N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Thursday, August 14, 2014

ZANZIBAR YAIKARIBISHA UJERUMANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133.
Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke na Rais SheinSERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imeiomba Serikali ya Ujerumani kupanua uwekezaji katika nyanja za viwanda vidogo vidogo pamoja na bahari kuu ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Makamu wa kwanza wa Rais wa  Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad  alitoa ombi hilo alipokutana kwa mazungumzao na Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke  aliyefika kwa ajili ya kujitambulisha.
Maalim Seif alisema miongoni mwa matatizo makubwa yanyoikabili Zanzibar kama nchi nyingine za Afrika ni vijana wengi kukosa ajira na shughuli za kujiletea maendeleo, hivyo Ujerumani inayo nafasi kubwa ya kupambana na jambo hilo.
Hata hivyo, alisema miongoni mwa njia muafaka ya kuweza kufanikisha azma hiyo, ni nchi hiyo kuelekeza nguvu zaidi katika kusaidia elimu ya amali ambayo itawawezesha vijana wa Zanzibar wakiwemo wale wanomaliza masomo kuweza kupata mbinu za ajira.
Aliongeza kuwa Zanzibar imeweza kupiga hatua kubwa katika sekta ya elimu lakini bado inayotolewa haijakuwa na ubora unaowezesha vijana kukabiliana na changamoto za uhaba wa ajira.
Seif alisema fursa nyingine muhimu za ushirikiano kati ya nchi mbili hizo ni katika sekta ya utalii na kilimo.
Naye Balozi Konchanke alisema amepokea maombi hayo na yatazingatiwa katika mipango ya ushirikiano wa nchi yake na Tanzania.
Alisema anaelewa kuwa Zanzibar inazo fursa muhimu za kiuchumi na biashara, ikiwemo kilimo cha viungo na utalii ambazo wawekezaji wa Ujerumani wanaweza kuzitumia katika kufungua miradi yao.
Alisema kuwa atakuwa balozi katika kuiuza Tanzania na Zanzibar kwa wawekezaji wa Ujerumani kwani wanaweza kuzitumia kwa kufungua miradi yao.
Chanzo:Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment

Blog Archive