Uta mwaaliieleza mahakama kuwa,ha watawezakusikilizakesi hi yokutokana nakutopewa rekodi hizo za ma hakama.Katika hatuanyingine W akili wa Utetezi,Beatu s Malimaalielezakuwam aw akiliw anaomteteamrufan iwakwanz a(Prof.Mahalu) ambaon i AlexMgongolwanaMabere Marand o wanaudhu ru, hivyowameshindwa kufika mahaka mani hapo.Kutok ananahal ihiyo,Jaji Utamwaalia hiri shas hauri hilohadi No vemba11mwaka huu kwa ajiliyausikiliz wa ji.Baa dhiy ahoja zaDP Pkatika rufaahiyo ni pamoja nak wambahakimu waMa hakamaya HakimuMkaziKis utualikose akisheria kusemak uwa, mjiburufani kusa ini mikatab amiwili hali kuwakosalajinai.

Hoja nyingine ni kwamba, hakimu huyo alikosea kisheria kukubali na kutumia ushahidi usiokubalika na kuwaachiwa huru wajibu waliokuwa washtakiwa wa kesi hiyo.Nyingine ni kwamba alikosea kisheria kuamua kuwa, upande wa mashtaka haukuweza kuthibitisha mashtaka yao bila kuacha mashaka yoyote.Kutokana na hoja hizo, DPP anaiomba mahakama hiyo itengue hukumu hiyo iliyowaachia huru Mahalu na mwenzake kisha iwatie hatiani na kuwahukumu adhabu kwa mujibu wa sheria na kutoa amri nyingine yoyote itakayoona kuwa inafaa.Prof. Mahalu na mwenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka sita yakiwamo ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60, katika mchakato wa ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.

Posted: 02 Sep 2013 09:17 PM PDT

 Na Eliasa Ally, Kilolo

HAL MASHAURIya WilayayaKilolo iliyop omkoani Iringakwamud awamiezi mitatu ime wezak uku sanyamapato ya ndanish. 295 ,144,378.33kutokakwenye v yanzombalimbali vyamap atoyak eyand an i nakufikia asili mia97 yale ng olakuk usanyamapato.Akizungumza jana wakati akitoa taa rifayau teke lezaji wash ughuli zaseri kal ikwakipindi c hamieziminneofi sinikwake, M kuuwaWilaya yaKilo lo, GeraldGuni nita alisema kuwa wilaya hiy oiliku waimejiwekeamalengoh ayona kuvukaasili mia60 .


Alise makuw amapato hayo yameanza kukusanywa kuanzia mwezi Mei hadi Agosti mwaka huu ambapo mapato hayo yanatokana na vyanzo vya ndani yakiwemo mbao, mazao ya kilimo, mifugo, biashara ndogondogo na kubwa ndani ya wilaya hiyo.Guninita alisema kuwa katika mwezi wa Julai, Wilaya ya Kilolo iliweza kukusanya jumla ya sh.69,014,520 sawa na asilimia 60 kwa mwezi huo pekee ambapo fedha hizo zilikuwa zimetumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali za wilaya na miradi kupitia idara zake zilizomo wilayani humo za ujenzi, elimu, barabara, maji, afya, kilimo, umeme, mawasiliano na misitu.


Alisema kuwa katika idara ya ujenzi wilaya hiyo kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali ambapo baadhi ya shughuli hizo zimekamilika ambapo jumla ya sh. 1,729,481,900 zimetumika na miradi hiyo inaendelea kutekelezwa kuanzia kipindi cha mwezi Mei 2013 hadi Agosti 2013 na kuwa baadhi ya kazi hizo zimekamilika.Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yamefanyiwa matengenezo ya kawaida na ya kudumu katika barabara kuwa ni jumla ya kilomita 54 ambapo kutoka Idete kwenda Kiwalamo hadi Kimara kilomita 16 zimetumia sh. 189,960,000, barabara ya Makungu hadi Mlafu kilomita 6 imegharimu sh.mil 86,barabara ya kutoka Ihimbo kwenda Kitelewasi kilomita 20 imegharimu sh. milioni 285, barabara ya Ruaha Mbuyuni kwenda Msosa kilomita 7 imegharimu sh.53,607,000 ambapo barabara ya kutoka Ukumbi kwenda Pomerini kilomita 5 imegharimu sh.milioni 20.

“Ujenzi wa madaraja mawili na vivuko vya barabara ya Idete, Kimara hadi Kiwalamo tumejenga madaraja makubwa mawili na makaravati kwa sh. 153,130,000 ambapo daraja la Kiwalamo pekee limegharimu gharama ya sh. milioni 108 na tunashukuru kazi hizo zimeweza kukamilika kwa muda mwafaka ambao ulipangwa na kukubaliana na wakandarasi na kuzikamilisha”, alisema Guninita

Posted: 02 Sep 2013 09:14 PM PDT

BODI yaKo roshoTanzania imet ang azabei e lekezi yakoro sho k uwanish .800kw akilokwakoro sh od araj ala kw anz anakorosho da rajalap ili ni sh600k wa msimuw amwa ka 2013hadi2014, anaripoti Mwandishi Wetu .Beih iyoi litangazw a ju zi kwenye kikao cha wadauwakoroshokilichofa nyika sikumbil i Mjini Dodomakwakujum ishawadauwotehapa nch ini.Ak itangazabeihiyo Mkurugenzi wa Bodi, Mfaume Juma, alisema kuwa soko la korosho nchini India halijatulia hivyo bei ya korosho nchini India kwa kilo ni sh.1070 ambapo kwa mujibu wa utafiti kuhusiana na gharama za korosho imefikia sh. 724. 


Mfaume aliwataka wakulima wa korosho kuelewa kwamba bodi hiyo imeweka bei hiyo ndogo ili kuwavutia wanunuzi kuliko bei kubwa ambayo haina tija.Alitolea mfano nchi za Magharibi kama Ivory Coast na Senegal kwamba ni wakulima wakubwa wa korosho Barani Afrika lakini wanauza korosho kwa bei ya chini inayofanya hawawi na matatizo. Aidha alisema kuwa ni vyema korosho zikabanguliwa hapa nchini ili kuondokana na dhana ya uuzaji wa korosho ghali, ambapo aliongeza kuwa soko kubwa la korosho ni nchini India ambapo zinabanguliwa kabisa na kwenda kuuza nchi nyingine. 


Alisema kuwa Vietnam ni wafanyabiashara wa korosho lakini wanategemea sana korosho kutoka nchi za Afrika Magharibi na zinapomalizika ndipo wananunua korosho za Tanzania.Kwa upande wao wadau wa korosho hawakuridhika na bei na kwamba bei haiendani na gharama na kwamba utafiti uliofanywa haukuzingatia gharama za uendeshaji za wakulima. Akichangia mada Mbunge wa Mtwara Vijijini, Bi. Hawa Ghasia, alisema mfano takwimu zilizotolewa si sahihi na kuiomba bodi hiyo ikae na kufanya utafiti upya kwa kuwashirikisha wakulima.


Katika mkutano huo wadau wengi walionesha kutoridhika na bei ukizingatia kwamba ushauri uliotolewa wa kukusanya korosho na kupelekwa ghalani kwa ajili ya kusubiri mnada ili walipwe fedha ni kutafuta migogoro kwa wakulimaAidha wadau hao waliomba kuendelea na mfumo wa stakabadhi ghalani lakini walipwe kwanza tofauti na sasa ambapo wakulima wanalipwa sh. 600 halafu baadaye wanamaliziwa sh.200

Posted: 02 Sep 2013 09:20 PM PDT

 KAMPUNI ya vinywaji b a r i d i y a Co c a -Co l a imezindua promosheni mpya ya 'Amsha Maisha Yako na Coca Cola' pamoja na wateja kujishindia pikipiki, anaripoti Mwandishi Wetu.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo juzi meneja wa bidhaa wa Coca Cola Maurice Njowoka alisema wanunuzi wa bidhaa za kampuni hiyo watajipatia nafasi ya kushinda pikipiki 200.  N j o w o k a a l i s e m a ma d h umu n i y a k u t o a pikipiki ni kusaidia kutoa ajira kwa vijana 200 ambao wataendesha ambapo kwa sasa zinatumika zaidi kwa usafiri wa haraka.“Tumeona ni vizuri kama safari hii tukatoa kitu, tungeweza kutoa magari, lakini yasingekua mengi kama hivi, tunaamini pikipiki ndiyo chombo kinachotumika zaidi kwa sasa,” alisema.

Al i s ema k i l a mt e j a atakayenunua vinywaji vya Coca Cola, Fanta, Sprite na Stone Tangawizi atapata nafasi ya kushinda pikipiki hizo kila kona ya nchi.“Kinachotakiwa kufanywa ni kukusanya vizibo vitatu vya soka ambapo ndani kutakuwa na alama tatu, moja kipande cha pikipiki cha mbele, kati na nyuma, hivyo ukipata vyote vitatu utakuwa umeshinda,” alisema.Mbali na zawadi hiyo kutakuwa na pesa taslimu ambapo wanywaji wa soda watapata fursa ya kujishindia kuanzia sh. 1,500,000, 100,000, 50,000, 20,000, 10,000, 5,000 na soda  ya bure.“Cha msingi kuzingatia ni kuwa kila kizibo chenye rangi ya dhahabu kitakuwa na zawadi,hakuna mambo ya jaribu tena, hivyo kila Mtanzania atakuwa na nafasi ya kushinda,” alisema.

na kwamba promosheni hiyo itakuwa ni kwa nchi nzima na imeanza rasmi juzi, itaendelea mpaka Oktoba 30.“Kama kampuni kila mwaka tunafanya kutoa asante kwa wateja wetu, mwaka jana tulikuwa na promosheni ya vuta mkwanja na watu wengi walinufaika, hivyo huu ni wakati wao kushinda pesa na pikipiki,” alisem

Posted: 02 Sep 2013 09:30 PM PDT

 Gaston Katindila

Jibu la hoja hii kimsingi ni rahisi, kwani kisheria mtu yoyote anaweza kuteuliwa kuwa msimamizi wa mali za marehemu, kama nilivyosema awali ilimradi apitishwe na wanandugu katika kikao cha ukoo na familia.TUNAFAHAMU kuwa zipo taratibu mbalimbali za kisheria zinazotoa mwongozo wa mambo fulani. Katika suala la mirathi za marehemu zipo taratibu na mwongozo juu ya namna ya uteuzi wa wasimamizi au msimamizi mkuu wa mali za marehemu


.Marehemu anapoacha mali, madai pamoja na haki zake mbalimbali familia ina haki ya kufuatilia na kupata haki zote stahiki za marehemu. Lakini hili limekuwa tatizo kwa watu wengi kwa kushindwa kufuata taratibu za kisheria. Familia nyingi zinapotokewa na tatizo la kufiwa na ndugu au jamaa hushindwa kufuata taratibu za kisheria zitakazowawezesha kupata haki mbalimbali ambazo ni stahiki kwa warithi wa mali za marehemu.


Kuna taratibu zinazotakiwa kufanywa na ndugu wa marehemu ili kuweza kupata uhalali wa umiliki au usimamiaji wa mali zilizoachwa na marehemu.Mara baada ya taratibu za mazishi kukamilika ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wanatakiwa kufanya kikao kitakachokuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo kujadili juu ya mali za marehemu.Pamoja na kujadili mali na mambo mengine ya kifamilia yanayomhusisha marehemu lakini pia kikao hicho kinatakiwa kumteua msimamizi wa mirathi ambaye kama ilivyozoeleka ndiye atakuwa msimamizi mkuu wa mali zote za marehemu kwa niaba ya wale warithi wanaokubalika kisheria.


Kikao pia kinaweza kumchagua msimamizi wa mirathi zaidi ya mmoja ilimradi tu waridhiwe na mkutano huo wa ndugu. Kuna jambo moja linaloshindwa kueleweka vizuri kwa watu wengi nalo ni juu ya nani anapaswa kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi?Jibu la hoja hii kimsingi ni rahisi, kwani kisheria mtu yoyote anaweza kuteuliwa kuwa msimamizi wa mali za marehemu, kama nilivyosema awali ilimradi apitishwe na wanandugu katika kikao cha ukoo na familia.Lakini ni vyema kwa mtu makini na wakaribu katika familia kuchaguliwa kuwa ndiye msimamizi wa mirathi za marehemu.Na hapa mara nyingi familia huchagua mtu mzima na mwenye busara ambaye wanaamini ataweza kusimamia vyema mirathi hiyo.


Mahakamani kumekuwepo na pingamizi nyingi juu ya wasimamizi mbalimbali wa mirathi, moja ya hoja ambazo zimekuwa zikiibuliwa ni juu ya uhusiano baina ya marehemu na msimamizi wa mirathi, lakini si sababu hiyo pekee zipo sababu nyingine zinazotolewa na wanandugu katika kupinga usimamizi wa mirathi.Mara baada ya uteuzi huo, ni vizuri kwa msimamizi wa mirathi kupata barua ya mwenyekiti au mtendaji wa mtaa kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wake huo.Msimamizi wa mirathi anaweza kwenda kufungua shauri la mirathi katika mahakama yoyote yenye uwezo wa kusikiliza shauri hilo. Msimamizi anatakiwa kupeleka muhtasari wa kikao cha wanandugu kilichothibitisha uteuzi wake, cheti cha kifo pamoja na barua kutoka kwa kiongozi wa mtaa ikithibitisha pia juu ya uteuzi wake huo.


Shauri linapofika mbele ya mahakama, uamuzi wowote unaweza kutolewa juu ya msimamizi aliyependekezwa kuwa msimamizi wa mali za marehemu.Kabla ya kusikiliza shauri mahakama huzingatia pingamizi kutoka kwa wanandugu kama kuna uwepo wa pingamizi lolote.Lakini pia mara baada ya kuchambua ushahidi mahakama huweza kuridhia uteuzi wa msimamiaji huyo wa mirathi au inaweza isiridhie juu ya mtu huyo aliyeteuliwa na wana kusimamia mali za marehemu.Katika mjadala wangu nitaeleza zaidi pale inapotokea msimamizi huyo anapopitishwa na mahakama kuwa msimamizi wa mirathi ya mali za marehemu.

Kumekuwepo na migogoro mingi ya wanafamilia na wasimamiaji wa mali za marehemu katika usimamiaji na ugawaji wa mali za marehemu kitu kinachopelekea migongano kwa wanandugu.Wasimamizi wengi wa mirathi hujigeuza kuwa wamiliki wa mali za marehemu na kuwatendea yasiyo mema warithi halali wa mali hizo za marehemu.Niseme tu kisheria msimamizi wa mirathi hana umiliki wa mali za marehemu, wala hana chochote katika fungu la mali za marehemu. Kazi yake ni kusimamia tu mgawanyo na mali zote za marehemu.Dhana ya msimamizi wa mirathi kuwa ndiye mmiliki wa mali hizo zilizoachwa na marehemu imekuwa ikidhaniwa na wasimamizi wengi wa mirathi hivyo kusababisha migongano baina ya wanandugu.


Hii hutokana na wasimamizi kuwanyima warithi halali haki zao muhimu na za msingi juu ya taarifa mbalimbali za mwenendo wa mali zinazosimamiwa na msimamiaji huyo mkuu wa mirathi.Hili pia hupelekea wanafamilia wengi kufika mahakamani na kutaka kumbadilisha msimamizi huyo ambaye wanaona kwa namna fulani anageuza maana ya familia na mahakama kumteua kama msimamizi na si mmiliki. Msimamizi wa mirathi huweza kubadilishwa pale kunapokuwa na haja ya kufanya hivyo, wanandugu na familia huweza kueleza sababu mbalimbali za kutengua na kufuta usimamizi huo mbele ya mahakama.Niseme kwa kuzingatia hoja zilizowasilishwa mahakama yaweza kutengua msimamizi yoyote wa mirathi ambaye kwa namna fulani hakubaliki na wanafamilia kwa sababu kama nilizoeleza hapo awali.


I e l ewe k e k uwa wa k a t i wa s imami z i wa mi r a t h i w a n a p o c h a g u l i w a n a kupendekezwa na wanafamilia wasiwe na dhana ya kwamba wao ndiyo wanaokwenda kuwa wamiliki mbadala wa mali zote za marehemu na badala yake wajue kwamba msimamizi wa mirathi ana jukumu moja tu la kusimamia mali zote za marehemu, na si kuwa na miliki dhidi ya warithi wa mali hizo. Warithi wa mali za marehemu wataendelea kuwa na haki zote juu ya mali zilizoachwa hata kama kati ya warithi hao hakuna aliyechaguliwa kuwa msimamizi wa mirath hiyo ya mali za marehemu. 

Mwandishi wa makala haya ni mwanahabari na mwanafunzi wa Stashahada ya Sheria katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto  0716230044 katindilagaston@gmail.com

No comments:

Post a Comment