Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura (wa pili kutoka kulia) akiwatambulisha baadhi ya wafanyakazi wa mfuko huo kwa waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (wa kwanza kulia) leo alipozitembelea ofisi za mfuko wa Vyombo vya Habari jijini Dar es salaam.
Mpiga picha kutoka Flame Tree Media Trust Bw. Mwanzo Millinga akimwonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi baadhi ya picha za matukio mbalimbali alizopiga katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kutoa habari kwa umma kutokana na ufadhili wa Mfuko wa vyombo vya Habari (TMF) leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi( wa kwanza kulia) akiwa na Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura(kushoto) pamoja na wafanyakazi wa mfuko huo na waandishi wa habari wakiangalia moja ya kipindi cha Nchi Yetu kilichoandaliwa kwa ufadhili wa TMF kumulika Haki za Binadamu na masuala mbalimbali ya kijamii.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya picha zilizopigwa mkoani Lindi leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akiongea na wafanyakazi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) leo alipotembelea ofisi hizo kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.Pamoja na mambo mengine kazi mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.Pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa mfuko huo kuhamasisha jamii kufanya kazi kwa bidii na kuibua masuala mbalimbali na fursa zilizopo nchini kwa maendeleo taifa.
MAKAMU WA RAIS KATIKA MAONYESHO YA NANENANE DODOMA.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwahotubia wakazi wa Dodoma leo wakati wa maadhimisho ya utekelezaji wa mwaka wa pili wa kauli ya kilimo kwanza kwenye maadhimisho ya wakulima nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali ( wa tatu kutoka kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Pampu za kumwagiliaji aina ya Money marker kwa mikoa ya Dodoma, Iringa na Ruvuma wa Kampuni ya Kick Start International Deus Shauri( wa pili kulia) jinsi pampu hizo zilivyo saidia kuinua kipato kwa baadhi ya wakulima wanaozitimika. Afisa huyo alitoa maelezo hayo kwa Makamu wa Rais leo mjini Dodoma alioptembea maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea.
Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia mkoani Dodoma Anna Makenge(kushoto) na Monica Haule(kulia)wakipata maelezo leo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-T) Margaret Mussai juu ya shughuli mbalimbali zinzosimamiwa na mfuko huo katika kuwaletea maendeleo Watanzania. Polisi hao walipata maelezo hayo jana mjini Dodoma wakati walioptembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima nane nane yanayoendelea.
Mmoja wa watumishi wa umma wastaafu ambaye alikuwa Afisa Kilimo Mwandamzi Elias Sabuni akimuuliza Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma(kushoto) juu hatua za uboreshaji wa stahili za wastaafu mbalimbali katika Wizara mbalimbali. Mstaafu huyo aliuza hayo leo mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya nane nane yanayoendelea m jinni Dodoma Kitaifa.
Afisa Mikopo Mwandamizi wa Benki ya Uwekezaji Tanzania(Tanzania Investment Bank-TIB) Adelitha Kibuya akimweleza Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali leo mjini Dodoma juu ya mikopo mbalimbali inayotolewa na Benki hiyo katika kusiadia uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wa wananchi. Afisa huyo alitoa maelezo hayo jana mjini Dodoma wakati Makamu wa Rais alipotembelea maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea Kitaifa mkoani hapa.
Afisa Elimu Mazingira Mkuu kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Martha Ngalowera akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali leo mjini Dodoma juu ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Ofisi hiyo katika kulielimisha jamii juu ya utunzaji mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho. Makamu wa Rais alitembelea maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea mjini Dodoma ili kujionea sshughuli mbalimbali zinazoendelea.
WATANZANIA WAHAMASISHWA KUPIGIA KURA MLIMA KILIMANJARO
BEATRICE MLYANSI NA ESTHER MUZE
MAELEZO
Watanzania wamehamasishwa kujitokeza kupigia kura Mlima Kilimanjaro ili uweze kushinda katika maajabu saba mapya ya dunia yatakayofanyika tarehe 11 Novemba 2011 Lisbon Ureno .
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dare es salaam Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Save Mt.Kilimanjaro Bw.Ernest Olotu amesema mlima Kilimanjaro ulipendekezwa kuingia kwenye mashindano ya maajabu saba mapya ya duniani . tarehe 7/7/2007.
Akielezea kuhusu mashindano hayo Bw. Olotu amesema shindano la Maajabu saba mapya ya duniani yalizinduliwa na shirika la New Open World Cooperation (NOWC) tarehe saba mwezi wa saba Lisbon Ureno ambapo kura zaidi ya milioni 100 zilipigwa kutafuta maajabu 28 mapya ya dunia.
Mwenyekiti huyo ameelezea kuwa vivutio 77 vilipendekezwa mwanzoni ambapo 28 vilipigiwa kura kuingia kwenye shindano hilo”,Afrika ikitoa nchi mbili Tanzania inayoshindanisha mlima Kilimanjaro pamoja na Afrika kusini inayoshindanisha Table Mountains.
Aidha Bw Olotu amesema Mlima Kilimanjaro una nafasi nzuri yakushinda kuingia katika maajabu hayo kama utapigiwa kura nyingi kutoka kwa watanzania.
“waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari mlioko hapa na wasiokuwepo hapa ni jukumu letu kuwahabarisha na kuwahamasisha Watanzania wote popote waliko bila kujali itikadi,dini ,rangi wala kabila kuonyesha uzalendo tushirikiane pamoja katika kupiga kura ili kuhakikisha Mlima Wetu unashinda”.alisema Bw.Olotu.
Amesema watu watakaotaka kupiga kura waingie kwenye tovuti ya http://www.smk.or.tz/ kupata maelezo ya kupiga kura au wanaweza kuingia moja kwa moja kwenye tovuti ya http://www.new7wonders.com/.
Sambamba na mtandao namba za simu zitakazotumika kupiga kura kimataifa kutokea nchini ni +2392201055,+18697605990,+16493398080 na +447589001290.
MSAJILI HANA UWEZO KUFUTA CHAMA CHA SIASA AMBACHO WABUNGE WAKE WANAFANYA FUJO BUNGENI
JOSEPH ISHENGOMANA MPOKI NGOLOKE
MAELEZO
Msajili wa vyama vya siasa amesema kuwa ofisi yake haina nguvu kisheria kifuta chama chochote cha siasa kutokana na wabunge wake kukosa heshima bungeni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo jinini Dar es Salaam Bwana John Tendwa amesema Bunge ni Mhimili mwingine wa serikali baada ya Mahakama na Utawala, na kuna kanuni lililojiwekea za kuwaongoza kufanyakazi.
Hivi karibuni kumekuwepo na vitendo vya vurugu bungeni, kuwasha vipaza sauti ovyo na kupiga kelele bila kuruhusiwa na Spika au Mwenyekiti wa Bunge. Hali hii imesababisha wabunge kadhaa kutolewa nje ya bunge kutokana na kukiuka kanuni.
“Wabunge wakiwa ndani ya bunge sio wangu, sina madaraka nao, lakini wakiwa nje ya kuta za bunge ni wangu. Ndani ya Bunge mikono na midomo yangu imefungwa kabisa, lakini kwa mtazamo wa wananchi wanajua kuwa mimi ninamamlaka ya kuwawajibisha kutokana na utovu wa nidhamu wanouonyesha bungeni, lakini sio,” amesema
“Mimi nimechukia sana kuona vitendo hivi kwasababu natupiwa lawama na watu kuwa wanaofanya vurugu bungeni ni watu wanaotoka katika vyama vyangu. Ninafurahi kwakuwa vyama vyangu nilivyovisajili viko ndani ya bunge, lakini sifurahishwi na utovu wa nidhamu wanaofanya”
Kwa mujibu wa Msajili wa vyama vya Siasa, baadhi ya wabunge vitendo wanavyofanya ndani ya Bunge kila anayesikia au kushuhdia vitendo hivyo, lazima asikitike.
“Taratibu na mamlaka ya kudhibiti utovu huo wa nidhamu uko ndani ya Bunge. Bunge ni taasisi inayojitegemea haiingiliwi na upande wowote (Mahakama na Utawala).
Baadaye mwezi huu, Msajili wa Vyama vya Siasa atakutana na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa katika baraza la vyama na kuwaelezea masikitiko yake.
“Tutakuwa katika baraza la vyama kabla ya bunge lijalo. Tutazungumzia hali hii na kutoa jibu,” amesema
Waziri Hamad Masuod Hamad akizindua kamati ya mabaharia
Waziri wa Wizara ya muindombinu na mawasiliano Hamad Masuod Hamad katika akisoma risala wakati wa uzinduzi wa kamati mbili ya usafiri wa anga na kamati ya mabaharia ambazo zitakuwa na jukumu la kusimamia uanzishwaji vyuo vya sehemu hizo na kulia ni ndugu Sururu ambaye ni meneja shirika la meli Zanzibar (Picha na Hamad Hija maelezo Zanzibar)
WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka Bungeni Mjini Dodoma Augost 3, 2011. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
Vyama vya UDP na NCCR Mageuzi vyashindwa kuwasilisha ripoti za gharama za uchaguzi
NA MPOKI NGOLOKE
MAELEZO
Vyama vya siasa 12 kati ya 18 vilivyosajiliwa nchini vimerejesha taarifa zao za matumizi ya fedha wakati wa uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba mwaka 2010.
Msajili wa Vyama vya siasa nchini Bwana John Tendwa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati alipoongea na waandishi wa habari na kuongeza kuwa vyama viwili vimeongezewa muda wa kukamilisha taarifa zake.
Bwana Tendwa amevitaja vyama vilivyowasilisha taarifa zake za matumizi ya fedha wakati wa uchaguzi mkuu kuwa ni UPDP,DP, NRA, UMD, APPT- Maendeleo, Chama Cha Mapinduzi, CUF na CHADEMA.
Vyama vingine ni AFP, TLP,NLD na SAU. “Vyama vya UMD na Chausta havikushiriki mahali popote katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana hivyo haviguswi na sheria hii,” amesema.
“Naomba nisitaje majina ya wagombea walioshindwa kuleta ripoti zao kwasababu wengine wanamatatizo ya msingi na bado tunayachambua, ila UDP na NCCR- Mageuzi wameshindwa kuwasilisha ripoti yao kwa muda na tumewapa muda wa wiki mbili kukamilisha taarifa yao,” amesema.
Kwa mujibu wa Sheria ya gharama za uchaguzi, endapo chama cha siasa kitashindwa kuwasilisha ripoti, kitapoteza sifa ya kushiriki uchaguzi mkuu utakaofuata na kulipa faini ya shilingi milioni tatu. Wakati mgombea wa chama chochote akishindwa kuwasilisha ripoti yake atalipa faini ya Tsh milioni mbili.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, wagombea wote walitakiwa kukamilisha ripotii hizo ndani ya siku 90 baada ya uchaguzi mkuu kumalizika, lakini Msajili aliwaongezea muda kwasababu ilikuwa mara ya kwanza sheria hiyo kutumika.
Bwana Tendwa amesema, “baada ya wiki mbili kuanzia sasa nitakabidhi ripoti hivi za vyama vya siasa kwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ili azifanyie kazi. CAG akimaliza kazi yake atawasilisha ripoti ya ukaguzi wake Bungeni na nakala nyingine ataipeleka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Jumla ya wagombea 10,000 walishiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 katika nafasi za urais, Ubunge na Udiwani.
Wakati huo huo Msajili wa Vyama vya Siasa amezungumzia uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora na kusema kuwa uchaguzi huo utakuwa mfano wa utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi na hakutakuwepo vitendo vyovyote vya rushwa vitakavyoruhusiwa katika uchaguzi huo.
“Rushwa katika uchaguzi Bye bye, hakutakuwa na rushwa Igunga. Igunga ni eneo dogo linalodhibitiwa. Sasa hivi Igunga kuna tatizo la njaa, tatizo hili lisitumiwe na wanasiasa vibaya kujipenyeza kwa wananchi na kutoa rushwa,” amesema na kuongeza kuwa kama mtu atataka kutoa msaada wa chakula apitie mamlaka husika ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa.
Ameeleza kuwa ofisi yake itashirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini TAKUKURU na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuelezea sheria ya gharama za uchaguzi kwa wananchi wa Igunga na Mkoa wa Tabora kwa ujumla ili watu wasijihusishe na vitendo vya kupokea na kutoa rushwa.
No comments:
Post a Comment