Friday, May 20, 2016
Monday, May 16, 2016
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA UHAULISHAJI FEDHA KWA JAMII AFRIKA
SERA YA TEHAMA YA 2016 KUSAIDIA TANZANIA KUINGIA KATIKA UCHUMI WA KATI MWAKA 2025.
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya Nchi
wameifanyia maboresho Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya
mwaka 2003 na kuja ya sera mpya ya mwaka 2016 ili kuunganisha sekta
muhimu za uzalishaji na viwanda katika miundombinu ya TEHAMA.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi
wa Sera ya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016.
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuiwezesha Tanzania kutumia fursa
zinatokana na uwepo wa miundombinu ya TEHAMA kuingia katika uchumi wa
kati ifakapo 2025 kwa kuimarisha matumizi ya TEHAMa katika sekta
mbalimbali za uzalishaji nchini.
Mhe. Ngonyani aliongeza kuwa Sera hiyo ni muhimu katika kujenga jamii
habari itakayowezesha nchi kufikia maarifa yatakayosaidia kwenda
sanajari na mpango wa Taifa kujenga uchumi wa viwanda.
Alisema kuwa Sera hiyo imejikita katika kukuza matumzi TEHAMA katika
uzalishaji ili kuongeza tija , kukuza utafiti na kuvutia uwekezaji wa
sekta binafsi katika TEHAMA kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa
kwa ujumla.
Awali akiongea kabla ya uzinduzi wa Sera hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Mawasiliano) Profesa Faustin
Kamuzora alisema kuwa Sera hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji
wa kazi wa kila siku katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema kuwa sera hii itasiaidia kwenda sanajari ya ukuaji wa kasi wa matumzi ya mawasiliano hapa nchini.
=======================================================
MATUKIO BUNGENI LEO.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) pamoja
na Mbunge wa Viti Maalul CCM, Mhe. Halima Bulembo wakielekea Bungeni
kwa jili ya vikao vya asubuhi vya Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini
Dodoma.
==============================================
Sunday, May 15, 2016
SAFARI YA MWISHO YA MWANETU MAGGID MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KITUO CHA KISASA CHA HUDUMA ZA MAGARI MKOANI ARUSHA
WIZARA KUPIMA VIWANJA 2180 CHASIMBA
Bi Senje
aliongeza kuwa kazi ya kupima viwanja hivyo ilianza mwezi Agosti mwaka
jana baada ya Wizara kuunda timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Wakala wa
Barabara Nchini (TANROADS) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) ili waweze kutambua mipaka ya eneo kwa ajili ya kuweka
miundombinu.
Aidha,
Bi. Senje amesisitiza kuwa wananchi wawe wavumilivu kwani huduma za
miundombinu kama vile maji, umeme na barabara zitawekwa baada ya upimaji
wa viwanja hivyo kukamilika.Mgogoro huo ulimalizika mnamo Juni 13 mwaka
jana baada ya uongozi wa Wizara kuweka kikao na uongozi wa Kiwanda cha
Saruji pamoja na wananchi wa Chasimba ambapo uongozi wa Kiwanda
ulikubali kuachia sehemu ya ardhi ambayo ilishaendelezwa na wakazi wa
eneo hilo kwa makubaliano ya kupewa fidia na Wizara.
LUHWAVI AWASILI TANGA LEO, ASIKILIZA MAFANIKIO NA KERO ZA WAFANYAKAZI WA CCM WILAYA ZOTE ZA MKOA HUO
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akisalimiana na Kada wa CCM, Mkuu wa
mkoa wa Tanga Martine Shigella, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Tanga, Shija Othman
Vijana wa
Umoja wa CCM mkoa wa Tanga, wakimfanyia mapokezi maalum, Naibu Katibu
Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
Vijana wa
Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Tanga, akila kiapo cha utiifu wakati
walipomfanyia mapokezi rasmi Katibu Mkuu wa CCM- Bara, Rajabu Luhwavi,
alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama
kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
Kijana wa
wa UVCCM, Mwanakombo Mwakulo akimvisha Skafu Naibu Katibu Mkuu wa CCM
-Bara, Rajab Luhwavi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na
watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. Kulia ni kada wa
CCM Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella.
UPDATES ZA MSIBA WA MTOTO WA ANKAL: MWILI UMESHAWASILI DAR ES SALAAM, MAZISHI LEO JUMAMOSI SAA 10 ALASIRI MAKABURI YA KISUTU
Updates
za familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na
Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin (18), aliyefariki Jumapili Mei 8, 2016
huko Durban, Afrika Kusini:
Subscribe to:
Posts (Atom)