Katibu
wa CCM Mkoa wa Singida Naomi Kapambala akizungumza na waanndishi wa
habari juu ya ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
Na Hillary Shoo, Singida.
Mbunge
wa Jimbo la Singida mjini (CCM), Mohammed Dewji ameulalamikia uongozi
wa Chama chake Mkoa wa Singida kwa kitendo cha kuchelewesha mchakato wa
kumalizia ujenzi wa Uwanja wa michezo Namfua ikiwa ni moja ya ahadi
zake alizotoa kwa wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Kuchelewa
huko kuanza kwa mchakato wa ukarabati na uwekaji wa nyasi za bandia
kwenye uwanja huo imeelezwa ni kutokana na urasimu na maslahi binafsi
miongozi mwa viongozi wa CCM Mkoa wa Singida.
Katika
barua yake ya Julai 31 mwaka huu kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana, Dewji amedai kuwa kwa kiasi kikubwa ameweza kutekeleza Ilani ya
Uchaguzi kwa vipindi vyote viwili pamoja na ahadi zake binafsi,
isipokuwa ahadi ya kumalizia ujenzi wa michezo Namfua.
Katika
barua hiyo, ambayo pia ameinakili kwa Rais Jakaya Kikwete, Katibu
Baraza la wadhamini CCM Taifa, Katibu wa Uchumi na Fedha na Katibu wa
CCM mkoa wa Singida, Dewji amedai kuwa kila alipotaka kufanya hivyo
alipata vikwazo kutoka kwa viongozi wa CCM mkoa wa Singida.
Katikati ya kiwanja chenyewe.
Amesema
kuwa matayarisho yote muhimu kuhusiana na ujenzi huo yapo tayari, ikiwa
ni pamoja na kuwepo dola za kimarekani 880,000 (sawa na sh bilioni
1.46) ambazo kwa kushirikiana na Rais Kikwete aliweza kuzipata kutoka
Makampuni ya Airtel Tanzania na Mohammed Ent (T) Ltd.
Dewji
amesema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 yeye pamoja na
Raisi Jakaya Kikwete walitoa ahadi ya kukarabati na kuweka nyasi za
bandia kwenye uwanja huo unaomilikiwa na chama cha mapinduzi CCM.
Hili ni jukwaa kuu la uwanja wa Namfua unaomilikiwa na CCM Mkoa wa Singida.
“Baada ya uchaguzi sote wawili tulishinda na sasa tunatumikia
wananchi, na kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi
kwa vipindi vyote viwili, pamoja na ahadi zetu binafsi, lakini ahadi
tuliyotoa ya ukarabati wa uwanja mpaka sasa hatujafanikiwa kuitekeleza.
Alisem MO na kuongeza Dewji amesema anasikitishwa na uongozi wa CCM
Mkoa wa Singida bila sababu za msingi wanachelewesha kuanza kwa mchakato
wa ukarabati wa uwanja huo.
Aidha
amesema kuna vikao vingi viimefanyika na makampuni hayo bila mafanikio
na hivyo anaomba CCM Makao makuu kuingilia kati ili kama kuna jambo
linasababisha kusuasua kwa mchakato huo liweze kupatiwa ifumbuzi na
ukarabati ufanyike haraka iwezekanavyo.
Vijana wakicheza mpira uwanjani humo.
Amesema
suala la uchakavu wa uwanja wa Namfua imekuwa ni kero kubwa
inayowakabili wananchi wa jimbo la singida mjini kwa sasa na hivyo
kuwanyima vijana fursa za kutumia uwanja huo ili kupata ajira na kukuza
vipaji kwa vijana. Kutokana na ukweli kwamba muda wa kuelekea Uchaguzi
Mkuu 2015 unayoyoma, Dewji maarufu kwa jina la "MO" amemwomba Katibu
Mkuu wa CCM kuingilia kati urasimu huo usio wa lazima ili ujenzi uweze
kufanyika mapema.
Akizungumzia
madai hayo ya Mbunge Dewji, Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Naomi
Kapambala alikiri kupata nakala ya barua hiyo na kusema kuwa wamefanya
matayarisho yote muhimu ikiwa ni pamoja na kufuatilia Airtel makao makuu
juu ya suala hilo.
Aidha
Kapambala amesema kuwa kamati ya siasa imemaliza kazi na kupeleka
baraza la wadhamini, na kinachosubiriwa na baraza kukaa ili kutoka
majibu.
“Mi
namshangaa ni kwa nini yeye mwenyewe Dewji hajafika hapa ofisini na
kupata ufafanuzi juu ya hili matokeo yake analeta nakala ya barua kwetu,
akamwulize katibu Mkuu ambaye amemwandikia hii barua.” Alisema
Kapambala Hata wakati katibu mkuu alipokuja hapa tulimweleza juu ya hilo
, yeye kama anaonaje ni vyema akafika ofisini ili kujua inachoendelea.
Sehemu ya jukwaa la uwanja wa Namfua linalotumiwa na washabiki likiwa linaonekana kuchakaa.
Aidha
Kapambala amesema Katibu mkuu msaidizi yuko jijini Dar es Salaam ambapo
pamoja na mambo mengine wamemwagiza kupitia baraza la wadhamini wa CCM
ili kujua hatma ya suala hilo. Pia Kapambala amesema pia ofisi yake
imekwishatoa notisi kwa wafanyabiashara mbalimbali kuondoka kwenye eneo
la uwanja ili kupisha ukarabati huo.
Mwenyekiti
wa SIREFA Baltazari Kimario alisema anasikitishwa kuona maendeleo ya
uwanja huo bado haujakamilika na hivyo kuathiri maendeleo ya soka katika
mkoa wa singida.
Aidha
wadau mbalimbali nao wametoa masikitiko yao kwa uongozi wa CCM Mkoa wa
singida kuchelewesha mchakato huo kwa maslahi binafsi, huku Mbunge
akiwa tayari kushughulikia kero hiyo. Uwanja huo hivi sasa umebaki kuwa
kama eneo maarufu la vijana kuvuta bangi na wengine kujisaidia hovyo
kwenye vyoo na hivyo kutapakaa kwa vinyesi kila mahali ndani ya uwanja
huo.
Ujenzi
wa Uwanja wa Namfua,ambao ulikuwa ukienda sambamba na Jengo la CCM
mkoa, ulisimama miaka ya 1990 na tangu wakati huo uwanja huo umebakia
gofu na kugeuka maficho ya wahalifu mbalimbali na eneo la choo cha
jumuiya.
Baadhi ya Waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida wakipiga picha jengo la makao makuu ya CCM Mkoa wa Singida.
Vijana hawa walikutwa wakivuta bangi kwenye majukwaa ya uwanja wa Namfua.
Hapa ndio makao makuu ya CCM Mkoa wa Singida.(Picha zote na Hillary Shoo).
No comments:
Post a Comment