Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Joseph Nyamhanga
amewataka watumiaji wa Daraja la Nyerere (Kigamboni) kuzingatia
matumizi bora na sahihi ya daraja hilo ikiwemo usafi ili kuliwezesha
kukidhi matarajio ya serikali na kudumu kwa muda mrefu.
Akizungumza
katika kikao maalum cha wadau kutathimini viwango vya tozo
vitakavyotumiwa katika daraja hilo Eng. Nyamhanga amewataka waendeshaji
wa daraja hilo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuimarisha huduma ya
ulinzi na usalama na kuwataka watumiaji wa daraja hilo kutumia fursa za
uwepo wake kiuchumi na kijamii.
“Hakikisheni tozo zitakazowekwa
ziwiane na hali ya maisha ya wananchi ili kuwavutia wengi kupita katika
daraja hili na kupunguza msongamano katika vivuko”, amesema Eng.
Nyamhanga.Tozo hizo ambazo zitaanza kutozwa kwa watumiaji wa Daraja la
Nyerere hivi karibuni zinalenga kuwezesha NSSF kurudisha gharama za
uwekezaji katika daraja hilo.
Aidha, Katibu Mkuu huyo amesema
hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhujumu
miundombinu na kukemea vitendo vya watu kufanya biashara katika daraja
hilo.Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara amesema tozo
kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere itaanza hivi karibuni baada ya
kupitishwa na Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
hivyo amewataka watumiaji wa daraja hilo kutoa ushirikiano kwa watendaji
ili kuwezesha huduma kufanyika kama ilivyokusudiwa.
“Tumejipanga
Vizuri na tutaanza kutoza watumiaji wa Daraja la Nyerere muda mfupi
kuanzia sasa.” amesema Prof. Kahyarara.Zaidi ya shilingi Bilioni 214
zimetumika katika ujenzi wa Daraja la Nyerere ambapo asilimia 60
zimegharamiwa na NSSF na asilimia 40 zimegharamiwa na Serikali Kuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)
Eng. Joseph Nyamhanga (katikati) akitoa ufafanuzi kwa wadau mbalimbali
wa sekta ya usafirishaji katika kikao cha kujadili viwango vya tozo
zitakazotumika katika Daraja la Nyerere (Kigamboni). Kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof Godius Kahyarara na
kushoto ni Mkurugenzi wa barabara (Ujenzi) Eng. Ven Ndyamukama.
Mkurugenzi wa Barabara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.
Ven Ndyamukama (Kushoto) akifafanua jambo katika kikao cha wadau
kujadili tozo za matumizi ya Daraja la Nyerere (Kigamboni). Kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawsiliano Eng, Joseph
Nyamhanga
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius
Kahyarara (kulia) akitoa taarifa ya namna tozo zitakavyokusanywa kwa
wadau mbalimbali wanaotumia Daraja la Nyerere zoezi litakaloanza hivi
karibuni.
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli akitoa maoni ya namna ya
kuwahudumia waendesha baiskeli katika kikao cha kujadili tozo
zitakazotumika kataka Daraja la Nyerere.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kujadili
tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyerere, Tozo hizo zitatangazwa
hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment