Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi wa masuala
Kisheria kwa waandishi wa habari kuhusu mchakato wa upatikanaji wa
katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akiwaonesha waandishi wa habari
Rasimu ya katiba wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya
kisheria katika mchakato wa Katiba wakati wa mkutano uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam
Baadhi ya
waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji
Frederick Werema wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Na Rose Masaka-MAELEZO
Viongozi
wa vyama vya siasa waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba wameaswa
kurejea bungeni ili kufanya maridhiano ndani ya bunge hilo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Jaji
Werema amesema kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi
kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza Rais kulivunja bunge hilo kwani
hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza bunge hilo.
“Sheria
inasema kuwa baada ya bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba
kupatikana, kinyume na hapo bunge husitishwa kufikia maridhiano na
kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia.” alisema Jaji Werema.
Pia
Jaji Werema alisema kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi
kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kuweza
kupata katiba iliyo bora kwa nchi na watu wake.
Aidha,
Jaji Werema aliviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili
muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji wa
taarifa na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza kusaidia
nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.
No comments:
Post a Comment