Mnamo tarehe 31 Oktoba 2010, Watanzania walishiriki katika uchaguzi wa
Rais wa Muungano, Rais wa Zanzibar pamoja na Wabunge na Wawakilishi
katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Huu ni mjumuisho wa yale
yaliyojiri katika blogu mbalimbali kuhusiana na uchaguzi huo.
Hata kama vyombo vya habari vya Tanzania vinahisi kwamba viko huru kuripoti kuhusu mkabiliano mkali uliopo kwenye mbio za uchaguzi, hili ni jambo lingine. Kuchapisha habari zinazoikosoa serikali katika kipindi hiki nyeti ilionekana kuwa jambo lenye hatari kubwa hasa baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sethi Kamuhanda, kutembelea ofisi za vyombo mbalimbali vya habari, ambapo alitishia kuvifunga vyombo vya habari “vinavyochapisha habari zinazoifanya serikali ionekane katika mwanga mbaya,” televisheni ya taifa iliripoti. Zaidi ya asasi 50 za haki za binadamu na vyombo vya habari vilitoa tamko la pamoja, vikidai kwamba serikali imevitishia vyombo vya habari mapema kabla ya uchaguzi huo.Inaendelea....
Tangu kampeni zilipoanza, Msajili wa Magazeti, shirika linalomilikiwa na serikali ambalo linasimamia utoaji leseni, lilikuwa likiandika barua na kuzituma kwenye magazeti mbalimbali, na kuyaonya dhidi ya kuandika habari yoyote inayoonekana kuikosoa serikali, waandishi nchini humu waliiambia CPJ. Magazeti matatu ya kila wiki ya Mwanahalisi, Raia Mwema na Tanzania Daima, tayari yaliweza kupokea barua za onyo kwamba hayana budi kukwepa kuandika habari zozote ambazo serikali itaziona kuwa ni za “uchozezi” vinginevyo yangeweza kusimamishwa.
“Aina hii ya vitisho imekuwa jambo la kawaida kusikia kutoka kwa Msajili wa Magazeti, ambaye waziri wa habari humtumia kama chombo cha kuhakikisha waandanishi wanachuja na kujizuia kuandika habari fulani wao wenyewe,” mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda,wakati huo alijikuta akiingia kwenye Hatari kubwa ikiwa ni pamoja na kumwagiwa Tindi kali pamoja na wahariri wengine kama Said Kubenea.
Gazeti la Kiswahili linaloongoza kwa kuwa na wasomaji wengi, Mwananchi, pia lilipokea barua mbili kutoka kwa Msajili huyo zilizotishia kulifunga kwa kuwa liliripoti habari ambazo ziliikosoa serikali, Mhariri Mtendaji, Theophil Makunga, alithibitisha.
No comments:
Post a Comment