Wafanyakazi wakiserebuka mara katika hafla ha kutimiza mwaka mmoja tangia kuanzishwa kwa hoteli ya JB Belmont katika hafla iliyofanyika hotelini hapo juzi jioni jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wageni waalikwa kadhaa.
Wafanyakazi waliochaguliwa kuwa ni wafanyakazi bora wa hoteli JB Belmont wakiwa katika picha ya pamoja
WAMILIKI wa hoteli wa ukanda wa Afrika Mashariki wametakiwa kutoa kipaumbele katika kuajili i wafanyakazi katika nchi za ukanda huu ili kuongeza nafasi za ajira ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo.
Hayo yalisemwa juzi na balozi wa Uganda hapa nchini Ibrahim Mukiibi katika hotuba yake kwenye hafla ya kutimiza mwaka mmkoja kwa hoteli ya JB Belmont iliyokuwa ikijulikana kama Paradise City hotel.
Mukiibi alisema kuwa muda umefika kwa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki waliowekeza katika sekta hiyo kutambua na kuendeleza uwezo wa kazi kwa wafanyakazi wa nchi ambazo wamewekeza.
Alisema kuwa hakuna haja ya kuajili watu kutoka nje ya ukanda huu kuja kufanya kazi katika ukanda huu wakati wahusika wa nchi hizi za Afrika Mashariki wanaweza kufanya kazi wao wenyewe.
Katika hafla hiyo ambayo iliendana na utoaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora wa hoteli hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa Kitchen Hut, Quality Savanah ambazo zote zipo chini ya mmiliki mmoja.
“ Ni kwamba kama huyu mwekezaji kutoka nchini Uganda akiwaajili watanzania wengi basi atajikuta anakuwa anawawekeza mazingira mazuri ya maisha kwa watanzania wa hapa nchini” alisema Mukiibi.
Hoteli iliyokuwa ikiitwa Paradise City kwa sasa itakuwa ikifahamika kama JB Belmont kutokana na kubadilishwa kwa umiliki wake na kuwa chini ya uongozi mpya.
No comments:
Post a Comment