N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Friday, August 26, 2011

WACHEZAJI TAIFA STARS WAITWA KUIVAA ALGERIA, VICTOR COSTA "NYUMBA" YUMO

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo (Agosti 25 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo dhidi ya Algeria ‘Desert Warriors’ kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon.
Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba). Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).
Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Juma Seif (Yanga) na Jabir Aziz (Azam). Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Salum Machaku (Simba).
Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Ramadhan Chombo (Azam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) na John Bocco (Azam).
Timu itaingia kambini Jumapili (Agosti 28 mwaka huu) mchana na jioni itaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Mechi dhidi ya Algeria itachezwa Septemba 3 mwaka huu kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI DODOMA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu Maswali Bungeni, katika kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu leo Augost 25, 2011. kila siku ya alhamisi ya wiki waziri mkuu huulizwa maswali ya ana kwa ana na wa wabunge.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Watoto wa Mbunge wa Viti Maalum, Angellah Kairuki, Ester (kushoto) na Kemilembe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Augost 25, 2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Watendaji waSerikali za Vijiji na Viongozi wa CCM wa jimbo la Magu kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Augost 25, 2011.. Kushoto ni MBunge wao, Dr . Dr Festus Limbu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara,Dr. Cyril Chami kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Augost 25, 2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Kibakwe , George Simbachawene kwenye viwanja vya BungeMjini Dodoma Augost 25, 2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Kamishina wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Bw. T. Alexander Aleinikoff, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Augost 25, 2011.
Mbunge wa Viti Maalum, Dianna Chilolo akimuuliza swali Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kipindi cha maswali Bungeni Augost 25, 2011. (Picha Zote na OFisi ya Waziri Mkuu)

MAZUNGUMZO YANAENDELEA JUU YA UUZWAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI.

(Na Veronica Kazimoto – MAELEZO)
DAR ES SALAAM
Mazungumzo bado yanaendelea kati ya Serikali na Muwekezaji aliyejitokeza kununua jengo la Mahakama ya Rufani iliyopo katika makutano ya barabara ya Kivukoni na Ohio jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Celina Kombani wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.
“Kuhusu suala la uuzwaji wa jengo la Mahakama ya Rufani, mazungumzo baina ya Serikali na muwekezaji aliyejitokeza bado yanaendelea hivyo basi napenda kuwatoa hofu waheshimiwa wabunge kuhusiana na suala hili,” amesema waziri Kombani.
Waziri Kombani amefafanua kuwa mazungumzo yanaendelea baina ya muwekezaji na ofisi mbalimbali za Serikali kama ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mahakama ya Rufani,Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Aidha, Waziri Kombani amesema muwekezaji aliyejitokeza ameahidi kujenga mahakama ya Rufani yenye hadhi kulingana na umuhimu waka kama mhimili mojawapo wa dola.
Kama muafaka utafikiwa kati ya muwekezaji na Serikali jengo hilo la Mahakama ya Rufani litajengwa maeneo ya mtaa wa Chimala mkabala na barabara ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikitoa taarifa kuhusiana na jengo la Mahakama ya Rufani kununuliwa na muwekezaji wa hoteli ya Kempinski na kuwa sehemu ya hoteli hiyo kwa ajili ya maegesho ya magari.
 ..............................................................................................................................................

Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP ni mmiliki halali wa jengo lenye hati namba 56998, Kiwanja namba 22/3/1 lililoko katika eneo la Mabibo Dar es Salaam
Mtandao wa Jinsia ulinunua jengo hilo kutoka kwa Mfilisi (Benki ya Rasilimali Tanzania- TIB) kwa Iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited ambayo ilikuwa sehemu ya kampuni tanzu ya Tanzania Textile Company Limited (TEXCO) kwa gharama ya shilingi milioni 200 ambapo makubaliano ya manunuzi yalifanyika tarehe 15/6/ 1997.
Mchakato wa uuzaji wa jengo hili ulikuwa wa wazi uliotangazwa katika vyombo vya habari nchini hususan magazeti.
Baadhi ya watumiaji wa ofisi waliokuwa ndani ya jengo hilo wakati TEXCO ikiwa inafilisiwa nao walishiriki katika mchakato wa kununua bila mafanikio. Baada ya TGNP kushinda ‘tender’, baadhi ya watumiaji hao , mnano mwezi wa Julai 1997 walifungua kesi namba 215 / 1997 dhidi ya TIB kama mshitakiwa wa kwanza na TGNP mshitakiwa wa pili katika mahakama kuu kupinga maamuzi ya TIB kuiuzia TGNP jengo hilo.
UAMUZI WA MAHAKAMA KUU
Kesi hii ilichukua muda mrefu sana takribani miaka kumi na mbili mpaka kufikia tarehe 15/10/ 2009,uamuzi wa Mahakama Kuu ulipotolewa. na Mheshimiwa Jaji T.B Mihayo wa mahakama kuu hukumu ambayo iliwapa haki TGNP na kuwaamuru walalamikaji kuondoka mara moja na kulipa gharama.
Wakati mchakato wa kutekeleza hukumu ya Mahakama Kuu ukiendelea, mnano tarehe 19/9/2009 walalamikaji walipeleka katika Mahakama ya Rufaa azimio la kusimamisha utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu ya kutowatoa kwenye jengo kwa kupitia ombi na 129 la 2009 ombi lao limetupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa tarehe 23 /8/2011.
MCHAKATO WA KUTEKELEZA UAMUZI WA MAHAKAMA
TGNP wamiliki halali wa hili jengo tunasubiri utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa iliyotolewa terehe 23/8/2011. Tutaendelea kuwataarifu maendeleo ya mchakato huu


Dewji: Mangumbaru wa siasa wananichafua, Apeleka Singida mradi wa maji wa bil 20/-


Na Mwandishi Wetu 
MBUNGE wa Singida Mjini, Mohammed Dewji amesema mangumbaru (watu wenye machachari, matata na fujo) wa siasa wanamchafua, kwa lengo la kuchukua kiti chake cha ubunge. Dewji, maarufu kwa jina la Mo, ametoa kauli hiyo wakati akifanua juu ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya watu waliodai ni wakazi wa Singida, waliodai eti kwamba hajafanya chochote cha maendeleo katika jimbo lake tangu achaguliwe kuwa mbunge. Tuhuma na malalamiko hayo yaliyotolewa na baadhi ya watu waliodai ni wananchi wa Singida kupitia mtandao wa Facebook, wakati wa kubadilishana mawazo na mbunge huyo. Pia Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) aliwataka wana-Singida kuungana na Watanzania wengine kufanya maandamano kudai ahadi ya maisha bora kwa wote kama ilivyoahidiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoko madarakani. Lema akiwa na wabunge wenzake, Chiku Abwao na Regia Mtema (Chadema - Viti Maalumu), alisema hayo wiki hii mjini Singida kwenye mkutano wa hadhara, huku akidai umefika wakati kwa wananchi wa Mkoa wa Singida ambao ni ngome ya CCM, kukiondoa chama hicho madarakani. Katika michango yao kwenye Facebook, wananchi hao walioruhusiwa kutoa maoni na dukuduku zao kwa Dewji, walidai kutoona maendeleo yoyote katika jimbo hilo kwa madai kwamba wananchi wa Singida wamekuwa wakiteseka na maisha kwa kukosa maji, ajira na masuala ya maendeleo. Katika ufafanuzi wake kuhusu malalamiko hayo, Dewji alisema tangu kuchaguliwa kwake amekuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwenye maeneo ya kero za maji. Dewji alisema amefanikisha uchimbaji wa visima virefu zaidi ya 21 kwenye kata za Unyambwa, Mungu Maji, Unyamikumbi, Mwankoko, Mtamaa, Mandewa na Mtipa pamoja na baadhi ya kata za Mjini kama Kindai, Mitunduruni na Utemini. Dewji pia aliongeza kuwa bado anaendelea na jitihada za kukabiliana na tatizo hilo kwa kuibana Serikali itekeleze mradi mkubwa wa Benki ya Dunia wa kuchimba visima 10 jimboni na anaendelea kuibana Serikali ifanye haraka kumalizia mradi mkubwa mwingine wa maji unaofadhiliwa na Benki ya BADEA na OPEC. "Mradi huo ukikamilika ndio utakuwa ufumbuzi wa tatizo la maji Manispaa ya Singida... Mradi huu utabadilisha miundombinu yote ya maji safi ndani ya manispaa yetu. Unatarajia kukamilika mwaka 2013 na utagharimu takriban sh. bilioni 20," alisema Dewji. Kuhusu ajira, Dewji alieleza kuwa amekuwa mstari wa mbele kutoa Ajira kwa vijana kupitia kampuni yake ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL) sambamba na kampuni nyingine mbalimbali. Alifafanua zaidi kuwa yuko mbioni kuwekeza katika jimbo lake kwa kufungua kiwanda kitakachotoa fursa zaidi kwa vijana na wakazi wa Singida kujipatia maendeleo na ajira, na kwamba kwa sasa anaendelea kuwasiliana na wataalamu mbalimbali wa uwekezaji ili kuona kama kuna fursa za kuwekeza katika manispaa ya hiyo. Alipongeza kupokelewa kwa mwito wa kuhamasisha michezo katika jimbo lake na kusisitiza kuwa ataendelea kunyanyua na kuibua vipaji kupitia mashindano yake yajulikanayo kama Mohammed Dewji Cup yakiwa na takriban miaka saba na yamekuwa na mafanikio makubwa kwa vijana wazaliwa wa Singida. "Kuhusiana na suala la ujenzi wa Uwanja wa Namfua, nilishaanza ukarabati katika eneo la jukwaa kuu, wananchi ni mashahidi... kama wanaufahamu uwanja ulivyokuwa mwanzo na wakati wa mashindano ya riadha kitaifa, nilikarabati eneo la kukimbilia wanariadha. "... Bado nitaendelea kukarabati kwa awamu mpaka tutakapoukamilisha. Ukumbuke ahadi hii haikuwa yangu peke yangu. Lakini nimeshanunua nyasi za bandia ambazo zimenigharimu sh. milioni 250... Natarajia kuziweka hizo nyasi mwaka 2012/2013," alisema Dewji.

President Kikwete adorns Police Officers in Dar es Salaam

The Commander in Chief, President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete adorns W.P Namsemba Amani Mwakatobe who graduated as Assistant Supertendent of Police Kurasini police staff college today .More than 200 police officers graduated with various ranks during the colorful ceremony .Flanking the President on the right, is the Inspector General of Police Said Mwema.(Photo by Freddy Maro).

Thursday, August 25, 2011

HIKI NDIYO KIJIJI KILICHOCHOMWA MOTO HUKO TABORA

Mkazi wa Kitongoji cha Luganjo Mtoni katika Tarafa ya Usinge mkoani Tabora, Bahati Hussein (kulia), akiwa amekaa na familia yake nje ya mabaki ya nyumba yake, baada ya kuchomwa moto na askari wa wanyamapori na polisi agosti 15 mwaka huu kwa madai ya kujenga katika hifadhi. Nyumba 317 zilichomwa na watu 773 hawana mahali pa kuishi wanaishi vichakani.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mgusa Maduhu (kulia) akiwa na familia yake baada ya nyumba yake kuchomwa moto.
Wakazi wa kijiji hicho wakiwaonesha mabaki ya baiskeli iliyoungua moto katika tukio hilo.
watoto wakicheza vichakani katika eneo la wazi walipopewa hifadhi na serikali ya kijiji.
Mama Mlemavu Magreth Jonas akilia wakati akihojiwa na waandishi wa habari hawapo pichani.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliochomewa nyumba zao.
Mama akipika nje baada ya nyumba yake kuchomwa moto huku watoto wake wakisubiri chakula kiive tayari kwa mlo wa mchana.
Mkazi wa kijiji hicho Elia Mrisho akionesha mafuvu ya nguruwe wake waliochomwa moto. Nguruwe 26 waliteketea.

Wednesday, August 17, 2011

Ziara ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania Ngorongoro

Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiangalia wanyama wakati warembo hao 30 walipotembelea Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro juzi kujionea maajabu mbalimbalimbali yaliyomo katika hifadhi hiyo. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo. 
Warembo wanaoshiriki la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakimpa ndizi mlemavu, Melkiori Mamasita, anae Hudumiwa katika Kituo cha Huduma ya Walemavu Monduli juzi. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo na kufanya shughuli za kijamii. 
Warembo wanaoshiriki la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakikabidhi msaada wa chakula kwa mlemavu, Nanyakwa Olumindi, anae Hudumiwa katika Kituo cha Huduma ya Walemavu Monduli juzi. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo na kufanya shughuli za kijamii. 
Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufika katika lango kuu la kuingilia hifadhi ya Bonde la Ngorongoro juzi. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo. 
Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Erikisongo iliyopo Wilayani Monduli juzi. 
Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakicheza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Wasichana ya Enyorrate E.Ngai inayoendeshwa na Masista iliyopo Monduli Juu mkoani Arusha juzi. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipiga picha katika kibao cha Shule ya Wasichana Maasae iliyopo Wilayani Monduli baada ya kutembelea shule hiyo juzi. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo. 

Mafunzo ya sensa-morogoro yalivyokuwa katika picha

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Amina Mrisho (kulia) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) juzi mjini Morogoro wakati wa mafunzo ya wiki moja ya uendeshaji wa sensa ya majaribio itakayoanza Septemba 4 mwaka huu.
Picha na Tiganya Vincent, MOROGORO.
Baadhi ya wakufunzi wa mafunzo ya Sensa ya majaribio wakifanya mazoezi kwa vitendo katika mitaa ya Kata ya Mji Mpya mjini Morogoro juzi ikiwa ni sehemu ya mafunzo kabla ya kuanza sensa hiyo litakaloanza Septemba 4 mwaka huu katika mikoa 11 ya Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa akitoa ufafanuzi juzi mjini Morogoro wakati wa mafunzo ya wiki moja ya wakufunzi wa Sensa ya majaribio inayotarajia kuanza Septemba 4 mwaka huu katika mikoa 11.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Augost17,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS MAHUSINO NA URATIBU STEPHEN WASSIRA (KULIA) AKIMPONGEZA MBUNGE WA VITI MAALUM REGIA MTEMA (KUSHOTO)KWA KITENDO CHA KUWA UKOMAVU WA KISIASA MARA BAADA YA KUOMBA RADHI BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA .NA KWA WATANZANIA KUTOKANA NA KAULI YAKE ISIYORIDHISHA ALIYOITOA JUZI BUNGENI KUWA WATU WASIOKUWA WAZAWA WA MKOA WA MOROGORO. KATWAONDOKE KATIKA MKOA HUO. KATIKATI NI WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, EZEKIEL MAIGE.
PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, EZEKIEL MAIGE AKIWASILISHA BUNGENI HOTUBA YAKE YA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2011/2012 MJINI DODOMA LEO(JANA).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto wanaotoka katika jimbo la Bumbuli, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Augost 17,2011. Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Mizengo PInda akisalimiana na Makatibu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) wa kata za mkoa wa Mtwara kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Augost 17,2011. Kushoto kwake ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoa wa Mtwara, Anastazia Wambura. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais wa Zanzibar azungumza na uongozi wa Wiazara ya habari

Rais wa Zabziar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,katika mkutano uliojadili mambo ya utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo ambayo yataweza kukuza uchumi wetu na kuwaletea maendeleo wananchi,(kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi.

Tuesday, August 16, 2011

Vodacom Miss Tanzania watembelea kaburi la Hayati Edward Moringe Sokoine


Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa wamevalia vazi maalum livaliwalo na wanawake wa jamii ya Kimasaai wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao baada ya kukaribishwa katika mji wa Monduli jana katika tafrija iliyoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine na dada wa Mbunge wa Monduli Kalaine Lowasa.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine akimshika mkono mmoja wa washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania baada ya kuvishwa mgolole wa kimasai na dada wa Mbunge wa Monduli, Kalaine Lowasa (wapili kushoto) jana baada ya kuwasili Monduli. Kushoto ni Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga.
Blessing Ngowi, Mshiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, akiwa amejivisha nyoka shingoni huku wenzake wakimwangalia wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.

Na Mwandishi Wetu
Ziara ya mafunzo ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 imeendelea Mikoa ya kanda ya Kaskazini na warembo hao wamepata fursa ya kutembelea kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine.
Wakiwa eneo la Monduli warembo hao walipokelewa na Mtoto wa Sokoine Namelok Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Arusha.
Mbunge huyo alipata fursa ya kuwapa historia fupi ya maisha ya baba yake hasa alipokuwa Waziri Mkuu,mapema walipowasili wilaya ya monduli walipokelewa na mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowasa na viongozi wengine wa wilaya hiyo,Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalum wa mkoa wa Arusha Namelok Sokoine na alipata fursa ya kuwaasa warembo hao pamoja na ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii na maeneo ya kihistoria watumie fursa hiyo kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike hasa jamii ya kimasai,alisema jamii ya kimasai ambayo inajishughulisha na ufugaji haijatoa kipaumbele katika kumsomesha motto wa kike hivyo ziara ya warembo hao inaweza kutumika kubadilisha mtizamo huo.
Akizungumzia ziara hiyo Meneja Uhusiano na Habari kwa Njia ya Mtandao wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu alisema washiriki hao walijifunza vitu mbalimbali alivyovifanya Hayati Sokoine enzi za uhai wake.
Mara baada ya kutoka katika eneo hilo warembo hao 30 pia walitembelea shule ya Maasai Girls iliyopo Monduli kabla ya kupata chakula cha jioni.
“Ziara yetu bado inaendelea na warembo wanaendelea kujifunza kupitia elimu inayotolewa na wataalam mbalimbali wanaopata fursa ya kukutana na warembo wetu. Ni matumaini yetu wataitumia elimu hii kulitangaza taifa katika medani za kimataifa,” alisema Nkurlu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ndio waandaaji wa Vodacom Miss Tanzania Hashim Lundenga alisema warembo hao pia watatembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro NCAA, ili kujionea moja ya maajabu saba ya dunia.
Akifafanua Lundenga amesema mwaka huu wanataka warembo wenye sifa ikiwemo elimu, muonekanao na tabia nzuri ili mshindi atakayepatikana aweze kutuwakilisha vema katika medani za kimataifa hususani kujua vivutio vya kitalii vilivyopo nchini.
“Baada ya kutoka Mikumi ziara hii ya mafunzo sasa imeingia kanda ya kaskazini, tukiwa safarini kutokea Morogoro warembo walipata fursa ya kupiga picha katika maeneo mbalimbali ikiwemo daraja la mto wami na mji maarufu wa Moshi mkoani Kilimanjaro,” alisema Lundenga.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wengine mrembo Jennifer Kakolaki alisema kuwa wanaifurahia ziara hiyo kwani mbali ya kujionea rasirimali tofauti zilizopo nchini wanajifunza mengi kuhusiana na utalii wa ndani.
“Kiujumla Watanzania hawana budi kutenga siku maalum katika mwaka ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini. Binafsi nimepanua kiwango changu cha ufahamu kuhusiana na utajiri wa rasilimali za taifa zilizopo nchini,” alisema Jennifer.
Mwaka huu warembo hao wameingia kambini kwa mfumo tofauti na uliozoeleka kwani wamewekwa kwenye jumba maalum la ‘Vodacom House’ ambapo matukio yao yatakuwa yakioneshwa kupitia Startv na Clouds TV na watazamaji watapata fursa ya kupiga kura kuchagua mrembo watakayemuona anafaa.

SMZ YAKEMEA VITENDO VIOVU MWEZI WA RAMADHAN


Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais Muhammed Abuod akitoa taarifa maalum ya serikali kwa vyombo vya habari na Umma juu ya vitendo viovu vinavyofanywa na wananchi na hasa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani picha na Hamad Hija maelezo Zanzibar.

Hoteli JB Belmont yapata wafanyakazi wake bora



Wafanyakazi wakiserebuka mara katika hafla ha kutimiza mwaka mmoja tangia kuanzishwa kwa hoteli ya JB Belmont katika hafla iliyofanyika hotelini hapo juzi jioni jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wageni waalikwa kadhaa.
Meneja rasilimali watu (HR) wa hoteli ya JB Belmont akiwa amepozi mbele ya banner ya hoteli hiyo.
Wafanyakazi waliochaguliwa kuwa ni wafanyakazi bora wa hoteli JB Belmont wakiwa katika picha ya pamoja
WAMILIKI wa hoteli wa ukanda wa Afrika Mashariki wametakiwa kutoa kipaumbele katika kuajili i wafanyakazi katika nchi za ukanda huu ili kuongeza nafasi za ajira ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo.
Hayo yalisemwa juzi na balozi wa Uganda hapa nchini Ibrahim Mukiibi katika hotuba yake kwenye hafla ya kutimiza mwaka mmkoja kwa hoteli ya JB Belmont iliyokuwa ikijulikana kama Paradise City hotel.
Mukiibi alisema kuwa muda umefika kwa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki waliowekeza katika sekta hiyo kutambua na kuendeleza uwezo wa kazi kwa wafanyakazi wa nchi ambazo wamewekeza.
Alisema kuwa hakuna haja ya kuajili watu kutoka nje ya ukanda huu kuja kufanya kazi katika ukanda huu wakati wahusika wa nchi hizi za Afrika Mashariki wanaweza kufanya kazi wao wenyewe.
Katika hafla hiyo ambayo iliendana na utoaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora wa hoteli hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa Kitchen Hut, Quality Savanah ambazo zote zipo chini ya mmiliki mmoja.
“ Ni kwamba kama huyu mwekezaji kutoka nchini Uganda akiwaajili watanzania wengi basi atajikuta anakuwa anawawekeza mazingira mazuri ya maisha kwa watanzania wa hapa nchini” alisema Mukiibi.
Hoteli iliyokuwa ikiitwa Paradise City kwa sasa itakuwa ikifahamika kama JB Belmont kutokana na kubadilishwa kwa umiliki wake na kuwa chini ya uongozi mpya.

Friday, August 12, 2011

WANAFUNZI ARUSHA WANUFAIKA NA TIGO

Watoto wakibeba vibao waliopewa na kampuni ya Tigo wakati wa ghafla yakugawa jana Arusha
Lydia Sakaya, msamizi wa mauzo wa Tigo akikgawa vibao kwa watoto wakiwa darasani shule ya msingi ya Themi, Arusha.

Lydia akiwakabdhi vibao vyakuandikia kwa waalimu bw. Zebedario Mollel wa shule ya msingi wa Themi na Bi. Eusebio Matamwa mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi ya Uhuru.

Lydia Sakaya akisimama pamoja na waalimu wa shule za msingi Themi na Uhuru za Arusha baada ya kukabishiwa vibao vyakuandikia

Blog Archive