N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Saturday, August 23, 2014

WAZIRI MKUU PINDA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA JAJI MAKAME

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Jaji Leila Makame Mgonya mmoja wa wana familia, wa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Marehemu Jaji Lewis Makame baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu huyo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimian na Mawaziri Wakuu, Wastaafu, Frederick Sumaye na Jaji Joseph Warioba (wapili kulia) kabla ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na kutoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. Kulia nI jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na jaji Mkuu Mohamed Chande Othman (kulia) na Mawaziri Wakuu Wastaafu, Joseph Warioba (wapili kulia) na Frederick Sumaye kabla ya kutoa salamu za Serikali na heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Marehemu Jaji Lewis Makame baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Blog Archive