N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Saturday, March 8, 2014

KIZAZI KIPYA KUWASHA MOTO KWENYE TAMASHA LA MIAKA 50 YA MUUNGANO JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 8.3.2014

220px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Said Ali Mbarouk anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la muziki wa kizazi kipya na tenzi, linalotajiwa kufanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es salaam kesho.
Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya  maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar . Kauli mbiu za maadhimisho ya mwaka huu ni Utanzania wetu ni Muungano wetu tuulinde , tuuimarishe na kuudumisha.
Tamasha hilo ni sehemu ya shughuli mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika kuelekea kilele cha Miaka 50 ya Muungano tarehe 26.4.2014.
Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yataambatana na shughuli mbalimbali zitakazowashirikisha wananchi kupitia makangomano, michezo na burudani na kilele chake itakua tarehe 26 Aprili,2014.
 Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kongamano na utengamano wa kikanda wa Afrika Mashariki, kongamano la Bara la Afrika ,tamasha la muziki wa dansi na taarabu , maonyesho ya Idara na Wizara za Muungano na  mkesha utakaofanyika kuamkia siku ya Muungano.
Aidha maadhimisho haya ya miaka 50 ya Muungano yalizinduliwa Machi 1, 2014 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  kwenye ukumbi wa Salama katika hoteli ya Bwawani Mjini Unguja msisitizo ukiwekwa  kwa wananchi kuendelea kudumisha udugu, amani, umoja na mshikamano.

WAZIRI MKUU NA MATUKIO YA BUNGE LA KATIBA

PG4A1091Mwenyekiti wa Kamati ya  Kumshauri  Mwenyekiti kuhusu Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, Profesa Costa Mahalu (kulia) akiteta na wajumbe wa kamati hiyo Bungeni Mjini Dodoma baada ya Semina  ya Wabunge wa Bunge Maalum la  Katiba kuahirishwa Machi 7, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A1121 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mjumbe  wa Bunge Maalum la Katiba, James Mbatia kwenye ukumbi wa bunge Mjini Dodoma Machi 7,2014. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Blog Archive