N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Saturday, September 14, 2013

NI VITA KATI YA NAPE NAUYE VS MBOWE



Katibu wa Itikadi na Uendezi wa Chama Cha mapinduzi (CCM),Nape Nnauye amemtaka Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe kujiuzulu nafasi hiyo mara moja kwa sababu ameshindwa kuiongoza kambi hiyo kusababisha valangati ndani ya bunge kwa mara ya kwanza tangu uhuru wa nchi hii.

Akihutubia mkutano wa hadhara ya maelefu kwa maelefu ya wananchi waliosombwa na malori ya pamba na mabasi kutoka sehemu mbali mbali ya mkoa wa shinyanga kuja kusikiliza ugeni huo wa kuhitimisha ziara ya siku Nne ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana katika mkoa huo.

Nape alisema vurugu zilizotokea hivi karibuni Bungeni ni uthibitisho wa wazi kuwa, Mbowe ameshindwa kuiongoza kambi hiyo kwa kuwa kabla yake hakukuwahi kuonekana fujo na vurugu kama hizo katika chombo hicho kinachoheshimika, alisema udhaifu wa Mbowe katika kuiongoza kambi hiyo ndiyo unaosababisha ishindwe kufanya kile ambacho Watanzania wanakitarajia kutoka kwa wapinzani.

Hata hivyo wakati Nape akisema hivyo Mwanasiasa mkongwe na mwenye nguvu ndani ya chama chama mapinduzi, ndugu Peter Kisumo akizungumzia vurugu zilizotokea bungeni akisema Naibu Spika, Job Ndugai anatumiwa kama buwa tu katika kiti hicho, hajui atendelo, Kisumo alisema alichopaswa kufanya Ndugai baada ya Mbowe kukaidi amri ya kutoka nje ni kumwita mpambe wa Bunge (Sergeant at Arm) na kama ataendelea kukaidi alitakiwa kuahirisha Bunge, “Mbowe alitolewa na Polisi nadhani Naibu Spika alikosea…Mpambe ndiye alipaswa amtoe na akishindwa alipaswa aahirishe Bunge halafu amshtaki kwenye kamati husika,” alisema Kisumo.

Kisumo alisema kitendo cha Ndugai kuamuru Polisi kuingia ndani ya Bunge ambao wamefunzwa kutumia nguvu, kilikuwa ni makosa makubwa na kusisitiza katika hilo Ndugai alikosea, naibu spika hapa alitumia ushabiki wa chama na hakufuata kanuni za bunge, ilifaa aazibiwe na wakubwa zake. Kisumo ambaye ni mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Wadhamini wa CCM, alisema ameanza kupata wasiwasi kuhusu mhimili wa Bunge hususan kiti cha Spika na jinsi wanavyowachukulia wapinzani bungeni. Kiongozi huyo atakuwa ni kiongozi wa kwanza wa juu wa CCM kumsema naibu spika kwamba alikosea kufuata vifungu na kanuni za bunge.

No comments:

Post a Comment