N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Thursday, August 4, 2011

WAZIRI WA HABARI DR. EMMANUEL NCHIMBI AZINDUA BODI MPYA YA MCT

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wajumbe wa Bodi mpya na ya zamani ya Baraza la Habari Tanzania(MCT), wakiwemo na wadau wengine wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jana jioni katika hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel (kulia) Nchimbi akimkabidhi cheti cha utendaji kazi mzuri katika kipindi cha bodi iliyopita Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji Robert Kisanga, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya uliofanyika jana jioni katika hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam.Jaji Kisanga amendelea pia kuwa Rais wa MCT.
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi wanne kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi mpya na ya zamani ya Baraza la Habari Tanzania(MCT), wakati wa uzinduzi wa bodi mpya uliofanyika jana jioni katika hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia) akimpongeza Mhariri wa gazeti la Nipashe Jumapili, Flora Fwingia kwa uhodari wake wa kuandika makala, ambaye pia alikuwa ni mjumbe wa Bodi ya zamani ya Baraza la Habari Tanzania(MCT), wakati wa uzinduzi wa bodi mpya uliofanyika jana jioni katika hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel (kulia) Nchimbi akimkabidhi vitendea kazi mjumbe wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bi. Badra Masoud kushoto na katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania(MCT),Kajubi Mukajanga. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jana jioni katika hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia) akifafanua jambo kwa Alex Mgongolwa ambaye alikuwa mjumbe wa Bodi ya ya zamani ya Baraza la Habari Tanzania(MCT), wakati wa uzinduzi wa bodi mpya uliofanyika jana jioni katika hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam.
Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars Jean Paulsen akizungumza na waandishi wa habari mchana huu katika ofisi za shirikisho la mpira wa miguu TFF, wakati alipotangaza kikosi cha timu hiyo kitakachopambana na Chard katika mchujo wa kushiriki kombe la Dunia. Timu hiyo inaingiaka kambini kesho katika hoteli ya Atriums iliyoko Sinza Afrika Sana jijini Dar es salaam. kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa kujipima nguvu Agosti 10 kutokana na kalenda ya FIFA hata hivyo timu ya taifa itacheza mchezo huo ugenini na itatangazwa baadae ni timu gani Taifa Stars itakutana nayo
Timu ya Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C Kanda ya Afrika ambalo lina timu za Cote d’Ivoire, Morocco na Gambia. Lakini kabla ya kuingia katika kundi hilo Stars italazimika kucheza raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Chad.
Stars ikifanikiwa kuitoa Chad baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zitakazochezwa kati ya Novemba 11-15 mwaka huu ndiyo itaingia katika kundi hilo la C. Pia mshindi wa kundi C ndiye atakayeingia katika raundi inayofuata kabla ya kupata tiketi ya kwenda Brazil, katika picha kushoto ni msemaji wa Shirikisho la pira wa miguu Tanzania TFF Boniface Wambura.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kocha wa timu ya taifa Taifa Stars wakati alipokuwa akitangaza kikosi chake kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu.
Na Tiganya Vincent, Dodoma _MAELEZO_Dodoma
Chuo cha Mipango cha Mjini Dodoma kinatarajia kufungua tawi jipya katika Mkoa wa Mwanza mapema mwezi ujao ili kuongeza udahili wa wanachuo waochukua Astashahaya ya Mipango vijijini.
Hatua hiyo inalenga kuzalisha wataalamu wengi watakaosaidia kuzalisha wataalamu wengi wa sekta ya mipango wataowezesha wananchi kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kuanzia ngazi ya kijjiji hadi Taifa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Afisa Masoko na Mahusiano wa Chuo cha Mipango cha Dodoma Godrick Ngoli wakati anaongea na waandishi wa habari mjini Dodoma kwenye Banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya wakulima ya nane kitaifa yanayofanyika mkoani hapa.
Alisema kuwa kimsingi masomo katika tawi la Mwanza yangeanza Mwezi wa Saba lakini kutokana na utaratibu wa uboreshaji wa miundombinu kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia wamelazimika kusogeza mbele hadi septemba mwaka huu ambapo ndio mwaka wa masoko kwa tawi hilo utakapoanza.
Ngoli alisema kuwa katika kuanzia wanatarajia kuchukua wanafaunzi 300 ambao watajiunga na kozi hikwa wale watakaofanikiwa kufaulu vizuri katika mitihani yao ya kila ngazi.
Aidha Afisa huyo alisema lengo la Chuo hicho ni kuanzisha astashahada mbalimbali zinazowiana na shaho la kuzalissha wataalamu waliobebea katika fani za mazingira na mipango ambayo ndio chachu ya kuwasaidia wakulima vijijini kupata mazao mengi.
Ngoli aliongeza kuwa bila kuwa na wataalamu waliobobea katika mipango mizuri ya utunzaji wa mazingira hatuwezi kuwa na kilimo kilichoendelevu.
Alisema kuwa Chuo hicho kimefanyia maboresho mitala yake ili kuhakikisha kuwa nchini kunakuwepo na wanasimia miradi ili kuifanya iwe endelevu badala ya kuwa ya muda mfupi.
Ngoli alisema kuwa mipango mizuri inayotokana na wataalamu walioelimika watasaidia kuharikisha mapinduzi ya kijani nchini.
Mke wa Rais wa Burundi Mama Denise Bucumi (kushoto) akiongea na waandishi wa habari katika Ofisi za Taasisi ya WAMA jijini Dar es Salaam August 3 baada ya kufanya mazugumzo na Mwenyeji wake mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia), Mke wa Rais wa Burundi amewasili August 3 2011 ambapo atakuwa na ziara ya siku sita nchini Picha na Mwanakombo Jumaa -MAELEZO,
Mke wa Rais Wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake nchini WAMA Mama Salma Kikwete(kulia) akifafanua jambo wakati alipoongea na waandishi wa habari August 3,2011 katika ofisi ya Taasisi yake jijini baada ya kumkaribisha mke wa Rais wa Burundi Mama Denise Bucumi Nkurunziza (kushoto) aliepo nchini kwa ziara ya siku sita, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) akimkabidhi vipeperushi vya Taasisi yake Mke wa Rais wa Burundi Mama Denise Bucumi (kushoto) alipotembelea katika Ofisi za Taasisi hiyo August 3,2011 jijini Dar es Salaam ambapo alifanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya wanawake na watoto pamoja na masuala mengine ya kijamii, Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Blog Archive