Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani Bw. Meng Wang (kulia) akimkabidhi
kinyago cha tembo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen
Masele wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani
lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu
Nyerere.
Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani Bw. Meng Wang (kulia) akimkabidhi
zawadi ya Kipepeo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen
Masele wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani
lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu
Nyerere.
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele
(aliyesimama kulia) akimkabidhi ramani ya Afrika iliyochongwa kwa mti Rais wa
Wajiolojia Afrika Profesa Aberra Mogessie wakati wa kufunga Kongamano la Tatu
la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi
wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele
(kulia) akimkabidhi zawadi Kijana Mwanasayansi Duniani toka nchini India wakati
wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini
Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele
(kushoto) akimkabidhi zawadi Kijana Mwanasayansi Duniani toka nchini Botswana
wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika
Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele
(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Vijana Wanasayansi Duniani
wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika
Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Wa kwanza
kulia ni Makamu Mwenyekiti na Mwakilishi wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES) na
anaemfuatia ni Rais wa YES Bw. Meng Wang. Wa kwanza toka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma
akifuatiwa na Rais wa Wajiolojia Afrika Profesa Aberra Mogessie.PICHA ZOTE NA BENEDICT
LIWENGA-MAELEZO.
Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani Bw. Meng Wang akitoa maelezo
machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga Kongamano la
Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika
Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa
Abdulkarim Mruma akitoa nasaha zake mbele ya Vijana Wanasayansi Duniani (hawapo
pichani) wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la
Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele
akiwahutubia Vijana Wanasayansi Duniani wakati alipokuwa akifunga Kongamano la
Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika
Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Meza Kuu ambapo katikati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na
Madini, Mhe. Stephen Masele, kulia ni Rais wa Vijana Wanasayansi Duniania Bw. Meng
Wang na kushoto ni Rais wa Wajiolojia Afrika Profesa Aberra Mogessie.
Baadhi ya Vijana Wanasayansi Duniani waliohudhuria siku ya ufungaji
Kongamano wakifuatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni rasmi wakati wa
kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini
Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani
(YES), Bi. Elyvin Nkhonjera kutoka nchini Malawi akikaribisha wageni waalikwa
wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika
Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
NAIBU WAZIRI MASELE AWATAKA VIJANA KUJIKITA KATIKA MAMBO YA SAYANSI NA
TEKNOLOJIA.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
14/08/2014.
NAIBU
Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele amewataka vijana nchini kupenda kujikita
katika masomo ya sayansi na teknolojia kama mihimili yenye kuleta maendeleo kwa
haraka ulimwenguni ili waweze kupata ujuzi na mitazamo katika sekta ya gesi
ambayo inakuwa kwa kasi kubwa nchini.
Mhe.
Masele ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akifunga Kongamano la Tatu la Vijana
Wanasayansi Duniani lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius
Kambarage Nyerere, kongamano ambalo liliwakutanisha vijana toka nchi zaidi ya
46 ulimwenguni zikiwemo baadhi ya nchi za Afrika ambapo Tanzania ilikuwa
mwenyeji wa Kongamano hilo.
Mhe.
Masele ameeleza kuwa sayansi na teknolojia ndiyo mihimili mikubwa ya sasa
katika kuleta maendeleo ya haraka katika nyanja mbalimbali kwani mambo mengi hivi
sasa hutegemea sayansi na teknolojia.
Aidha,
Mhe. Masele amezitaja baadhi ya changamoto zinazozikabili baadhi ya nchi za
Afrika katika kupata maendeleo ni pamoja na kutowekeza katika sayansi na
teknolojia hali inayopelekea baadhi ya nchi nyingi kukosa wataalam wa kutosha
katika mambo ya sayansi na teknolojia, hivyo amezitaka nchi za Afrika kuwekeza
katika sayansi ili kuweza ili kubadilisha uchumi wa Afrika.
“Sayansi
na teknolojia huleta maendeleo makubwa hivyo nawapa moyo vijana muendelee
kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika mambo ya sayansi na teknolojia ili
muweze kuleta uchumui endelevu”. Alisema Masele.
Akizungumzia
kwa upande wa Serikali ya Tanzania, Mhe. Masele amesema kuwa serikali ya
Tanzania imewekeza nguvu zake kwa sasa katika kuendeleza sayansi ya afya kwa
kuanzisha Vyuo mbalimbali na kuwasomesha watanzania nchi mbalimbali za nje ili
waweze kwenda kupata ujuzi na kuwa wataalam na wakaguzi katika sekta ya gesi
pamoja na mafuta kwa lengo la kuja kuisaidia nchi yao.
“Wajibu
wetu kama Serikali tumeamua kwa makusudi kusomesha vijana katika nchi
mbalimbali ili wakaweze kupata elimu juu ya sayansi na teknolojia hasa katika
masuala ya gesi ili kupata wataalam na wakaguzi wa kutosha nchini ambao
watalisaidia taifa kuinua uchumi wake na hivi sasa serikali imeanzisha vyuo
mbalimbali nchini, program mbalimbali za mafunzo kwa watanzania, imetoa
ufadhili wa masomo kwa watanzania na imedhamini makongamano ya vijana ili
wapate fursa ya kujiendeleza.” Alisisitiza Masele.
Mhe.
Masele amempongeza Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kwa
kazi kubwa anayoifanya katika Wizara yake na pia amewapongeza vijana
waliohudhuria katika kongamano hilo pamoja kuyapongeza Makampuni wadhamini wa
kongamano hilo na kuyataka makampuni hayo kuendelea kuwekeza pamoja na kulipa
kodi ili serikali iweze kukusanya mapato na wananchi wapate kunufaika na mapato
hayo.
Naye
Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES) Bw. Meng Wang amemshukuru Makamu wa
Rais wa Tanzania, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Naibu Waziri steven
Masele kwa kuwaunga mkono vijana waliohudhuria kongamano hilo na kuonesha hali
nzuri ya ushirikiano baina ya serikali na vijana na amewaasa vijana kujikita
katika sayansi na teknolojia kama mihimili mikuu ya maendeleo duniani.
“Naishukuru
sana Tanzania pamoja na ujio wa Mawaziri wake katika kufanikisha kongamano hili
la vijana wanasayansi, nawashukuru pia wadhamini wa makampuni mbalimbali wa
kongamano hili pamoja na vijana kwa ujumla toka nchi mbalimbali duniani”.
Alisema Wang.
No comments:
Post a Comment