N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Wednesday, January 7, 2015

LHRC: WATANZANIA WOTE WANA HAKI YA KUJADILI KATIBA,WASIZUIWE!

Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) chenye makao yake jijini Dar Es Salaam,kimewataka wajumbe wa bunge maalum la katiba kuacha tabia ya kuwafumba midomo wananchi wanaotoa maoni yao kuhusiana na mchakato mzima wa kuandika katiba mpya nchini Tanzania.BISIMBA
Akiyasema hayo leo asubuhi akiongea na waandishi wa habari,Mkurugenzi Mtendaji,Dr.Helen Kijo-Bisimba alisema,”Bunge linaposema wananchi waache kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya ni kwenda kinyume na katiba ya nchi yetu,ibara ya 18 na 21 kifungu cha pili”. Alisisitiza kuwa kwenye katiba ya Tanzania, ni haki ya kila raia kutoa ama kupokea taarifa na ni wajibu wake pia kuzitumia taarifa hizo kwa maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi-Mtendaji-Ananilea-Nkya
Kwa upande wa Bw.H.Sungusia na Bi.Ananilea Nkya waliongezea kwa kushauri kuwa bunge hili lisimamishwe na lisiendee kwani limekosa uhalali wa kisheria,kisiasa na kuna wasiwasi wa kupoteza pesa nyingi kwenye kitu ambacho kinajulikana wazi kitakataliwa na wananchi.
“Wananchi tusimamie ukweli, tupaze sauti zetu na twende juu ya vyama vyetu,juu ya familia zetu na tuweke maslahi ya nchi mbele”,alisema Bi.Ananilea. Aliyasema hayo akisisitiza kuhusu usimamishwaji wa bunge maalum la katiba na kuwasihi wajumbe hao wajali watanzania kuliko kujali “matumbo yao”. Aliongezea kwa kusema,”anayezorotesha mchakato huu hafai kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi,kwani Rais na Jaji Warioba wameshamaliza kazi zao”
Sungusia   Kwa upande wa kuomba msaada kutoka mahakamani ili kusitisha bunge hilo,mwanasheria Bw.Sungusia alisema ni jambo linalohitaji umakini zaidi kwani ni kama wapo mtegoni. “Ndugu waandishi,kuna kesi nyingi sana zipo mahakamani tangu 2008 lakini hakuna uamuzi uliochukuliwa,tunasita kupeleka suala hili mahakamani kwani hatujui uamuzi wake utatolewa lini na litakuwa na faida na hasara kwa kiasi gani”.
Mkutano huu wa waandishi wa habari uliitishwa na LHRC pamoja wadau wake wa karibu ikiwemo asasi ya vijana ya Tanzania Youth Vision Association (TYVA) iliyowakilishwa na Bw.Naamala Samson ambaye ni mratibu wa mradi wa FURSIKA NA AJIRA.
Unaweza kupakua tamko zima hapa: TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI- MWENENDO MCHAKATO WA KATIBA 7-8-2014
By ijuekatiba

LHRC YATOA MACHAPISHO KUHUSU KATIBA KWA TYVA

LHRC Logo
Katika kutambua mchango wa asasi ya Tanzania Youth Vision Association(TYVA) kuwafikia vijana na kuwaelimisha kuhusu kuifahamu katiba, rasimu za katiba na kuwawezesha kutoa maoni yao kuhusu haki wazitakazo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimetoa machapisho kwenye maboksi zaidi ya 31.
Machapisho kutoka LHRC
TYVA inaendesha mradi wa IJUEKATIBA unaolenga kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wao kwenye kufuatilia mchakato mzima wa katiba. Mradi huu ulioanza tangu mwaka 2011 umeshafikia vijana milioni tano walio kwenye mikoa zaidi ya 18 Bara pamoja na Zanzibar, na inatarajiwa utawafikia walio kwenye mikoa zaidi mijini na vijijini, mashuleni na mitaani kwa njia mbalimbali za midahalo,mafunzo na vyombo vya habari.
Machapisho ya katiba
Randama za Katiba
Shukrani za dhati ziufikie utawala mzima wa Kituo cha Sheria na Haki Za Binadamu kuunga mkono zinazofanywa na TYVA.
By ijuekatiba

MDAHALO WA KATIBA KUFANYIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Muungano wa Asasi za Kiraia Tanzania umeandaa Mdahalo wa wazi kuhusu Changamoto za Mchakato wa Katiba mpya. Mdahalo huo utafanyika tarehe 31 /5/2014 katika Ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 10.00 Jioni. Mdahalo huo utatangazwa moja kwa moja na vituo vya ITV, ABM Radio ya Dodoma, pamoja na Chuchu FM na Istiqama Radio za Zanzibar. Vyombo vingine vya habari vitakavyopenda kuutangaza Mdahalo huu kwa maslahi ya umma pia vinakaribishwa.
Watoa Mada ni waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba: Prof. Mwesiga Baregu na Bw. Awadhi Ally Saidi.
Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika mdahalo huu ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata katiba mpya inayokidhi maslahi ya watanzania.
Wote Mnakaribishwa na HAKUNA KIINGILIO !!!
By ijuekatiba

RAIS KIKWETE AWAASA WAJUMBE KUANDIKA KATIBA BORA!

RAIS Jakaya Kikwete, amelihutubia Bunge Maalum la Katiba na kuwapongeza Wabunge wa Bunge hilo na kusisitiza kuwa Mchakato wa kupata Katiba Mpya, unahitaji umakini wa ziada ili Watanzania Wapate Katiba inayotekelezeka isiyo na Masharti Magumu.



Aidha amewatahadharisha Wajumbe hao kuwa Makini katika Mchakato wa kupata Katiba Mpya , ili isije ikakataliwa na Wananchi, kwani hatua ya maamuzi katika suala hilo imeanzia kwenye Bunge hilo na mwisho kwenda kwa Wananchi kupigiwa kura ya kukubalika na hivyo wajiridhishe na Uandishi uliopo kwenye Rasimu hiyo.

“Kile mtakachoona kinafaa kurekebishwa au kufutwa msisite kikuondoa! Tunachotaka ni ili Watanzania wapate Katiba iliyo nzuri ila tunaweza kupata wakati mgumu kuitekeleza msipozingatia mambo muhimu, Bunge hili linawajibu wa kuzuia jambo hilo ili lisitokee katika Nchi yetu”

Alisema kwasababu Rasimu hiyo ina mambo mengi Wajumbe hao wafanye Uchambuzi kuhusu kufaa kwake na manufaa yake, ili isije kuwaumiza Wananchi, huku akitolea mfano wa kipengele kinacho mwekea Mbunge kizuizi cha Miezi (sita) kuingia Bungeni au kushiriki shughuli za Kibunge endapo atakuwa gerezani au kuugua kwa kipindi hicho, jambo ambalo amependekeza kuwa kipengele hicho wakijadili kwa kina kwani kinaumiza watakao wekewa vizuizi kutokana na kuwa magonjwa hayaepukiki kwa maisha ya Mwanadamu.

Ukomo wa Wabunge

Aidha amesema kuhusu suala la Kikomo kwa Wabunge kuongoza kwa mda wa Miaka Mitatu, yeye binafsi katika kifungu hicho, ambacho kipo kwenye Rasimu ya pili ya Katiba ameona kina utata kwa vile haijaelezwa kama ni awamu mbili mfululizo au la! Hakuna Nchi Duniani iliyoweka ukomo wa Wabunge na hivyo kupendekeza Ukomo huo uwe kwa Viongozi wa Wakuu wa Serikali.

Muundo wa Muungano

Alisema pendekezo hilo, limesababisha kujaa kwa mijadala mirefu kuanzia kwenye Rasimu ya Kwanza na ya pili, na kuleta hisia kwa pande zote mbili katika upande wa Muungano ulipo hivi sasa, na kuwaomba Wajumbe hao kuwa wawe watulivu ili wanapolijadili, wasiwe na ‘Jazba’ kwani wakitumia nguvu Zaidi hawatafika popote.

“Waasisi wa Tifa letu Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume waliamua kuchagua Mfumo wa Serikali mbili ili Tanganyika kuepuka gharama kwa Tanzania Bara kugharamia serikali ya bara na ya Muungano, nafikiri tuzingatie mawazo ya Wazee hao” alisema Dk Kikwete

‘Tume imependekeza kuwepo Kwa Muundo wa Serikali tatu, kwa kuwa itakuwa endelevu kutokana na Muundo uliopo sasa wa Serikali mbili”

Apigia debe Serikali mbili

Alisema kuna hatari ya Nchi kushindwa kujiendesha kukiwa na Muundo wa Serikali tatu ambapo alisema uamuzi wa kuwa na Serikali mbili au tatu uko mikononi mwa Wajumbe hao, na lazima waweze kupitia Ibara kwa Ibara, Sura kwa Sura na Neno kwa Neno, ili wakichagua Serikali tatu, wayaondoe mambo yatakayokuwa vikwazo kwa Nchi washirika, kwani kama watapitisha Muundo wa Serikali mbili hakutakuwa na tatizo.

Hata hivyo alisema Muundo wa Serikali tatu Tume ilipendekeza kuwa utumike kutokana na maoni ya Wananchi, ila mipaka ya Madaraka haijawekwa katika kipengele hicho na upande wa mapato ambayo hayajawekwa bayana na kusababisha malalamiko ambayo yamekuwepo kwamuda mrefu.

Anasema kuwa mjadala wa Muundo wa Katiba sio jambo geni kama alivyoeleza Juzi Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kwani Mwaka 1984 ulikuwa chanzo cha Machafuko Zanzibar. Pia mwaka 1993 jambo hilo lilikuwa ni chanzo na G55.

Rais Kikwete amehutubia Bunge hilo, kwa mujibu wa kanuni ya 75 (1), inaeleza taarifa ya Katibu wa Bunge la Katiba, ambapo Viongozi wa Kitaifa wameingia Bungeni kwa maandamano wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Chanzo: FIKRA PEVU | KISIMA CHA BUSARA
By ijuekatiba

BUNGE LA KATIBA LAPATA WENYEVITI NA MAKATIBU

Na Naamala Samson,
Baada ya kuendeshwa kwa zaidi ya wiki tatu bila mwenyekiti wa kudumu wala kujadili rasimu ya katiba,sasa bunge maalum la katiba litaanza kujadili vipengele na ibara mbalimbali zilizomo ndani ya rasimu ya katiba kwani wajumbe wa bunge hili muhimu wameweza kufanya uchaguzi na kumchagua Mhe. Samwel Sitta awe Mwenyekiti wa kudumu wa bunge hili kwa muda uliosalia mpaka kupatikana kwa katiba mpya kabla ya katiba hiyo kurudi kwa wananchi kupigiwa kura.
Image
Kwa kitendo hiki kilichokuwa kinangojewa kwa hamu kubwa na wananchi, inatarajiwa sasa kusikia kama wajumbe wataweka maslahi ya taifa mbele au watajali tu maslahi yao binafsi na kuweka utaifa nyuma.

Ikumbukwe kuwa mashirika mengi yalikuwa yanapigia kelele suala zima la wajumbe hawa kutoangalia ubinafsi wao bali kuwaza taifa zima na kutengeneza katiba kwa ajili ya vizazi vijavyo ili Tanzania iwe nchi inayopiga hatua kwa kasi.
By ijuekatiba

ASASI YA VIJANA YA TYVA KUFANYA BARAZA LA KATIBA TAREHE 17 AGOSTI 2013

Image

Dear All,
TYVA is humbly inviting you to attend the Youth Constitutional Council to be held on Saturday 17th August 2013 at Peacock Hotel City Centre Mnazi Mmoja, Dar es Salaam from 08:00am to 4:00pm
The main Goal of the Youth Constitutional Council is to facilitate the collection of youth views on the recently released first draft of constitution, towards the process of writing the new constitution of United Republic of Tanzania.
TYVA will provide breakfast, Lunch Break and all refreshments during the conference. To show your commitment, TYVA request you to cover your own transport to and from the conference at Mnazi mmoja and we will NOT give any transport and sitting allowances to the participants.
Please confirm your participation by sending your Full name to Alfred Kiwuyo by Phone or Email before 14th August, 2013 for farther logistics arrangements. Should you have any questions, please do not hesitate to contact us through the addresses below.
Looking forward to have you on 17th August, 2013
Alfred Kiwuyo, 
Head, Lobbing, Advocacy and Networking (LAN)
akiwuyo@yahoo.ca 
+255 713 618 388 
Tanzania Youth Vision Association
By ijuekatiba

Mhe. Samuel Sitta afungua rasmi Baraza la Vijana la Taifa la Katiba leo jijini Dar es Salaam.

Na Benedict Liwenga.
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashiriki, Mhe. Samuel Sitta amewaaasa vijana kutoa maoni yao juu ya uundwaji wa Katiba mpya ambayo haijengi mifumno ya serikli ya Udikteta, ubinafsi na ambayo haitaibebesha mzigo Serikali.
 
Image
 
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mhe. Sitta wakati akifungua rasmi Baraza la Vijana la Taifa la Katiba lililoandaliwa na Taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Coalition (TYC) kwa kushirikiana na Restless Development, UNFPA na ILO lililojumuisha vijana 120 kutoka Wialaya 50 za mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na ambao wanatoka katika mashirika mbalimbali, asasi, jumuiya na vikundi mbalimbali vya vijana.
 
Waziri Sitta amewaasa vijana kuwa TYC pamoja na vijana wengine nchini wanalojukumu kubwa la mapambano dhidi ya kupinga ulafi katika mambo ya uongozi, udikteta pamoja na ubinafsi kwani vinailetea mzigo serikali.
 
“Mtu ajue kuwa kutumia madaraka kwa manufaa yako mwenyewe ni mwiko”. Waziri Sitta alisema.
 
Waziri Sitta ameongeza kuwa vijana nchini wanatakiwa wawe Wanaharakati katika kujali maadili mema na kusimamia kwa dhati pamoja na kupigania haki na usawa nchini.
 
Image
 
Aidha, kwa upande mwingine Waziri Sitta amevishukuru vyombo vya habari kwa mchango wake mkubwa wa kufanya kazi ya kuhabarisha umma na npia ameipongeza taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Coalition kwa kuandaa baraza hilo kwa vijana wenzao kwani litawasaidia kutambiua mabo ya msingi yanayohitajika kuwepo katika Katiba mpya ya nchi.
 
Waziri Sitta alisema kuwa katika kutoa maoni juu ya Katiba mpya, vijana wanaweza kupata katiba yenye manufaa mazuri au yenye athari kwa maisha yao, hivyo amewaasa vijana wote watumie fursa wanazozipata kupitia baraza hilo lililoandaliwa na TYC ili waweze kusikika katika mambo yanayohitajika katika Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Coalition ni moja ya taasisi iliyoundwa kwa malengo ya kuhakikisha kuwa vijana wanashirki na kushirikishwa katika mchakato wa kuunda katiba mpya ulioanza mwaka jana hapa nchini.
 
Image
 
By ijuekatiba

VIONGOZI VIJANA WA YLTP 2013 WATOA MAENEO SITA YA KUZINGATIA KWENYE KATIBA

Image
Washiriki vijana katika mjadala kuhusu rasimu ya katiba.
Katika kuendelea na mchakato wa kutoa maoni kuhusu rasimu ya KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vijana wapatao 25 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wanaoshiriki mafunzo ya uongozi yanayotolewa na Shirika la Kijerumani la Friedrich Ebert Stiftung(FES) wamefanya mjadala wa siku mbili wa kujadili rasimu hiyo na kutoa maeneo sita wanayoona yanatakiwa kupewa uzito katika kupata katiba mpya.
Maeneo hayo sita ni:
1.Kuimarisha vyombo vya kusimamia uwajibikaji.
2.Suala la umiliki wa Ardhi
3.Usimamiaji na ugawanyaji wa rasilimali.
4.Kutajwa kwa lugha ya kufundishia
5.Kutajwa suala la serikali za mitaa 
6.Mfumo mzima wa kubadili katiba hii kwenda mpya.

Image
Dr.Ayoub Rioba akitoa mada katika mjadala wa rasimu ya katiba katika ofisi za FES.

No comments:

Post a Comment