N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Thursday, August 14, 2014

Nacte Inter College TANZANIA Debate Competition

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133.

Mratibu wa Tamasha la Vyuo vya Elimu ya Kati Tanzania( NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014-2015, Bi, Magreth Kilawe,(kulia) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari. kuhusiana na Michezo hiyo katika Vyuo vya NACTE TANZANIA

Mashindano ya Mijadala kwa kwa vyuo vya Elimu ya Kati kwa kanda ya Dar es Salaam, yanatarajiwa kuanza Novenber mwaka huu.
Akizungumzia katika semina elekezi, iliyowakutanisha baadhi ya walimu wa mijadala kutoka katika  Vyuo mbalimbali, Mratibu wa Tamasha la Nacte Inter College Tanzania 2014/2015, Magreth Kilawe, kutoka Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo, Bi Magreth Milawe, amesema jumla ya Vyuo 33 kutoka Kanda ya Dar es Salaam,Vimeshathibitisha ushiriki wao katika Tamasha hilo ambalo ni la kwanza kufanyika Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Mratibu wa Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015

: Bi, Magreth Kilawe


Bi, Magreth, amesema Tamasha hilo pia litaonyeshwa kwenye moja ya runinga hapa nchini kuwapa fursa watazamaji kushuhudia vipaji vya wanafunzi katika kujieleza mbele ya jamii.
Amesema nia na madhumuni ya Tamasha hilo, mbali na kuondoka na kitita cha zawadi kwa washindi lakini pia ni njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu hapa nchini kwa wanafunzi kupata nafasi ya kujieleza mbele za watu, kufanya utafiti kutokana na mada itakayowekwa mezani, kuweka mahusiano mema dhidi ya wanafunzi na kujenga kizazi kipya katika nyanja ya elimu kupitia mfumo wa mijadala.

Bi, Magreth Kilawe(kulia) kushoto ni Mwakilishi wa Viongozi Serikali ya Wanafunzi Mr.Stephano

Vyuo vilivyojitokeza mpaka sasa miongoni mwa vyuo 105 kushiriki Tamasha hilo mpaka sasa ni
26.Lugalo Military Medical School - Dar es Salaam 
32. Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) - DSM
Kwa Mujibu wa Bi, Magreth,nafasi za ushiriki bado zipo kwa vyuo ambavyo bado havijathibitisha ushiriki na kwamba mwisho wa Usajili ni tarehe moja mwezi wa tisa mwaka huu.
Maandalizi yanaendelea vizuri mpaka sasa tunaendelea na mazungumzo na wadhamini na ambao tayari wameonyesha nia ya kusaidia Michezo hii ya NACTE katika vyuo vya Elimu ya Kati ni Pamoja na N.M.B, P.S.P.F, TCRA,AZAM, CXC TOURS,PCCB,LAPF,TAHA, BANK YA POSTA,MALT MEDIA GROUP, NSSF,TTCL,FAST-JET,IKONDOLELO LODGE, Global Publishers, East Afrika Radio Radio & TV,Clouds Media Group"pamoja na mtandao wa www.shaabanmpalule.blogspot.com(FULL UTAMU-JUMWAGE), ameongeza Bi, Magreth
Michezo mingine katika tamasha hilo ni pamoja na Soka, Netball,Basketball,Handball, Voleyball, Marathoni,Vipaji vya Utangazaji,Mashindano ya DJ's, Shindano la Mavazi ya Ofisini,Uongozi na Utawala, pamoja na Vipaji vya Kuimba (Muziki).
Fulsa hiyo ya uwepo wa michezo kwenye vyuo vya elimu ya kati Tanzania, imekuja baada ya hitaji la muda mrefu kutoka kwa wanafunzi waliokuwa wakitoka kwenye Shule za Sekondari kujiunga katika Vyuo vya Elimu ya Kati, ambapo walikuwa hawapati fulsa ya kukutana kimichezo katika kubadilishana mawazo na kutengeneza mahusiano mema miongoni mwa Wanafunzi, Walimu na Wadhamini.
Hata hivyo Bi, Magreth amesisitiza kwamba, wakati wa Tamasha Msisimko mkubwa utakuwa kwa washiriki wa Mijadala(Debate Competition)na kwamba baada ya kukamilika tamasha la Kanda ya Dar es Salaam, itafuata Kanda ya Mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Zanzibar,katika kipindi cha 2014/ 2015.
Michezo yote itachezwa kwenye viwanja vilivyopendekezwana Kamati Kuu ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, mbavyo ni
The Mwalimu Nyerere Memorial Academy, University of Dar es Salaam, TCC Chang’ombe, Kibaha Secondary, Gymkhana Posta, na Leaders Club.

No comments:

Post a Comment

Blog Archive