Muungano mmoja wa wanamgambo nchini Libya unasema kuwa umeuteka
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli baada ya mapigano makali kati
yake na kundi pinzani la waasi.
Picha zilizowekwa katika mtandao zimeonyesha wapiganaji hao
wakisherehekea juu ya ndege na katika majengo ya uwanja huo.Muungano huo
unaoshirikishawanamgambo wa kiislamu pamoja na wanamgambo kutoka mji wa
Misrata umesema kuwa uliuteka uwanja huo licha ya mashambulizi ya
angani yanayodaiwa kutekelezwa na Misri pamoja na nchi za ufalme wa
kiarabu.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli anasema kuwa kuna ripoti za kuendelea
kwa vita kati ya makundi pinzani viungani mwa mji huo.Uwanja huo
umefungwa kwa takriban mwezi mmoja sasa kufuatia vita kati ya makundi
pinzani ya wanamgambo yaliozuka tangu kuondolewa madarakani kwa
aliyekuwa rais wa taifa hilo kanali Gaddafi mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment