SERIKALI YAPATA BILIONI 1.71 KUTOKANA NA MAONESHO YA VITO JIJINI ARUSHA.
Wizara
ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa
madini Tanzania (TAMIDA) iliendesha Maonesho ya tano ya Kimataifa ya
Madini ya Vito yaliyofanyika Jijini Arusha katika Hoteli ya Mount Meru
kuanzia tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016. Maonesho haya hufanyika kila
mwaka Jijini Arusha na hukutanisha washiriki mbalimbali ikiwa ni pamoja
na Wachimbaji, Wafanyabiashara wa madini ya vito wa ndani na nje,
wanunuzi wa madini wa ndani na nje, na wataalam mbalimbali wenye uzoefu
wa shughuli za madini ya vito.
No comments:
Post a Comment