N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Wednesday, September 7, 2011

Warembo walamba bingo ya papazi na kujinyakulia kitita cha DOLA 1000 na Udhamini wa Filamu

 Maafisa wa Papazi wakiongozwa na Mkurugenzi wao, Hans Zakaria, wakipiga picha na Washindi hao baada ya kukabidhiwa zawadi zao
 Washindi Wakionyesha Zawadi zao, kutoka kushoto Christine Mwegoha aliyepata dola 200, Zubeda Self aliyepata dola 1000, na Husna Maulid, Warembo hawa wa Vodacom Miss Tanzania pia watafanya kazi na Kampuni ya Papazi kwa upande wa Filamu.
 Mrembo Zubeda Self, aliyejipatia zawadi ya Kitita cha Dola 1000, akimnanga Muigizaji Nguri wa Filamu,  Jackline  Wolpa, wakati wa kutafuta Miss Vodacom Kipaji cha Uigizaji wa Filamu na Kampuni ya PAPAZI
 Vodacom Miss Tanzania Top Model, Mwajabu Juma(kushoto), akijibizana na Princess Mashonobo.
 Husna Maulid, akionesha Makali yake katika kucheza Filamu na hapa akiigiza kuwa na Machungu
Mshindi wa Vodacom Miss Tanzania, Glori Lory akicheza kipande chake na Yusuf Mlela.

Mgombea wa CCM arejesha Fomu Igunga

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM, Jimbo la Igunga Dk. Dalaly Kafumu(kulia), akimkabidhi fomu yake msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo, Magayane Protace, katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

NIZAR KHALFAN AKABIDHI JEZI KWA JAKAYA




Mtanzania anayecheza soka ya kulipwa katika timu ya white Caps ya jijini  Vancouver ya Canada, Nizar Khalfan, akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Jezi ya timu yake wakati alipokwenda kumsalimu na kumshukuru IKULU jijini Dar es Salaam, (Picha na Fredy Maro)

Monday, September 5, 2011

ZIARA YA DR. NAIBU KATIBU MKUU MIUNDOMBINU, JOHN NDUNGURU, KIVUKO CHA MV- KILOMBERO

 Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(Kulia) na Eng -Msaidizi wa Temesa Ngome Rajabu, wakiwasili kwenye Eneo la Kivuko cha Mv-Kilombero juzi, ambako walikwenda kushughulikia Kivuko cha Mv-Kilombero II kilichokuwa kimeharibika injini moja, lakini hata hivyo walifanikiwa baada ya kuagiza injini mbadala kutoka Songea,
  Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru, akiendelea na zoezi la Ukaguzi wa Kivuko ambacho kilidaiwa kuharibika na hivyo kusitisha huduma ya usafirishaji,
 Kutokana na hali hiyo, Wakazi wa Mahenge walilazimika kutumia usafiri wa Mitumbwi, kwani kivuko cha Mv-Kilombero I akikuweza kukidhi haja za kuondoa msongamano uliokuwapo kabla ya kutengemaa kwa MV-Kilombero II.
  Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(wa pili kulia) akitafakari na baadhi ya watendaji wa TEMESA ambao walifuatana naye kushughulikia Tatizo la Usafiri lililokuwa limejitokeza Kilombero.
 Fundi wa mashine akisimamiwa na eng wa Temesa, kutafuta kifaa kilichodaiwa kusababisha kutofanya kazi kwa kivuko cha MV-Klombero II,
 Wakazi wa Mahenge, wakitelemka kwenye Kivuko cha Mv-Kilombero
 Baadhi ya Wasafiri wakielekea Mahenge, kuvuka mto Kilombero
 Baadhi ya Madereva wakisubiri kuvuka, katika foleni ambayo ilifikia idadi ya magari 62
 Kutokana na hali ya kivuko cha MV-Kilombero kuwa mbaya inasababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo wanaotumia usafiri huo, ususani wenye vyombo vya usafiri kama baiskeli, pikipiki, na magari
 Wafanyakazi wa Kivuko cha Mv-Kilombero wakiendelea na usafi wakati wa matengenezo ya kivuko cha MV- KILOMBERO II
 Hali ya kivuko cha MV-Kilombero I, si shwari
 pamoja na hali hiyo wakazi wa Mahenge na Kilombero hawakuwa na jinsi iliwabidi kuendelea kukitumia, ni hatari lakini salama
 Injini ambayo ilikuwa tatizo baada ya kuharibika, ikiwa tayari kwa ajili ya kuirejesha Dar es Salaam kwa matengenezo
WAUDUMU wa  MV-Kilombero I, wakiendelea kunyonya maji ambayo yanazidi wakati ikiendelea na safari zake
Dereva wa vivuko vya MV-KILOMBERO I na II akiwa hoi bin taabani, hapa akijipumzisha baada ya uchovu wa kila dakika 
hali ambayo ilisababisha msongamano wa Abiria kama hivi,  
 Dr. Naibu katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(kushoto) Eng- Amosi na Msaidizi wa Eng Temea Rajabu Ngome(kulia) wakiendelea kusimamia zoezi la kutengeneza kivuko cha Mv-Kilombero II.
 Askari wa kivuko akiendelea na ukaguzi wa tiketi katika kivuko cha KILOMBERO
 Mashine ambayo ilipelekwa kutoka Songea, ikitelemshwa kwa ajili ya kufunga kwenye kivuko cha Mv-Kilombero II
  Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(kushoto) akiendelea kusimamia zoezi la utengenezwaji wa kivuko cha Mv- Kilombero.
 Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(kushoto) akifurahi baada ya kukamilisha zoezi la matengenezo ya Kivuko cha MV-kilombero II, hapa kivuko kikitoka kufanya safari ya majaribio mbele ya Naibu katibu Mkuu John Ndunguru 
  Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru, akitoa ufafanuzi wa kina kwa waandishi wa habari kuhusiana na kuharibika kwa kivuko cha Mv- Kilombero II, kulia ni  eng msaidizi Temesa-Ngome Rajabu
 Dr. Naibu Katibu Mkuu Miundombinu, John Ndunguru(wa pili kushoto) akiagana na wakuu wa Temesa, baada ya kukamilisha zoezi la kutengeneza kivuko hicho(Picha Zote na Shaaban Mpalule)

Friday, August 26, 2011

WACHEZAJI TAIFA STARS WAITWA KUIVAA ALGERIA, VICTOR COSTA "NYUMBA" YUMO

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo (Agosti 25 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo dhidi ya Algeria ‘Desert Warriors’ kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon.
Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba). Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).
Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Juma Seif (Yanga) na Jabir Aziz (Azam). Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Salum Machaku (Simba).
Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Ramadhan Chombo (Azam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) na John Bocco (Azam).
Timu itaingia kambini Jumapili (Agosti 28 mwaka huu) mchana na jioni itaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Mechi dhidi ya Algeria itachezwa Septemba 3 mwaka huu kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI DODOMA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu Maswali Bungeni, katika kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu leo Augost 25, 2011. kila siku ya alhamisi ya wiki waziri mkuu huulizwa maswali ya ana kwa ana na wa wabunge.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Watoto wa Mbunge wa Viti Maalum, Angellah Kairuki, Ester (kushoto) na Kemilembe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Augost 25, 2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Watendaji waSerikali za Vijiji na Viongozi wa CCM wa jimbo la Magu kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Augost 25, 2011.. Kushoto ni MBunge wao, Dr . Dr Festus Limbu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara,Dr. Cyril Chami kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Augost 25, 2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Kibakwe , George Simbachawene kwenye viwanja vya BungeMjini Dodoma Augost 25, 2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Kamishina wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Bw. T. Alexander Aleinikoff, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Augost 25, 2011.
Mbunge wa Viti Maalum, Dianna Chilolo akimuuliza swali Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kipindi cha maswali Bungeni Augost 25, 2011. (Picha Zote na OFisi ya Waziri Mkuu)

MAZUNGUMZO YANAENDELEA JUU YA UUZWAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI.

(Na Veronica Kazimoto – MAELEZO)
DAR ES SALAAM
Mazungumzo bado yanaendelea kati ya Serikali na Muwekezaji aliyejitokeza kununua jengo la Mahakama ya Rufani iliyopo katika makutano ya barabara ya Kivukoni na Ohio jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Celina Kombani wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.
“Kuhusu suala la uuzwaji wa jengo la Mahakama ya Rufani, mazungumzo baina ya Serikali na muwekezaji aliyejitokeza bado yanaendelea hivyo basi napenda kuwatoa hofu waheshimiwa wabunge kuhusiana na suala hili,” amesema waziri Kombani.
Waziri Kombani amefafanua kuwa mazungumzo yanaendelea baina ya muwekezaji na ofisi mbalimbali za Serikali kama ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mahakama ya Rufani,Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Aidha, Waziri Kombani amesema muwekezaji aliyejitokeza ameahidi kujenga mahakama ya Rufani yenye hadhi kulingana na umuhimu waka kama mhimili mojawapo wa dola.
Kama muafaka utafikiwa kati ya muwekezaji na Serikali jengo hilo la Mahakama ya Rufani litajengwa maeneo ya mtaa wa Chimala mkabala na barabara ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikitoa taarifa kuhusiana na jengo la Mahakama ya Rufani kununuliwa na muwekezaji wa hoteli ya Kempinski na kuwa sehemu ya hoteli hiyo kwa ajili ya maegesho ya magari.
 ..............................................................................................................................................

Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP ni mmiliki halali wa jengo lenye hati namba 56998, Kiwanja namba 22/3/1 lililoko katika eneo la Mabibo Dar es Salaam
Mtandao wa Jinsia ulinunua jengo hilo kutoka kwa Mfilisi (Benki ya Rasilimali Tanzania- TIB) kwa Iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited ambayo ilikuwa sehemu ya kampuni tanzu ya Tanzania Textile Company Limited (TEXCO) kwa gharama ya shilingi milioni 200 ambapo makubaliano ya manunuzi yalifanyika tarehe 15/6/ 1997.
Mchakato wa uuzaji wa jengo hili ulikuwa wa wazi uliotangazwa katika vyombo vya habari nchini hususan magazeti.
Baadhi ya watumiaji wa ofisi waliokuwa ndani ya jengo hilo wakati TEXCO ikiwa inafilisiwa nao walishiriki katika mchakato wa kununua bila mafanikio. Baada ya TGNP kushinda ‘tender’, baadhi ya watumiaji hao , mnano mwezi wa Julai 1997 walifungua kesi namba 215 / 1997 dhidi ya TIB kama mshitakiwa wa kwanza na TGNP mshitakiwa wa pili katika mahakama kuu kupinga maamuzi ya TIB kuiuzia TGNP jengo hilo.
UAMUZI WA MAHAKAMA KUU
Kesi hii ilichukua muda mrefu sana takribani miaka kumi na mbili mpaka kufikia tarehe 15/10/ 2009,uamuzi wa Mahakama Kuu ulipotolewa. na Mheshimiwa Jaji T.B Mihayo wa mahakama kuu hukumu ambayo iliwapa haki TGNP na kuwaamuru walalamikaji kuondoka mara moja na kulipa gharama.
Wakati mchakato wa kutekeleza hukumu ya Mahakama Kuu ukiendelea, mnano tarehe 19/9/2009 walalamikaji walipeleka katika Mahakama ya Rufaa azimio la kusimamisha utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu ya kutowatoa kwenye jengo kwa kupitia ombi na 129 la 2009 ombi lao limetupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa tarehe 23 /8/2011.
MCHAKATO WA KUTEKELEZA UAMUZI WA MAHAKAMA
TGNP wamiliki halali wa hili jengo tunasubiri utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa iliyotolewa terehe 23/8/2011. Tutaendelea kuwataarifu maendeleo ya mchakato huu


Dewji: Mangumbaru wa siasa wananichafua, Apeleka Singida mradi wa maji wa bil 20/-


Na Mwandishi Wetu 
MBUNGE wa Singida Mjini, Mohammed Dewji amesema mangumbaru (watu wenye machachari, matata na fujo) wa siasa wanamchafua, kwa lengo la kuchukua kiti chake cha ubunge. Dewji, maarufu kwa jina la Mo, ametoa kauli hiyo wakati akifanua juu ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya watu waliodai ni wakazi wa Singida, waliodai eti kwamba hajafanya chochote cha maendeleo katika jimbo lake tangu achaguliwe kuwa mbunge. Tuhuma na malalamiko hayo yaliyotolewa na baadhi ya watu waliodai ni wananchi wa Singida kupitia mtandao wa Facebook, wakati wa kubadilishana mawazo na mbunge huyo. Pia Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) aliwataka wana-Singida kuungana na Watanzania wengine kufanya maandamano kudai ahadi ya maisha bora kwa wote kama ilivyoahidiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoko madarakani. Lema akiwa na wabunge wenzake, Chiku Abwao na Regia Mtema (Chadema - Viti Maalumu), alisema hayo wiki hii mjini Singida kwenye mkutano wa hadhara, huku akidai umefika wakati kwa wananchi wa Mkoa wa Singida ambao ni ngome ya CCM, kukiondoa chama hicho madarakani. Katika michango yao kwenye Facebook, wananchi hao walioruhusiwa kutoa maoni na dukuduku zao kwa Dewji, walidai kutoona maendeleo yoyote katika jimbo hilo kwa madai kwamba wananchi wa Singida wamekuwa wakiteseka na maisha kwa kukosa maji, ajira na masuala ya maendeleo. Katika ufafanuzi wake kuhusu malalamiko hayo, Dewji alisema tangu kuchaguliwa kwake amekuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwenye maeneo ya kero za maji. Dewji alisema amefanikisha uchimbaji wa visima virefu zaidi ya 21 kwenye kata za Unyambwa, Mungu Maji, Unyamikumbi, Mwankoko, Mtamaa, Mandewa na Mtipa pamoja na baadhi ya kata za Mjini kama Kindai, Mitunduruni na Utemini. Dewji pia aliongeza kuwa bado anaendelea na jitihada za kukabiliana na tatizo hilo kwa kuibana Serikali itekeleze mradi mkubwa wa Benki ya Dunia wa kuchimba visima 10 jimboni na anaendelea kuibana Serikali ifanye haraka kumalizia mradi mkubwa mwingine wa maji unaofadhiliwa na Benki ya BADEA na OPEC. "Mradi huo ukikamilika ndio utakuwa ufumbuzi wa tatizo la maji Manispaa ya Singida... Mradi huu utabadilisha miundombinu yote ya maji safi ndani ya manispaa yetu. Unatarajia kukamilika mwaka 2013 na utagharimu takriban sh. bilioni 20," alisema Dewji. Kuhusu ajira, Dewji alieleza kuwa amekuwa mstari wa mbele kutoa Ajira kwa vijana kupitia kampuni yake ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL) sambamba na kampuni nyingine mbalimbali. Alifafanua zaidi kuwa yuko mbioni kuwekeza katika jimbo lake kwa kufungua kiwanda kitakachotoa fursa zaidi kwa vijana na wakazi wa Singida kujipatia maendeleo na ajira, na kwamba kwa sasa anaendelea kuwasiliana na wataalamu mbalimbali wa uwekezaji ili kuona kama kuna fursa za kuwekeza katika manispaa ya hiyo. Alipongeza kupokelewa kwa mwito wa kuhamasisha michezo katika jimbo lake na kusisitiza kuwa ataendelea kunyanyua na kuibua vipaji kupitia mashindano yake yajulikanayo kama Mohammed Dewji Cup yakiwa na takriban miaka saba na yamekuwa na mafanikio makubwa kwa vijana wazaliwa wa Singida. "Kuhusiana na suala la ujenzi wa Uwanja wa Namfua, nilishaanza ukarabati katika eneo la jukwaa kuu, wananchi ni mashahidi... kama wanaufahamu uwanja ulivyokuwa mwanzo na wakati wa mashindano ya riadha kitaifa, nilikarabati eneo la kukimbilia wanariadha. "... Bado nitaendelea kukarabati kwa awamu mpaka tutakapoukamilisha. Ukumbuke ahadi hii haikuwa yangu peke yangu. Lakini nimeshanunua nyasi za bandia ambazo zimenigharimu sh. milioni 250... Natarajia kuziweka hizo nyasi mwaka 2012/2013," alisema Dewji.

President Kikwete adorns Police Officers in Dar es Salaam

The Commander in Chief, President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete adorns W.P Namsemba Amani Mwakatobe who graduated as Assistant Supertendent of Police Kurasini police staff college today .More than 200 police officers graduated with various ranks during the colorful ceremony .Flanking the President on the right, is the Inspector General of Police Said Mwema.(Photo by Freddy Maro).

Thursday, August 25, 2011

HIKI NDIYO KIJIJI KILICHOCHOMWA MOTO HUKO TABORA

Mkazi wa Kitongoji cha Luganjo Mtoni katika Tarafa ya Usinge mkoani Tabora, Bahati Hussein (kulia), akiwa amekaa na familia yake nje ya mabaki ya nyumba yake, baada ya kuchomwa moto na askari wa wanyamapori na polisi agosti 15 mwaka huu kwa madai ya kujenga katika hifadhi. Nyumba 317 zilichomwa na watu 773 hawana mahali pa kuishi wanaishi vichakani.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mgusa Maduhu (kulia) akiwa na familia yake baada ya nyumba yake kuchomwa moto.
Wakazi wa kijiji hicho wakiwaonesha mabaki ya baiskeli iliyoungua moto katika tukio hilo.
watoto wakicheza vichakani katika eneo la wazi walipopewa hifadhi na serikali ya kijiji.
Mama Mlemavu Magreth Jonas akilia wakati akihojiwa na waandishi wa habari hawapo pichani.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliochomewa nyumba zao.
Mama akipika nje baada ya nyumba yake kuchomwa moto huku watoto wake wakisubiri chakula kiive tayari kwa mlo wa mchana.
Mkazi wa kijiji hicho Elia Mrisho akionesha mafuvu ya nguruwe wake waliochomwa moto. Nguruwe 26 waliteketea.