(Na Veronica Kazimoto – MAELEZO)
DAR ES SALAAM
Mazungumzo bado yanaendelea kati ya Serikali na Muwekezaji aliyejitokeza kununua jengo la Mahakama ya Rufani iliyopo katika makutano ya barabara ya Kivukoni na Ohio jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Celina Kombani wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.
“Kuhusu suala la uuzwaji wa jengo la Mahakama ya Rufani, mazungumzo baina ya Serikali na muwekezaji aliyejitokeza bado yanaendelea hivyo basi napenda kuwatoa hofu waheshimiwa wabunge kuhusiana na suala hili,” amesema waziri Kombani.
Waziri Kombani amefafanua kuwa mazungumzo yanaendelea baina ya muwekezaji na ofisi mbalimbali za Serikali kama ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mahakama ya Rufani,Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Aidha, Waziri Kombani amesema muwekezaji aliyejitokeza ameahidi kujenga mahakama ya Rufani yenye hadhi kulingana na umuhimu waka kama mhimili mojawapo wa dola.
Kama muafaka utafikiwa kati ya muwekezaji na Serikali jengo hilo la Mahakama ya Rufani litajengwa maeneo ya mtaa wa Chimala mkabala na barabara ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikitoa taarifa kuhusiana na jengo la Mahakama ya Rufani kununuliwa na muwekezaji wa hoteli ya Kempinski na kuwa sehemu ya hoteli hiyo kwa ajili ya maegesho ya magari.
..............................................................................................................................................
Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP ni mmiliki halali wa jengo lenye hati namba 56998, Kiwanja namba 22/3/1 lililoko katika eneo la Mabibo Dar es Salaam
Mtandao wa Jinsia ulinunua jengo hilo kutoka kwa Mfilisi (Benki ya Rasilimali Tanzania- TIB) kwa Iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited ambayo ilikuwa sehemu ya kampuni tanzu ya Tanzania Textile Company Limited (TEXCO) kwa gharama ya shilingi milioni 200 ambapo makubaliano ya manunuzi yalifanyika tarehe 15/6/ 1997.
Mchakato wa uuzaji wa jengo hili ulikuwa wa wazi uliotangazwa katika vyombo vya habari nchini hususan magazeti.
Baadhi ya watumiaji wa ofisi waliokuwa ndani ya jengo hilo wakati TEXCO ikiwa inafilisiwa nao walishiriki katika mchakato wa kununua bila mafanikio. Baada ya TGNP kushinda ‘tender’, baadhi ya watumiaji hao , mnano mwezi wa Julai 1997 walifungua kesi namba 215 / 1997 dhidi ya TIB kama mshitakiwa wa kwanza na TGNP mshitakiwa wa pili katika mahakama kuu kupinga maamuzi ya TIB kuiuzia TGNP jengo hilo.
UAMUZI WA MAHAKAMA KUU
Kesi hii ilichukua muda mrefu sana takribani miaka kumi na mbili mpaka kufikia tarehe 15/10/ 2009,uamuzi wa Mahakama Kuu ulipotolewa. na Mheshimiwa Jaji T.B Mihayo wa mahakama kuu hukumu ambayo iliwapa haki TGNP na kuwaamuru walalamikaji kuondoka mara moja na kulipa gharama.
Wakati mchakato wa kutekeleza hukumu ya Mahakama Kuu ukiendelea, mnano tarehe 19/9/2009 walalamikaji walipeleka katika Mahakama ya Rufaa azimio la kusimamisha utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu ya kutowatoa kwenye jengo kwa kupitia ombi na 129 la 2009 ombi lao limetupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa tarehe 23 /8/2011.
MCHAKATO WA KUTEKELEZA UAMUZI WA MAHAKAMA
TGNP wamiliki halali wa hili jengo tunasubiri utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa iliyotolewa terehe 23/8/2011. Tutaendelea kuwataarifu maendeleo ya mchakato huu
No comments:
Post a Comment